Mkuu sovereignty naielewa vyema sana pamoja na Liberty!
Ila kwa alichokuwa anataka kufanya Ukraine haikuwa sawa. Marekani na Warudi ni mahasimu na Ukraine inapakana directly na Urusi!
Baada ya vita ya pili ya dunia waliwekeana mikataba kuwa hakuna ambaye hakuna mtu ambaye anaruhusiwa kuweka majeshi ama barracks zake kwenye eneo lililopakana na mwenzie.
Mwanzoni Urusi aliweka Cuba marekani akamfurusha akaondoka hakukuwa na mvutano wowote. Ila sasa Marekani nae anataka kufanya kile kile ambacho yeye hakukikubali Cuba. Anataka aweke majeshi yake Ukraine
Kwenye historia pia nahisi utakuwa umeenda mbali sana... mpe tu mfano ulio hai hivi sasa...
China na Solomon wamesign security deal ya pamoja, US na Australia ambao wapo thousand of mile kutoka Visiwa vya Solomon wanamtishia kumpiga kisa mahusiano yake na China wakidai n threat kwao...
Je huko sio kuingilia Sovereignty ya Taifa jingine lililo huru? Deal liwe kwa China na Solomon kwao ligeuke kua threat? Je hizo bloc wanazotengeneza wao sio threat kwa wengine?
Na kama wako sawa na sio kuingilia Sovereignty ya taifa hilo... kama wao wameona threat thousand of mile kutoka kwenye mipaka yao je vipi kuhusu huyu Russia kwa hili kundi linalotaka kukaa kwenye kibaraza chake?
Kwanini kunya anye kuku akinya bata kaharisha... Hii double standard ya nini ka kweli mnaipenda na kutaka kusimamia misingi ya haki?
US aliona kua kuna tatizo Iraqi mile zaidi ya ef 11 kutoka kwake, na akavamia akalipua akamnyonga Rais wa watu kwa kisingizio cha WMD... Weapon of Mass Destructions walizodai hazikuepo na hakuna aliyezungumza zaidi waliishia kuiba mafuta na dhahab walizozikuta...
Obama huyo hapo kisa Gadaffi kutoa proposals ya matumizi ya Gold standard ka mbadala wa dola akafatiwa kuvamiwa na jeshi la NATO hapo na kumuua... Hakuna waliozungumza na mwisho Obama anatunukiwa tuzo ya Amani mikononi akivuja dam za wasokua na hatia...
Leo hii huyu yupo anapigania usalama wa nchi yake dhidi ya hao hao warmongers kutoka western tunasimama kumuita kichaa [emoji52] kisa UK na US wamessma... so interesting.
Eeh sasa to know hili ni zuri na hili ni baya tunatumia standard ipi? Tupunguzeni unafiki na ifike hatua walau sie watu weusi tuwe na courage ya kuita nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe and not otherwise bila kujali nani aliyefanya...
Kwa mtu mwenye akili timamu ingetosha tu kutizama list ya wanao'msupport zelensky ni watu wa aina gani na haraka kujitenga nae...
US anadai anataka kulidhoofisha jeshi la Russia, huku mswahili Poporipo anaona Zele anapigana kutetea nchi yake...
Kama kweli kuna watu wako huru na halmashauri za vichwa vyao haikutosha tu kujiuliza kwanini solidarity wanayoifanya Western kutoka US na EU kwa Ukraine dhidi ya Russia haikuwah kufanywa kabla ilhal kila leo kuna migogoro kila kona za dunia? Why Ukraine tu na sio sehem zingine? Mmmh?
Wengi tutafika tumechoka sana kwenye hii safari ya matumaini. [emoji23][emoji23][emoji23]
It's okay kufuliwa kupikiwa hata kuogeshwa vile vile ila ikifikia hatua mtu unaanza kupokea msaada wa kufikiria, yan someone think and decide on your behalf... ni huo mda tu huwa tunakuwa hatuna tofauti na MISUKULE.