kwenye jukwaa hili mimi ndo najiona sina kitu kuliko wote, nimefuatilia thread hii toka mwanzo :
nilichogundua hapa nikuwa
Russia wanapoona silaha, za Ukraine zinaongeza makali nao wanaongeza kidogo nguvu,
kwa mtazamo wangu mimi Ukraine wangemaliza hii vita kidiplomasia
huko mbelee Russia watakaza zaidi alafu wanataiharibu nchi yote,,
ila nyuma ya hii op naona kuna kitu wengi huenda hatukijui au tunakijua ila hatukielew....
maana bwana zelewesky nashindwa kumuelew kitu kimojaa..."kwani kujiunga NATO na kutojiunga mkaishi na jirani yako kwa amani shidaa iko wapo?"
kwani NATO wana faida gani kubwa ambayo inaweza kureplace maisha ya watu na miundo mbinu inayoharibiwa kila uchwao ?
au mimi ndo sijui ?
faida gani member wa NATO wanapata kinacholingana na kila Ukraine inapoteza ?
na uchumi wa dunia unatatizika kiasi hiki ?
kila siku nasikia wataalamu mbalmbl wanasema Russia ili miscalculate resistance ya Ukraine, lakin mimi nahis USA ndo ili miscalculate response ya RUSSIA kwa Ukraine kujiunga NATO,,,,
ila kwa kutumia historia tu, mimi binafsi nafikiri Russia pia hajakurupuka kwenye hili,,,, huenda hii vita ikatufikisha mahali AMBAPO sis third world countries hatukutegemea..........
wengi tunafikiri RUSSIA kakosea sana,
lakin siku chache hizi nimeona china ikitaka kuweka millitary base solomon island USA NA Australia wamekuwa wakali sana na wamesem watarespond accordingly,
ndo najiuliza kwa nn wao Ukraine hawafeel the same taste ??
jaman sisi hapa jamiiforum nahis kuna vitu hatuvijui zaidi ya yale tusumayo Google huko....ila mataifa haya yanajuana.....
kwa kifupi tu niseme dunia inahitaji Russia yenye NGUVU kuliko yenyewe inavotuhitaji kwa sababu USA akiwa kiranja wa dunia ana misuse power yake..
nadhani temeshuhudia akitumia nguvu yale kunyanyasa mataifa mengi Libya, Iraq, etc