Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Iwe kwa US RUSSIA NATO
Suala lakuivamia nchi nyengine bila yasababu halikubaliki nawala sio lakushadidiwa wala lakuungwa mkono nahalifai hata robo!!!
Nina imani ulifanya hivyo hata Iraq, Afghanistan, Syria na Libya vinginevyo shule zifunguliwe tu tupumue
 
Aisee mkuu umemaliza kila kitu,na kwny ile post ya mkuu Galip S-22 alivyoeleza Ni kwanini Russia haimalizi Vita haraka na Ni kwanini haiwafungii mabomba yake ya gas EU nilizidi kupanuka mawazo.

Kwa Hii generation yetu propaganda za wazungu zitafeli big big time na hii Vita ita-prove hilo,nadhani watakuja na silaha nyingine lkn silaha ya propaganda ishafeli hio.

From Uni-polar to Multi-Polar.Imeisha hio
Kabisa MKUU hapo Galip S-22 alinena sanaa
Kuhusiana na propaganda jamaa washafail hiki kizazi sio kama hivyo vilivyopita
Kizazi hiki wakiharibu kwalaana nyengine sio propaganda
Kama uliliona hili saga la mauaji ya BUCHA kule kwenye media zao kila wakiweka post watu wanakuja na fact IRAQ mlivamia kwauongo kama huo mara CONGO wanakufa zaidi ya hao hamsemi wengine wanaenda mbali zaidi wanasema kama kufa acha wafe hata wapi walikufa wanakufa hamsemi
Nahisi baad yamajamaa kuona kwenye angle ya propaganda wanafail wameamua kuwaramba BAN watu wanaokua against na PROPAGANDA zao huko kwenye social zao refer twita nk
Dunia lazima iwe na wababe zaidi ya mmoja ili ukiona US anakuzingua unamkimbilia UCHINA maana US hatakua nalakukufanya ama kuwafanya nawao ukiona huwaelewi unaenda kwa RUSSIA nae akiwa haeleweki unaelekea INDIA akizingua unaenda BRAZIL
Hii VITA watu wanakufa ila inafaida sana namabadiliko yaulimwengu kutoka kwenye ule mfumo wamtu mmoja mmoja kuelekea mfumo wa watu wengi wenye mamuzi ambayo watu watawakimbilia kwasera zao nasio ubabe wao kama wanavyofanya sasa US na WEST watu wanawaekea kabisa masharti siwapi misaada mpaka mukubali homosex si niupuuzi huuuu!!!??
 
Umeongea point nzuri sana mkuu. Na hili ndilo tunatakiwa tulipinge na si kuchukua upande na kuanza kuparuana.
Sure
Ila nadhani watu hua wanaamua kuwa na upande nakushabikia haya majambo sababu wanaona DUNIA haipo fair
Yaani akifanya US anakua sahihi ila akifanya RUSSIA anakosea
Kama hakutakua na fairness sidhanii kama hii hali itaisha ama itapungua kikubwa kutakua naushabiki kama ule wa mpira ama mtu atachagua anaeona yeye kwaupande wake angalau anafaa kusapotiwa
Ila mauaji yanatakiwa yapingwe kila UPANDE iwe CHINA kule UIGHUR iwe RUSSIA pale UKRAINE iwe US na NATO kule MIDO EAST nk
 
Nimeona mechi yenu ya kiutu uzima nami niongezee.

Kuimarisha mipaka sawa ila kumbuka kuna watu wanaoongea Russian ndani ya Ukraine.
Hawa watu walitakiwa kulindwa la Russia . Walikuwa wanateswa na wanazi.
Nafikiri nadhani ndo hayo majimbo ya Donnbas na Luha
Russian na Ukrainian ni Lugha za aina moja zote Slavic.

Idea ya kuwa Homogeneous group of people should be live under One geographical territory imepitwa na Wakati na ndio ilisababisha vita zisiishe Ulaya na Hadi WWII ikatokea..

What about Tartars in Crimea inabidi walindwe na Uturuki au wale Waislam wa China nao walindwe na Uturuki?

Hili swala la Russian speaking people kuwa sababu ya Russia kuivamia Ukraine ni utter nonsense kutolewa na Russia...

Binadamu lazima wajifunze kuishi pamoja kwa kuheshimiana, hii hoja ya Russian speaking people ndani ya Russia tuangalie Ubelgiji ambayo Ina jamii ya watu wanaongea Lugha tatu Kijerumani, Kifaransa, na Kiholland na wanaishi pamoja...

Hii ni vita ya Putin na Wala sio ya Russia, Kiev imekuwepo hata kabla Moscow haijawa nchi mji mkubwa, what if na wao wangetumia hizi hoja
 
Sure
Ila nadhani watu hua wanaamua kuwa na upande nakushabikia haya majambo sababu wanaona DUNIA haipo fair
Yaani akifanya US anakua sahihi ila akifanya RUSSIA anakosea
Kama hakutakua na fairness sidhanii kama hii hali itaisha ama itapungua kikubwa kutakua naushabiki kama ule wa mpira ama mtu atachagua anaeona yeye kwaupande wake angalau anafaa kusapotiwa
Ila mauaji yanatakiwa yapingwe kila UPANDE iwe CHINA kule UIGHUR iwe RUSSIA pale UKRAINE iwe US na NATO kule MIDO EAST nk
Ubaya hauwi wema kwa kutegemeana na anayeufanya. Ubaya ni ubaya tu. Upingwe.
 
Okey mkuu...

ina maana unapokuwa jirani na nchi kama Urusi hutakiwi kuwa imara kijeshi wakati huo huo ukawa na rafiki na nchi isiyopatana na Urusi, hichi ndicho kinachokufanya uone ni sawa Ukraine kupigwa si ndio?
Ki ulinzi hakuna nchi duniani anatamani jirani awe na nguvu sawa au kumzidi. Itakuwa uwendawazimu kumruhusu jirani unayemmudu akuletee adui mlangoni.

Hii ndio sababu Israeli inapambana kwakila njia nchi jrani yake asiwe na nguvu.

Marekani inapambana kwakutumia UN kuwazuia wengine kuwa na nguvu kama zake au kumkaribia. Yupo tayari aingie gharama kukulinda ili usiwe na nguvu

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Tuachane na Urusi na USA sijui u NATO twende katika wanachotenda field.

Urusi anaziheshimu nchi mwanachama wa NATO au nchi yenye uwezo mkubwa kivita na humuoni akizishambulia badala yake inaishambulia Ukraine sababu anajua haina uwezo mkubwa wa kudhuru raia wa Urusi ndani ya Urusi.

USA na NATO wanaiheshimu Urusi na hawajathubutu kuishambulia Urusi moja kwa moja ingawa wanampa silaha Ukraine ili kumpa uhai na uwezo wa kuendeleza mapigano huku Urusi akijua hilo na bado hapeleki mashambulizi kule kwenye kisababishi kikuu yeye anaendelea kuipiga Ukraine.

Sasa hii tafsiri yake ni kwamba hawa wawili Urusi na USA ni giants katika vita na ni bullies kwa nchi ndogo zisizo na uwezo wa kivita na wanashambulia nchi zenye uwezo mdogo kivita sababu raia wao watabaki kuwa salama nchini kwao wakati vita ikiendelea.

Hili ndilo ninalolipinga mimi. Kuwa bully kwa nchi zenye uwezo mdogo kwa sababu hazina uwezo wa kutuma bomu lenye madhara nchini kwako.

Huwa nina swali nauliza, China ingepata raisi wakafikiria kuungana na Ulaya kijeshi na USA je Urusi angeivamia? Au angetaka diplomacy itumike?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] nikiwa nasoma maelezo yako moyoni najisemea "The guy gotta pure and humble soul ila unfortunately the world is not in line as the way you look at it..."

Sitaki kukuonesha nani yuko sawa nani hayuko sawa... I don't want to claim be for you kua my perspective is TRUTH, ila ngoja nikuongezee maswali mbadala ili uendelee kujiuliza why hiki why kile.

2014 kulipitishwa azimio wanaliita pale MINSK ila miaka 8 hilo azimio halikutekelezwa na hawa Ukraine? Ushajiuliza kwanini?

Kile kilichokuwa kinaendelea hapo Donbas dhidi ya raia wa Ukraine wenye ethnity ya Russia kimefichwa hakizungumzwi na hakikupewa nafasi kabisa na hizi media pa1 na hawa viongozi w magharibi... Unaeza kujiuliza Kwanini?

All EU leaders walikuwa wana chance ya kuisadia Ukraine miaka 8 iliyopita kwa kuwashinikiza Ukraine Regime kufata na kutekeleza adhimio la Minsk. Ila walifumba macho kabisa na leo hii wapo msitari wa mbele kutuma silaha na fedha Ukraine... Unaeza kutupa sababu?

Unaeza kujiuliza kwanini western wanafanya censorship ya taarifa, na wako so aggressive na kila chombo ama individuals anayejarib kuelezea perspective tofauti na yao kwenye huu mgogoro?

Kuhusu NATO, why NATO?? Hizi nchi zinaungana kujilinda na nani? What if the whole world join NATO. Then nini kitafata? Na kwanini expansion ya NATO iwe toward Russia? Kwani Brazil, Venezuela, Mexico, Panama, Argentina wasisogezwe kujiunga NATO iwe lazima kwa hizo nchi zinazozunguka Russia?

Je, una habari ka Russia, alishawah kutaka kujiunga NATO? It sound ka haiwezekani sio? Its true, katika term ya kwanza ya Urais huyu V. Putin, alipeleka Ombi la kujiunga NATO ila wakamtolea nje na kumpuuza. Je kwa hapa em jiulize kama lengo la NATO ni ulinzi kwanini against others, kwanini walimpuuza huyu huyu ambae kwa sasa wanadai wanaungana kujilinda dhidi yake?

Toka Mgogoro uanze, na kabla ya mgogoro kuanza, ni kua Russia hataki Silaha za US kibarazani kwake, ukumbuke US ndani ya NATO ana jeshi lake kwenye kila nchi. kama US aliamua kupigana na CUBA kisa Russia kuweka silaha zake pale ye kwanini atake kuweka Silaha zake jiran n border za Russia kwa mgongo w Ukraine ajiunge na NATO?

Comment itakuwa ndefu ngoja nikomee hapa.

Jarib tu kulitizama tu hili swala katika different angle utapata different observations na utaweza pata kwa utashi wako kuona nani yuko sawa na nani hayupo sawa.
 
Kwahiyo mmeacha kumdharau Zelensky mliyekuwa mnamuita Joti?

Malengo ya Urusi wakati anaanzisha operation ni yapi na kati ya hayo ni lipi limetimia. Kama hawana lengo la kuiteka walipeleka majeshi yao kufanyaje au kuna drills walikaribishwa wafanye.

Lengo la Ukraine ni kujilinda na kujitetea. Wewe mwenyewe najua unajua progress ya lengo hilo.

Putin atamkamataje Zelensky? Kwani mpaka Putin anawaambia wanajeshi wa Ukraine wampindue Zelensky ile wiki ya kwanza lengo lake lilikuwa nini. Kadyrov si anashinda Tiktok na vitisho vyake vilikuwa ni hivyo.
You are better than this
Hivi ni kwanini ProNato mkiulizwa maswali hamjibu badala yake na nyie mnakuja na maswali mengine!? Hii ni namna mbaya sana ya kufanya mjadala. Nimeuliza maswali kibao hapo kuhusu hoja zako ulizozitoa cha ajabu badala ujibu/utetee hoja zako wewe unaniuliza tena mimi. Mm ntakujibu vipo ikiwa wewe hujanijibu!?

Hatuwezi kwenda kiubishi hivyo. Jibu kisha uulize.

Au unakimbia kijanja [emoji848]

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Jibu ni angetaka diplomacy, the same anachosema kuhusu Finland na SWEDEN kuingia NATO angekifanya kwa Ukraine kuimarisha Ulinzi wa mpaka wake na Ukraine
Russia can't take risk Sweden na Finland wakijiunga na NATO atawavamia kabla ya kujiunga na wenyewe hawezi kufanya kosa kama hilo la kujuinga na Nato
 
West kwny propaganda wame-invest heavily,Ila kitu kimoja nilichokipenda khs hii Vita mainstream media zote/sijui hizo CNN,BNC,SKYNEWS etc/Twitter/FB/YouTube etc watu wameshazijua Ni propaganda machines na baada ya hii Vita vinaenda kupoteza mashabiki Sana.

Wazungu walitumia akili Sana kwny propaganda,fikiria mtanzania wa kawaida anaesikilia Radio Free Africa(RFA):

Ile ameamka tu saa 6:00 asubuhi anasikiliza DW Swahili/BBC idhaa ya kiswahili.

Mchana saa 1:00 kamili mpk -2:00 kamili anasikiliza DW Swahili.

Jioni saa 6:00 anaanza kusikiliza Dw Swahili mpk saa 6:30 jioni ,then from hiohio saa 6:30-Mpk saa 7:30 usiku anasikiliza BBC Swahili na from hio 7:30-8:00 usiku anaunganishwa na VOA(Voice of America) ya kiswahili (ya wale watangazaji wakina Vincent makori) after hapo saa 9:00-9:30 usiku anaangalia wakina Salim kikeke kwny BBC Swahili (kupitia Star tv).

Siku nzima mtu anashinda anamezeshwa uongo wa wazungu, kiukweli tulichelewa Sana kuwafahamu wazungu lkn hizi propaganda zao kwa generation ya Sasa hivi zinaenda zinakufa/kufifia maana watu kwa sasa wana njia nyingi za kupata habari from independently sources.
[emoji1787] Sana tena sana... Na sio kabla tu ya hii OP. Toka nyuma huko watu ila kwa wafatiliaji tu wanajua Media are lying, wanajua Western ni Empire of lies.

Wanafaham vizuri tu. Kuna kundi flan hivi nipo limejaa aina flan hv ya watu wanajiita "Patriots"... Hawa ndio huwa wanafunguka madudu ya nchi zao unayajua na kuelewa kiundani...

Mfano issue ka hii ya US uko Iraqi huezi kutwa imewekwa kwenye MS Medias yoyote
-5956294727114536949_120.jpg
 
Russia can't take risk Sweden na Finland wakojounga na NATO atawavamia kabla ya kujiunga nawenyewe hawezi kufanya kosa kama hilo
Do you believe Russia can fight two fronts?

In theory Sweden has much power than Ukraine...
 
Ki ulinzi hakuna nchi duniani anatamani jirani awe na nguvu sawa au kumzidi. Itakuwa uwendawazimu kumruhusu jirani unayemmudu akuletee adui mlangoni.

Hii ndio sababu Israeli inapambana kwakila njia nchi jrani yake asiwe na nguvu.

Marekani inapambana kwakutumia UN kuwazuia wengine kuwa na nguvu kama zake au kumkaribia. Yupo tayari aingie gharama kukulinda ili usiwe na nguvu

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
Nchi nyingi duniani zina majirani yanayozidi nguvu. Botswana yenye watu 2.5 ifanye nini ikiwa jirani ya Afrika Kusini yenye milioni 60? Benin yenye milioni 11 ikiwa jirani ya Nigeria yenye milioni 211??
Tunachohitaji ni utaratibu unaokubalika kote ukiheshimu haki ya kila taifa. Utaratibu huu upo katika mapatano ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.
Uko pamoja na mashariti kutumia kwanza kila uwezekano wa kuondoa matatizo kwa njia ya majadiliano na mbinu zisizo za mabavu.
 
Vladimir kwa kupenda kiki hajambo,Judo,Newyork marathon, horseriding. Ila "adventure" ya Ukraine mtu mzima ameanguka flat on face .
Mademu wa Ukrain walishapigwa mulimba za kutosha, bahati mbaya hakuna dawa za kutoa mimba maana hospitali zishakuwa magofu itabidi wazae tu hakuna namna.
 
Back
Top Bottom