Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Mkuu umefafanua vzr ngoja nijazie kuna kitu US mpaka sasa hajiamini hajui maadui zake hata hao ambao wapo NATO ikianza WW3 wapo watakao mgeuka wengi wapo kimaslahi pale.
Ná Marekani anajua kuwa kuna kundi kubwa halimsapoti, hivi unafikir Japan hakumbuki machungu ya hiroshima?? Anajikaza tu

Kumbuka kuna kundi kubwa la nchi za Asia zitakua pamoja na Russia kuna china, NK, india brazili hao ni moja ya partner wa Russia. WW3 ikitokea Europe ndo watakaoumia zaid manake vita itapigwa hapo Europe.
USA ana hali mbaya sana.
 
Kuna watu hadi Leo hawajawahi kujua kwa nini Russia ni threat 80% kwa USA kuliko China katika U super power hadi Leo.
Kwanza,Russia yupo vizuri kijeshi zaidi ya China kwa 95%,usipo kuwa na nguvu za kijeshi sio rahisi uwe super power wa dunia-unaweza ukaupata lakini unaweza ukatoweka muda wowote.Hivyo kwa USA Urusi ni hatari kwake kuliko China ndio maana anatumia njia zote za kijeshi kukabiliana naye kumzunguka na huwezi kuona anatumia hizo njia dhidi ya China maana anajua China sio chochote.

Pili,ni Rasilimali zinazoendesha Dunia-zaidi ya mataifa yote ulaya ambayo ndio mataifa tajiri zaidi Ulimwenguni yote yanamtegemea Urusi katika kuendesha Uchumi wa Nchi zao.Hivyo,ikitokea chochote ni rahisi Russia kuya control mataifa hayo Politically-ndio maana USA anafanya kila namna Russia asiwe na mahusiano mazuri ya kisiasa na hizo Nchi kwa kuwatishia kuhusu mambo ya Usalama. USA anajua fika ikiwa EU itakuwa na mahusiano mazuri ya kisiasa na Russia basi ni mwisho wa U super power wake maana wanaweza waka dictate chochote na kumuweka USA nje.

Tatu,Ukiachana na hayo mataifa ya Ulaya ambayo yapo chini ya Russia kiuchumi-Mataifa ambayo ni Makubwa kama India,China,Brazil na yale yanayoongoza kwa uzalishaji wa mafuta Duniani yote yana mahusiano mazuri na Urusi.

Ukiangalia matukio haya utaona ni kwa jinsi gani USA atatakiwa kuzicheza karata zake,lasivyo inaweza kuwa mwisho wa Utawala wake.
 
Ukweli mchungu
Screenshot_20220429-204118.jpg
 
Kwa nini wengine hawafuati mfano wa Urusi? Kwa sababu ni hatari kuchezea thamani ya pesa ambayo ni picha ya nguvu ya uchumi.
Urusi inajaribu kusukuma thamani ya pesa yake juu zaidi , maana wasingechukua hatua walizochukua, rubel ingeshuka kabisa na baadaye hakuna duniani anayetaka kuigusa.
Kwa mbinu wanazotumia (kulazimisha makampuni yao ya gesi/mafuta kupeleka $€ zote benki kuu na kununua rubel, kuzuia $€ zisitolewe nje, kuzuia wawekezaji kuuza hisia na kurudisha pesa nyumbani) , wamefaulu kutetea thamani ya ruble sokoni; ila hii inategemea kabisa mapato ya kuuza gesi/mafuta na mauzo hayo yanazidi kupungua. (itachukua miaka hadi kupata njia mbadala kwa wateja wengine - kama wapo)
Kwa upande mwingine nguvu halisi ya uchumi unazidi kushuka; hawawezi kupata tena vipuli vingi (uzalishaji wa magari katika viwanda vya Urusi ulishuka vikali tangu Machi, ona Russian car market has decreased by 63% in March 2022 | RusAuto.News) , makampuni mengi ya kimagharibi yaliyozalisha magari na mashine yanaondoka.
Urusi inahitaji kutafuta njia mpya za kupata vipuli . Maana kabla ya vita asilimia 40 za bidhaa zilizonunuliwa na Urusi nje zilitoka Eu na Marekani. sehemu kubwa ya bidhaa hizo hazipatikani tena kutokana na vikwazo.

Ona hii
Russia’s main imports are machinery, chemicals, and other manufacturing goods, and that Russia depends on the rest of the world for the supply of many complex products. One factor explaining Russia’s sectoral trade profile and dependency is its poor labour productivity. Russian labour productivity in the industrial sector is 21 percent of US and 36 percent of EU’s labour productivity. In other words, the Russian economy needs five workers to do the job of one US factory worker. chanzo: Russia Import Dependency Problem |

Hata katika sekta ya silaha inayotajwa hapa mara kwa mara, udhaifu wa uchumi wa Urusi unaonekana: wana mahandisi wazuri waliobuni silaha bora (au: zinazoaminiwa kuwa bora maana hazikufika vitani bado) kama kifaru T-14 na ndegevita SU-57 lakini silaha hizo hazikufika kwenye jeshi bado kwa sababu hadi sasa tasnia ilishindwa kuzitengeneza mbali na mashine chache za majaribio na uchumi kwa jumla haikuwa na nguvu kuzalisha mapato ya kutosha kulipa gharama za mitambo hii. Hapo sababu kwamba wala T-14 wala SU-57 haikuonekana bado katika vita hii, na hazitaonekana.
Mkuu nakusisitizia kila siku mapato ya nishati ya Urusi hayajapungua bali yameongezeka ila unajifanya huelewi kabisa.
Screenshot_20220428-205334.jpg


Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
 
Putin kapeleka msiba mzito Marekani...

Majeshi ya Russia yamemdedisha mwanajeshi wa Jeshi la Marekani (US Marine) aliyeenda Ukraine kupigana dhidi ya majeshi ya Russia....kaacha mjane (mke mbichii) na mtoto yatima

Asante sana Putin kwa kupeleka msiba Marekani, kutengeneza mayatima marekani na kuunda wajane marekani...kila mtu ajishindie mechi zake

View attachment 2205138View attachment 2205137
Kwamba "Willy Joseph Cancel" has been Cancelled by RFA.... Aseee Wamem-cancel ka jina lake shenzi kabisa. Unaacha familia ako unaenda pigania hizo punguani za Neo-Nazi...
 
Mkuu nakusisitizia kila siku mapato ya nishati ya Urusi hayajapungua bali yameongezeka ila unajifanya huelewi kabisa.View attachment 2205167

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
$46,300,000,000 ni sawa na Tsh 107,645,786,900,000.02

Yaani Tsh Trillion 107.6

Gharama ya SGR Dar mpaka mwanza ni around Tsh 12 Trillion.
Kwa pesa hiyo ya mwezi mmoja na sehemu iliyopata Russia. Tunaweza kujenga SGR 9 zenye urefu wa Dar mpaka mwanza.
 
$46,300,000,000 ni sawa na Tsh 107,645,786,900,000.02

Yaani Tsh Trillion 107.6

Gharama ya SGR Dar mpaka mwanza ni around Tsh 12 Trillion.
Kwa pesa hiyo ya mwezi mmoja na sehemu iliyopata Russia. Tunaweza kujenga SGR 9 zenye urefu wa Dar mpaka mwenza.
Na hiyo ni kwenye nishati iliyo uzwa ulaya tu bado ile inayo uzwa Asia, America ya kusin,Afrika.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
 
Hehe sawa ngoja tumngojee ila MKUU Galip QiL tutolee mwanga kidogo kama linafahamika
Aaaaah happana, kwenye issue za kivita sio mjuzi kiiivo, Huwa sio kipaumbele changu kuyachimba deep...

Ila tatoa maelezo mafupi vile namna navyojua so far kuhusu hao Dolphins.

Hao dolphins wako trained kama viumbe wengine wanavokuwa trained katika utambuzi wa vitu hatarishi kama mabom au route za adui.

Na hawa Dolphins nahisi wamechaguliwa special kwa hii task kwasabab wana-possess naturally kitu hiki wanaita SONAR... Technique flan hv ya kutumia sound propagation katika kunavigate na kutambua objects on or under water surface...

So hao dolphins ndani ya maji kuzunguka hizo meli naona kazi yao ndio itakuwa hiyo katika kudetects presence ya mines ambazo zinaeza wekwa au kuletwa karib na Adui katika meli zao hao Russia...

Maelezo zaidi watakuja wataalam wataongezea.
 
Raisi Zelensnkyy myahudi nakuaminia

Biblia inatamka wazi Askari mmoja myahudi anakimbia Askari elfu 10 wa adui bila kujali adui ana silaha gani iwe nyukilia au chochote

David kwenye Biblia aliua Goliathi mwenye misilaha kibao wakati yeye alikuwa na manati tu

Zelensnkyy Komaa wewe ni Joshua wa Generatio hii ndio utawaletea ushindi wayahudi walioko Ukraine usiogope mi nyukilia yake huyo Putin pigana kiume mtoto wa kiume
 
Ulichokiandika %kubwa ndo uhalisia

Kwa kuongezea hapo, Russia kwasasa anatumia wapiganaji wa majimbo yaliyo jitenga na Ukraine kupigana na majeshi ya Ukraine huku small scale ya Russian army kama wanchenchen wakishambulia kama back up tu na siyo frontlines. Ndo maana husikii hawa jamaa wakifa au kukamatwa hovyo hovyo zaidi ya kuwaona wakipiga self na mazoezi nchini Ukraine.

Pia inaonekana wanajeshi aliopeleka urusi kwenye operation hii ni wale wa kiwango cha kawaida kabisa size ya jeshi la Ukraine.
Halafu wale high trained military personnels wamebaki urusi kwajili ya kujipanga na vita kamili endapo kama hii operation ikigeuka kuwa vita baada ya NATO kujiingiza moja kwa moja.

Kwanini nadhani hivo?; ukiangalia picha za wanajeshi wa urusi walio tekwa au kuuawa wengi wao ni vijana wadogo sana aged kati ya 17 to 24 yani kibongo bongo unaweza kusema ni wale service men(kuruti walio iva) walio rundikana makambini wakisubiri ajira za mama za JWTZ.

Ukitaka kuona kuwa urusi haijatumia hata 10% ya jeshi lake halisi kwenye hii operation subiri gwaride la siku ya ushindi(victory day) on 9/5/2022 hapo ndo utajua Russia alijua na anajua anachokifanya.

Tatizo watu mnakosea sana kulinganisha maamuzi ya kijeshi au operation ya nchi kubwa kama Russia au USA na operation za polisi wenu wa kibongo za kupambana na vibaka pamoja na wezi wa pikipiki Hapo DSM.

Urusi siyo Zaire na Putin siyo IGP Siro.

Nalog off.
Dadeki, Oyaaa bibingi unaona wafuasi wa Putin walivyo Smart [emoji847][emoji847][emoji847] Unasoma mwisho wa maelezo unaishia kutabasam tu...

Some arguing with facts that are real and reasonable while others arguing bas tu kuonekana wanajadiliana... Full of BS.
 
Back
Top Bottom