Mr Tyang
JF-Expert Member
- Sep 30, 2018
- 1,727
- 6,807
Naona hujui hata unachosimamia, huko mwanzo ulisema Urusi ameshindwa vita vya ardhini amebaki tu kurusha makombora kutoka ardhini mwake, nimekupa facts kwa kuangalia dunia tulipofika juu ya tekinolojia ya kisasa kuwa mtu anaweza kukupiga akiwa ndani anakunywa chai, umegeuka nakusema sijui hayo ni mambo ya kwenye Movie.Vita halisi ni tofauti sana na unachoona kwenye movies za 'kubonyeza tu button' watu wanakufa katika uwanja wa vita.
Halafu Putin tayari amekwishawatoa kafara wanajeshi wake 20,000 waliovamia kichwa kichwa huko Ukraine. Kafara gani zaidi wewe unayozungumzia??
Kwahiyo kwako Russia anavyo bonyeza vitufe vya hypersonic missiles akiwa urusi na kwenda kusambaratisha military bases za Ukraine kwako ndo movie siyo?
Tatizo lako bado una akili za kijima na ndo maana hata vita vya kisasa unataka vipiganwe kwa mbinu za kijima.
Watu wanamiliki mabomu ambayo yanaweza kuiteketeza DSM yote kwa bomu moja tu halafu unataka wapoteze muda na nguvu kushambuliana ardhini kwa bastora na bunduki za AKA47 kweli?
Majeshi ya ardhini kwa zama hizi yapo kufanya tu clearance baada ya Air forces na missiles kuharibu hali ya hewa.
Thing you have to note is "Majeshi ya ulaya siyo kama majeshi yenu ya jadi"
Na ukiona Urusi anamshambulia Ukraine kutoka Urusi basi tambua kuwa Ukraine kazidiwa kwa hilo na wala hana huo uwezo wa kuishambulia urusi kutokea ardhini kwake. Ndo maana kila siku mnaambiwa kuwa URUSI SIYO VISIWA VYA USHERISHERI bado hamuelewi.
Sawa endeleeni kukaza hayo mafuvu yenu wakati Ukraine inaendelea kubaki majivu siku hadi siku.