Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Siku ya 79 ya Oparesheni ya Urusi nchini Ukraine, na ni siku ya 20 ya oparesheni phase 2. Tarehe 13/5/2022.

Kwa siku tatu juzi, jana na leo, Urusi imeongeza nguvu kubwa katika mashambulizi yake Ukraine ambapo imepanua mara nne zaidi ya eneo ililokusudia kulilinda baada ya kujitangazia uhuru wa maeneo hayo katika majimbo ya Ukraine ya Luhansk na Donetsk. Upanuzi huo umefanya Ukraine kumegwa katikati ya nchi hiyo kutoka Kaskazini mji wa Kharkov hadi kusini mji wa Mykolaiv ikimega kwakukatisha katikati ya nchi hiyo hadi mji wa Zapolozhye.

Urusi imetumia mwanya Wakati dunia ya Magharibi iko kwenye mtanziko mkubwa kwa mauaji ya Israel dhidi ya waislamu waislsmu wa Palestine wenye meimamo mkali kule Al Aqsa na vurugu za mauaji yw mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Aljazeera Bi Shereen Abu Akleh. Hadi sasa Marekani, NATO, na nchi zingine binafsi kama Uingereza nk imeziba masikio na midomo hazitoi kauli yoyote kulaani au kuunga mkono mauaji haya ya Israel dhidi ya raia wa Palestine tofauti kabisa na walivyo mstari wa mbele kwa mgongo wa Ukraine.

Vvyombo vya habari Moscow hasa vile vinavyosimamiwa na jeshi la Urusi kama vile RUDENKO na vingine, Vimerejea Hotuba ya Rais Putin aliyoitoa 01.07.2016 akionya Finland isikiuke miiko na kujiunga NATO.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ni kama alitabiri nyuma mnamo 2016 nini kitatokea ikiwa Finland itajiunga na NATO.

Kulingana na hutiba ya Rais Putin, kwa kujiunga kwa Finland katika Umoja wa Kujihami NATO, wanajeshi wa Ufini hawatakuwa huru tena. Watakuwa sehemu ya miundombinu ya kijeshi ya NATO, ambayo itaonekana ghafla kwenye mipaka ya Shirikisho la Urusi.

Putin: "NATO itafurahi kupigana na Urusi hadi mwanajeshi wa mwisho wa Kifini, Fikiria Finland inajiunga na NATO. Unafikiri tutaendelea kufanya hivi: askari wetu wameondoka hadi kilomita 1,500, kwa hiyo watabakia huko, au vipi? Tunathamini hali ya kutofungamana ya Finland na kuiheshimu, lakini sio kwetu sisi kutatua suala hili.

Ili kufafanua taarifa ya mmoja wa marafiki zangu wa Kifini, naweza kusema kwamba shirika la NATO labda lingefurahi kupigana na Urusi hadi askari wa mwisho wa Kifini. Unaihitaji?".

Hotuba hii aliitoa miaka sita iliyopita, Leo Finland inatumia mwanya wa mgogoro wa Ukraine inaamua kujiunga na NATO kwa shinikizo la Uingereza na Marekani. Nini jibu la Moscow? Tuendelee kusonga mbele.

Rais wa zamani wa Urusi na Makamu Mwenyekiti wa sasa wa Baraza la Usalama la Urusi Dmitry Medvedev ameonya Marekani na Ulaya kwa misaada wanayoendelea kuitoa kwa Ukraine na kwamba kitendo hicho ni kutangaza vita rasmi na Moscow. Amesema Moscow iko tayari kujibu iwe mchana au usiku lakini haitakaa kimya usalama wake ukitishiwa.

Mkuu wa Usafirishaji gas ya Urusi nchini Ukraine bwana Sergiy Makogon amesema wamefunga valvu mbili kati ya zile zinazosafirisha gas kwenda Ulaya. Hatua hiyo ni sehemu ya vikwazo vya Ulaya na Marekani kwa Urusi. Sergiy Makogon amesema Ukraine itaendelea kuchukua hatua zaidi kadiri muda unavyokwenda. Mataifa ya Ulaya yote yanapata gas ya Urusi kupitia mabomba yaliyotandazwa toka Urusi kupitia Ukraine hadi Ujerumani.

Ikulu ya Kremlin imesema mji wa Kherson utaunganishwa na Crimea kuwa eneo la Urusi au utaunganishwa kuwa eneo la Donetsk kulingana na matakwa ya Wananchi wa Kherson. Mji huo uko chini ya Majeshi ya Urusi tangu ulipotekwa ambapo sasa mji huo unapata huduma zote za kiserikali kijamii nk kutoka Moscow.

Msemaji wa Ikulu ya White House Bwana Ned Price amesema nchi yake haifadhili harakati za Taiwan kujitenga na China, Hatua hiyo imekuja baada ya China kuionya Marekani iache kuchochea uasi wa Taiwa kwa China. Wiki juzi China ilipewa taarifa za kijasusi kutoka shirika la Ujasusi la Urusi la FSB kwamba kuna kikao cha maafisa wa juu wa Uingereza na Marekani kimekalika kwamadhimuni ya kuinjinia uasi wa Taiwan kwa China, Taarifa hizo zilikuwa sahihi kwani Idara ya Usalama China ya Ministry of State Security [MSS] pia ilikuwa na taarifa hizo japo haikujua muda na mahali kikao hicho kitakapofanyika, hivyo Taarifa ya Moscow ilikuwa mwarobaini kwa China.

Makomandoo 405 wa Chechnia wamepelekwa uwanja wa vita huko Luhansk kuongeza nguvu, Chechnia inapigana begakwabega na Urusi kuhakikisha Jamhuri za Donetsk na Luhansk zinakuwa Huru, ambapo tayari Donetsk imeshakombolewa na iko chini ya majeshi ya Jamhuri ya Donetsk, huku Luhansk inaendelea kurindima makombora kila upande kuanzia Kharkiv, Izium, hadi mjini Luhansk.

Baada ya Finland na Sweden kuwasilisha rasmi maombi ya kujiunga na NATO, Kampuni ya INTER RAO ya Urusi ambayo ndio msambaji wa umeme nchini Finland imesema itakata huduma ya umeme kesho 14 May 2022. Hatua hiyo inafuatia Ufini kukiuka makubaliano ya kutofungamana na upande wowote.

Vatican imebadili maneno iliyoyatoa juzi ambapo ililaani upelekaji wa silaha Ukraine nw kusema ni kuchochea vita, ambapo leo Kadinali Yeptero Parolin, Katibu wa Serikali na Mjumbe wa Pili wa Vatikani, amekaririwa akisema, Kutuma silaha kwa Ukraine ni halali kimaadili, Akirejelea mafundisho ya Kanisa Katoliki, Kadinali Yeptero Parolin, Katibu wa serikali na mjumbe wa pili wa Vatikani, amesema kwamba kukidhi mahitaji ya silaha za Ukraine ili kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi ni "halali ya kimaadili chini ya masharti fulani."

Vikosi vya Urusi vimeendelea na Opareshe leo kwa kushambulia kwa nguvu kubwa maeneo ya Khakyiv, huku vikosi vinavyoendelea kushika doria kule Azovstal Steel vikiendelea kushusha mvua ya makombora na kuvuka uzio mkubwa wa kiwanda hicho tayari kuelekea ndani. Nako katika mji wa Avdiivka usiku mzima wa leo kumekumbwa na mashambulizi makali ambapo vikosi vya Urusi vilikumbana na kizuizi cha makuruta wa Ukraine, na hatimaye Majeshi ya urusi yametwaa mji huo baada ya kuvishinda vikosi vya makuruta toka Ukraine.

Kwa mara ya kwanza, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Jenerali Shoigu amezungumza na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin katika mazungumzo ya kwanza tangu operesheni ya Urusi nchini Ukraine kuanza.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani ya Pentagon imesema upande wa Marekani ulisisitiza umuhimu wa kuweka mawasiliano wazi, na kuhimiza usitishaji wa mapigano uanzishwe. Huku upande wa Moscow ukisisitiza Marekani iache kuingilia Oparesheni ya Moscow nchini Ukraine kwakufadhili siala na Ujasusi.

Waziri wa Mashuri ya Kigeni wa Urusi Sergey Lavrov ameelezea mashaka yake juu ya ombi la Ukraine la kujiunga na EU - akisema kuwa Umoja huo unageuka kuwa mwigizaji pinzani na matamanio zaidi ya bara la Ulaya. Kimsingi Urusi itajenga ukuta wa kinchi baina yake na NATO eneo lolote penye mashaka ya kiuslama kama inavyofanya leo kuhakikisha inadhibiti kila mashaka juu yake.

Waandishi watatu wa Habari wa kituo cha runinga cha Rassia today tv, ripota wa habari Bwana Valentin Gorshenin na wapiga picha/video Vladimir Batalin na Viktor Miroshnikov wamejeruhiwa kwa riketi la Ukraine lilirushwa katika mji wa Dokuchaevsk huko Jamhuri ya watu wa Donetsk. Eneo hilo liko chini ya Urusi lakini mashambulizi ya rasharasha bado yako.

Kikosi cha Wadunguaji (Snipers) wa Urusi kutoka kikosi cha 22nd GRU Special Forces Brigade wamefanikiwa kuwadungua wadunguaji wa Ukraine waliokuwa wamejichimbia kwa muda mrefu katika eneo la Donbass, kikosi cha Urusi cha 22nd GRU Special Forces Brigade ni maalumu kwa udunguaji ambapo kimefanikiwa kusafisha maeneo mengi katika Oparesheni hii na kinasifika kwa shabaha za hali ya juu duniani.

Mizinga ya roketi ya Jeshi la Urusi imeangamiza eneo muhimu la kimbinu la Ukraine na vifaa vya Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine huko Donbass, mwelekeo wa Liman. Huko kwingineko jioni ya leo, madaraja matatu muhimu kwa uhamishaji wa vikosi vya Ukraine yalipuliwa katika mkoa wa Kharkiv, madaraja hayo ni karibu na makazi ya Stary Saltov, Pechenegi na Rubezhnoye.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan amesema Finland na Swideni ni nyumbani kwa magaidi, Na Kwamba Uturuki inapinga kwanguvu zote uanachama wa nchi hizo katika NATO. Na ikilazimu itapinga kijeshi. Tangu oparesheni ya Urusi nchini Ukraine mnamo 22 Februari 2022, maoni ya umma na vyama vya Finland na Uswidi vimeonyesha mwelekeo usio na hasi wa kujiunga na NATO, huku maafisa wa serikali ya Finland wakitangaza jana kuwa nia ya Finland ya kujiunga na muungano huo. Finland inatarajiwa kutangaza uamuzi wake kesho kutwa Jumapili.

Urusi imepuuza propaganda zinazofanywa na Shirika la Ujasusi la Uingereza MI6 kwamba leo Ukraine imeangamiza vifaru na askari wa Urusi zaidi ya 1,000 waolitaka kuvuka mto Siversky unaopakana na Donetsk na Luhansk. Kamanda wa vikosi vya Urusi nchini Ukraine Jenerali Alexander Dvornikov amesema propaganda hizo zimetolewa na Jasusi wa Uingereza anayeendesha kampuni la Ujasusi la Sibylline Ltd ambalo liko Ukraine likiendesha Ujasusi kwaajili yw Ukraine, na kusambazwa na wanamgambo wa Ukraine taarifa ambayo ni kinyume chake.

Yericco Nyerere
 
Resources zote za Russia zitaguswa safari hii.

Hadi kufikia December Putin atazidi kuchoka kwasababu nchi yake hivisasa IPO busy na vita, hujuma ndani ya nchi yake, vikwazo vya uchumi na ugonjwa wake WA cancer.

Kwa kifupi huyu Fala kuingia choo cha kike bila kujua
 
Russia hana uchumi mzuri usimlaumu mkuu wa jeshi la anga. Russia anategemea mikwara na kupigana vita za kina Syria na Libya ila mataifa makubwa yanamtoa jasho.

Wala wasiwasi wangu juu ya uwezo wake haujaanza vita hii, ule upinzani wa Uturuki waliouonesha pale Libya, Syria na Azerbaijan dhidi ya Russia nilianza kuwa na wasiwasi na silaha za Urusi.

Mkuu si unakumbuka Ukraine ilienda mbio kununua hizo Bayraktar TB2 baada ya kuona kila zinakokutana na silaha za Mrusi zinapiga.

Uzuri wenzetu wanafanya analysis hawasikilizi propaganda, Urusi miaka yote huwa inalaumu wale iliowauzia silaha kwamba hawafanyi training vizuri na maintenance ndio maana wanafeli ila hii hapa yenyewe inashindwa kuzitumia effectively.

Russian airforce zile fighters zao walizifunga electronic jamming pods ila zikawa zinadondoshwa kama kawaida. Technology yao sio kubwa sana
 
Wangekuwa na iyo teknolojia wasingekimbia kwa wataliban
 
Sawa Urusi hana tekcholojia kubwa je nani anayo?.maana hakuna ambaye yupo perfect kwenye uwanja wa vita.
 
Kama marekani na Nato wametumia silaha zote pale Afghanistan zaidi ya miaka 20 na mwisho wa siku wakanyanyua mikono juu unategemea nao wana maajabu gani kwenye uwanja wa vita.

Wote wanapiga porojo tu kwenye upande wa silaha ila kazi ni zile zile tu hakuna mwenye silaha bora
 
When sanctions hits you back, so hard than your enemy.
Ndani ya Miezi mitatu Euro inazidi kupoteza thamani, now its almost level up with Dollar. It's 1vs1.04 from 1vs1.14 in February, a drop of around 10%.

For us who have savings in this currency, ni sawa na kusema tumepoteza 10% of Value of our savings in three months.

Up to Feb, let say ulikuwa na savings ya 10k Euro, ulikuwa na around 26.4M but now, if you want to withdrawal all your money. Utapata around 24.7Mil. A loss of around 2M within 3 months.

This is just as low as 10k, Can you guess how much people have lost kwa wale walio na savings kubwa zaidi kwenye hii currency?
 
Sioni msaada wake maana warusi wanazidi kusonga mbele.vha kushangaza wa Ukraine wanavunja madaraja ili Warusi wasipite,sasa je wao hawaitaji tena hayo maeneo.
Nilizungumza kuhusu hizi M777s hotwizers zenye uwezo wa kupiga 40 kms away Sasa kazi yake mmeiona. Yani kwa silaha za kuazima Ukraine wanamjambisha Putin, je wakipigana na USA baba lao [emoji848] View attachment 2223541View attachment 2223542
 
Unaposema "US mwenyewe" unataka kutuaminisha kuwa USA ni bora sana!!!?
Ikiwa umejiaminisha hivyo,itakuwa movie za kimarekani zinakuhadaa sana. Marekani popote anapokwenda anakuwa na mabaunsa wake. NATO.

Akisogeza pua peke yake,na asitumie silaha za maangamizi basi hata JWTz wanawakalisha. Kama wasomali walivyowafanya.
Ndio sababu hataki nchi zingine ziwe na silaha za maangamizi,kwani ubabe wake utatamatika. Na kutokana na unyama na wizi aliowafanyia wengine,wangemfuta kwenye ramani ya dunia

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
na ww unaamin kuwa kwa kila distance itachukua 2min?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…