triga
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 1,029
- 5,712
Maswali yako ni mazuri kwa mtu anayetaka kutetea hishma yake!Kurudi mezani na kumpigia magoti Urusi sio option yenye manufaa kwa raisi wa Ukraine
Vipi kuhusu wanajeshi wako uliowaambia tukapigane na sasa wamekufa?
Raia wako waliobeba silaha na sasa wamekufa?
Utawaambia raia waliobaki nini? Kuwa vifo vyao ni for nothing? Watakuelewa?, si tulikubaliana tunaingia vitani huku tukijua adui ni Urusi na ana mabomu makubwa makubwa? Tukakubali tufe tukitetea msimamo wetu? Iwaje leo ndugu zetu wamekufa halafu unabadilisha msimamo sababu ya maslahi ya uhai wako wewe? Uhai wako unathamani kuliko wengine waliosimama na wewe na kumkabili Urusi?
Akipiga magoti anaweza tengeneza uadui mkubwa na raia wake waliopoteza ndugu na rafiki kuliko akisimama na jeshi lake wakapigana mpaka mwisho.
Unafikiri dignity na uhai ni kipi kinaanza!?
Anaweza kurudi mezani akakubaliana na Putin majeshi ya urusi yakarudi nyumbani nchi ikawa salama kisha yeye akastep down kuepusha uhasama kwa raia wake.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app