Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hivi hawa jamaa wanapotoa updates za kila siku kuhusu vita hii kwa nini huwa wanatoa taarifa za kuwapiga maadui tu . mbona hawatoi taarifa kuwa katka mapigano ya Leo tumepoteza askari kadhaa na vifaa vyetu kadhaa?
Vitani kila mtu huwa anatangaza mafanikio aliyo yapata.
Hata Ukraine tangu kuanza kwa vita inatangaza kuuwa wanajeshi wa Urusi lakini haijawahi kutangaza kuuwa kwa wanajeshi wake.
 
Uwe unasoma na kuelewa,Mimi Sina meli wala ukoo wetu haumiliki meli!Nilichosema umeingia mkenge,Russia anasema hili na Ukraine anasema lile!Nimekwambia hata media kubwa kwenye kureport tukio Hilo Bado wameliacha wazi bila kuegemea stroy za upande wowote!Sasa who are you uconclude kuwa Ilikuwa striked na missiles?
Acha upunguani!
 
Ukikadiria ukubwa wa Ukraine kutoka kule Magharibi, hutaweza bisha au kukataa kuwa Bado Odessa ipo mashariki.

Sijajua unachobisha, lugha yao ni kirusi.View attachment 2188923View attachment 2188925
Maumivu yakizidi, umwone daktari. Kijiografia Odessa iko kusini mwa Ukraine. Kati ya mashariki na Magharibi iko katikati, lakini zaidi upande wa magharibi. Kwenye ramani juu kuna neno 1 la Kirusi, ambalo ni "Москва", sijui wewe umeona nini, lakini usisahau kumweleza daktari! Menginevyo Odessa wanaongea lugha tofauti; hata Waukraine wengi kabisa wanaopigana sasa na jeshi la Putin wanatumia Kirusi kama lugha ya kwanza au ya pili.
Ukijua kusoma ramani: Ukraine sehemu ya magharibi kabiso iko kwa nyuzi 22°09', sehemu ya mashariki kabisa iko kwa 40°10'. Odessa iko kwa 30°40'.
Kwa hiyo utaona iko karibu katikati (ambao iko mnamo 31°) lakini upandew wa magharibi.
Ndugu: kuvuta propaganda mno si vizuri kwa afya, wala ya macho wala wa roho na akili.
 
Yani brother unawaza kidogo sana Russian hawezi ku sustain even for 10 years kupigana na ukrain
Na Putin must go
 
Hizi taarifa Huwa Wanapita kimya kimya!Habari kwao ni meli kuzama!
 
Vitani kila mtu huwa anatangaza mafanikio aliyo yapata.
Hata Ukraine tangu kuanza kwa vita inatangaza kuuwa wanajeshi wa Urusi lakini haijawahi kutangaza kuuwa kwa wanajeshi wake.
Kwa hyo tuamini taarifa za 🇷🇺🇷🇺 au🇺🇦🇺🇦?
 
Kaka unachosha. Lete ushahidi kuhusu majasusi, propaganda ya kirusi haikubaliki. Waliosimama walikuwa wananchi. Serikali?
Mapinduzi yalimlenga rais. Unavyojua serikali ina mihimili mitatu. Rais aliamua wakati ule kukataa azimio la bunge lililotaka mkataba na EU. Rais alikataa -kwa siri mwanzoni alijaribu kuificha- akaanza majadiliano kuhusu mkataba na Putin. Ambacho wananchi wake hawakutaka, jinsi injavyoonekana katika kura za chaguzi huru zote baadaye.
Sasa wewe kutoka nchi ya chama tawala kisicho na mwisho unataka kuwafundisha Waukraine uchaguzi huru ni nini??
Au unakubali Bwana Putin aliye hodari kughushi kura zote tangu ameingia awafundishe?
Nakutakia mafanikio mema!
 
Wewe utanisumbua na Hilo fuvu maana kingekuwa kichwa ungeshaelewa.

Mwanzo uliizungumzia mariupol kuwa haipo Mashariki sijui, nikakuelewesha kuwa ipo Mashariki.

Naona unakomaa hapa, kweli ipo kusini na wakazi wengi wanaoongea either kirusi au kigiriki hivyo kufanya eneo muhimu kwa Urusi.

Kumbuka hiyo Odessa pia imepakana na eneo muhimu la kimkakati la Transtiria ndani ya nchi ya Georgia.

Hivyo kuwa kusini haiondoi kle nilichokueleza kule mwanzoni na kukukosoa, pia ni mji wa bandari na Urusi ikifanikiwa kupashika hapo itakuwa rasmi imeikata Ukraine na access ya bahari.
 
Wamarekani wenyewe wanajua MAKOSA ya kivita waliyofanya Afghanistan na Iraq ...na hawamtaki kujiunga na ICC kulinda MAKOSA ya wanajeshi wao lakini Kuna wamarekani wa bunyokwa .... Wanakaza shingo Urusi nae atumie upuuzi wa Kimarekani Ukraine. Unapigwa kistaarabu ...unapigwa huku unapewa maji una pewa chakula na dawa...
 

Attachments

  • VID_20220414_212305_389.mp4
    2.1 MB
Lakini mkuu hata Urusi si ameshateka baadhi ya maeneo ya Ukraine?

Hapana mkuu hizi settlements/ maeneo zote/yote bado zimeshikiliwa/yameshikiliwa na Ukraine ... Urusi bado anapaka rangi na kuvuta umeme na maji mkuu. Maana kaishiwa silaha na chakula na dawa ... Na vifaa vibovu .... Anapigikaaaaaa hiiiiii
 
Kakaaa.... Watu wameshachagua upande......... Hakuna Rationale behind the OP(wengine wanaitwa War). Ni hoyahoya tu mpeleke mpeleke sekeseke mguu wa shingo watu weweeeeeeee huyo kapigwa ngwala watu woyoooo .... Kwa nini kamrukia shingoni na yule kampiga mwenzie ngwala .... Wanapoteana/tunapoteana jukwaani . Muvi lefu hili kama series ya Jumong bado sanaaa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…