Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Mkuu hapo utofauti ni Time-period hata California ilikuwa huru kabla USA hajaivamia na ilatambulika kama Taifa kisheria.

Na huu mfano wa California hauna utofauti na Ukraine,jibu swali rahisi sana Leo hii Urusi akatengeneza propaganda California ikajitenga-kisha waanzishe ushirikiano na Urusi dhidi ya USA wewe ukiwa Rais wa USA utafanyaje???
 
Naomba nikujibu.

Unaposema ukoloni una maana gani?

Poland haikuwahi kuivamia Urusi?

Unafahamu muungano wa Poland-Lithuania na cossacks wa zaphorozhia?

Haya Mataifa Yana historia zao, visasi vyao na chuki baina yao.

Lakini hauwezi kuuita ukoloni.

Labda tufahamishe nini maana ya ukoloni?
 
Russia is expelling three Swedish diplomats in a tit-for-tat response to the expulsion of its diplomatic staff by Stockholm, the country’s foreign ministry has announced.

Swedish Foreign Minister Ann Linde later said Russia had decided to expel four Swedish diplomats – three from the embassy in Moscow and another at the Swedish consulate in Saint Petersburg – and denounced the move as β€œunmotivated and disproportionate”.

Alafu kuna kamtu humu kanasema Sweeden anaumogopa Russia
 
Wacha wajiliwaze maana wakifikiria kuwa mzalendo Kwa nchi ambayo watu 6 wamechukua 6bln tena BOT inahitaji moyo
Tena moyo mpana SANA...

Kuna issue huwa zinaendelea unazitizama unakereka hadi unakereketwa kibaya uwezo wa kuyabadili ukijitizama hauna...

Ukiangalia kando labda unaweza pata support ya kubadili kile kilichopo mbele yenu wote unakosa wa kumwamini...

Kwa kifupi kuna mambo yanahitaji kujitoa akili kwanza ili uweze kuyavumilia otherwise unaeza ishia kusikojulikana tu [emoji25]...
 

Sometimes kuwa serious sweeden wa kumsumbua Russia?? Au unataka tucheke mzee? Endelea kutupa vichekesho thread ichangamke.
 
Sometimes kuwa serious sweeden wa kumsumbua Russia?? Au unataka tucheke mzee? Endelea kutupa vichekesho thread ichangamke.

Urusi hawezi pigana na Sweden kwasasa,
Urusi haina uwezo wa kuendesha vita na nchi nyingine hapo ulaya, atachakazwa vibaya sanaa....

Akijaribu hivyo, tunampa miezi 4 kwisha habari yake...
Ndo mana Finland, sweden wana kiburi cha kujiunga Nato sasa, wakijua Urusi hawezi fanya chochote kwa sasa na muda waliokua nao ni sasa....
 
mkuu hao watu ni matusi tu na mipasho ndio wanaelewa, vipi kwanza EU wameshanza kulipa kwa ruble? maana mwsho ilikua march 31
Hili hawaliongelei kabisa kwa sasa,tangu lini mwenye njaa akachagua chakula,kwa sasa Pro Putin wamekuwa kama chombo kilichokosa mwelekeo baharini,walisharukia hadi uchaguzi wa France na matokeo walikuwa nayo mfukoni mwao[emoji3][emoji3],uhalisia umekuja kuonekana,wamekaa kimya kama siyo wao
 

Hao Finland na sweden utaona kma watajoin NATO. Hizo ni porojo jomba
 
Kwani kwa sasa Urusi anaendesha vita wapi??
 
Kuna tofauti ya Umoja wa kiuchumi na umoja wa Kijeshi.

Je, NATO ni umoja wa Kiuchumi kama sivyo, unaufananaishaje na Jumuiya ya afrika mashariki ambayo ni umoja wa kikanda kwenye masuala ya uchumi ukiutolea mfano wako wa DRC.

Duniani kote hakuna himaya isiyojitanua kwa kutumia mabavu ya Kijeshi.

Sio wachina, Warusi au Wamarekani.
Unafikiri kwa nini Marekani walipinga na wataendelea kupinga kuanzishwa kwa jeshi la umoja wa Ulaya.

Dunia imebadilika ambapo Sasa maendeleo ya sayansi na Teknolojia yamefanya Mataifa kuja na hybrid warfare.

1) VIKWAZO
Nani hajui kwamba vikwazo vya kiuchumi vinatumia na Mataifa ya Magharibi dhidi ya maadui zake hivyo kufanya economic war.

2)Mbinu za ujasusi za Maandamano na kupindua.

Nani hajui Maandamano mengi, huandaliwa na Mashirika ya majasusi ya kigenibili waweze kupitisha sera zao, au kupindua serikari iliyopo madarakani ili waweke watu wao.
Mfano Venezuela, Egypt, Kazakhstan

3) Mapinduzi ya Kijeshi (coup' d tat)
Haya tumeyaaona kwa in service ambao wapo kwenye Mataifa mbalimbali kupindua kwa ajili ya maslahi ya Mataifa ya kigeni na maslai yao

Mfano afrika ya Magharibi na kinachoendelea kufanywa na Wafaransa.

4) Kuanzishwa kwa vikundi vya waasi na kuvipa siraha na nyenzo nyingine za kifedha.

Sina haja ya kukielezea hilo, maana kila mtu analijua

5)Vita halisi (Actual war)
Naona amejaribu kidogo kuchambua kwamba wanajitanua bila uwanja wa vita,

Ukiangalia ameangalia tu bara la Ulaya,
Je wanavyojitanua Mashariki ya kati bila vita, Amerika ya kusini bila vita.

Tukiacha kuwa wanafiki, USA anatumia mbinu zote mpaka vitisho.
Tuendelee na kuchambua wakulungwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…