Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?


Mwanangu, kwenda ku google vitu haraka haraka na kurudi hapa vitakuchanganya, aanza kusoma historia ya Ukraine kuanzia 2004 ndo utapata ufafanuzi.

Ndoto ya Ukraine kuingia NATO ilianza 2008 na mwaka 2010 ikakufa kutokana na kuchaguliwa raisi pro Kremlin. Kuanzia kipindi hicho mpaka 2014 jamaa walikua Neutral/pro Kremlin.

Mwaka huo 2014, Viktor yanukovych raisi wa Ukraine Pro Kremlin alikataa Ku sign mkataba ambao ungewezesha Ukraine na EU kushirikiana bila vikwazo. Hapo ndipo wakaanzisha revolution na kumuondoa madarakani.

Muda kidogo urussi ikaivamia Ukraine, na hapo ndo wakafufua mpango wa kujiunga na NATO. Sasa ukisema Russia iliivamia Ukraine kwa kuingia NATO unajidanganya mwenyewe na Chawa wenzako wa Russia. Sababu kuu ni kuwacha kuegema Kremlin na kugeukia Euro vision.
 
Unapotetea nchi isiyo ya kwako lazima uwe na akiba ya maneno hata kama utaonekana mnafiki.

Leo unatokwa na mishipa ukiitetea Europe na USA, ila jana kuna nchi ya Europe ilitawala nchi yako na kuwatesa watu wako na kesho huna hakika watafanya nini kwa wajukuu zako.

Kwangu mm ni mwendo wa kukemea tendo sio kutengeneza mahaba ya kudumu na nchi. Unaitetea USA kwa mahaba yote kesho unasikia inawekea vikwazo nchi zisizosapoti ndoa ya jinsia moja utaficha wapi sura yako?

Unaitetea Urusi kwa nguvu zote kesho unasikia inaitaka Tz kuacha kushirikiana na USA kutengeneza silaha au itaivamia unaficha wapi sura yako?
 
Bado umelala
 
Huo ni mwanzo tu, pale Poland nasikia kuna Raia wamempiga hadi kumuua.
 
USA alipeleka askari 2,700,000 kwenye ardhi ya Vietnam kwa ajili ya kupigania vita,
Vita aliyopigwa na kushindwa vibaya.

Sijui unaposema hakupigana mwenyewe, una maana gani?

Mwanzoni alianza kusaidia Wafaransa na south Vietnam waliokuwa wanapigana na Vietcong ila kwenye battle ya BIEN DIEN PHU waviet Cong walishinda na mfaransa kupigwa, hivyo hakuwa na jinsi ikamlazimu aingie vitani Moja kwa Moja.

Ambapo alikutana na dhahama kubwa mpaka kutumia chemical weapons maarufu kama agent orange.

Na Bado alishindwa vita.
 
Biashara huru? duniani.

Mkuu Hebu tuelezee hapo vizuri tukuelewe
 
Tunalazimika kukujibu ilhali unajaribu kupotosha ukweli.

Yanukovch alipinduliwa 2014 kwa sababu ya mlengo wake kuelekea Kremlin, upo sahihi.
Je mapinduzi yale, yalifanywa kwa kutumia mgongo wa nani?
Unakataa kwamba yalifadhiliwa na Marekani pamoja na washirika wake?

Kama hapana naomba unielezee kwa nini Victoria Nuland ambaye ni undersecretary of political affair alikuwa anafanya nini maiden square wakati wakimlazimisha yanukovch ajiuzulu?

Je mashinikizo Yale ya waandamaji yalikuwa na baraka za nchi nzima??!!
Jibu ni hapana, ndio maana upande wa mashariki uliamua kujitenga na kuokutambua serikari iliyopo kiev na Kuanzishwa Jamhuri zao.

Kwa nini useme Urusi iliivamia Ukraine 2014 wakati wananchi wenyewe ndio waliotangaza kutoitambua serikari ya kiev?

Acha ubangalala
 
Swali lako lina dalili zote za mtu mwenye uvivu wa kufikiri hivo linaleta uvivu pia kulijibu ila kujibu kwa faida ya wengine ni kwamba Marekani walienda Vietnam kuzuia Vietnam ya Kusini isichukuliwe na Vietnam ya Kaskazini iliyokuwa ya Kikomunisti ambayo ndio ilikuwa muanzilishi wa vita. US walifanikiwa kuzuia hilo kwa muda wa miaka 8 ambayo majeshi yake yalikuwa huko na miaka mingine 2 baada ya majeshi yake kuondoka.

Hawakwenda Vietnam kuteka vijiji kama unavyojaribu kulisha watu hayo matangopori. Walienda kuzuia upande wa Vietnam Kusini usianguke dhidi ya majeshi ya Kikomunisti ya Kaskazini.

Vita vya Vietnam ni sawa na vita vya Korea Kusini na Kaskazini, tofauti ni kwamba US haikuwahi kuondoa Korea Kusini mpaka leo na iliendelea kuipa msaada. Vita ya Vietnam ilipoteza ushawashi kwenye siasa za Marekani na msaada kwa serikali ya Vietnam Kusini ukakatwa.

Hujajibu hoja zangu Marekani alienda kufanya nn nchini Uvitenam?
 
Ulichokiandika kinaleta jawabu la wazi kuwa hili sakata la Russia na mgogoro wa Ukraine umelijua baada ya kutokea vurumai inayoendelea sasa. Hii hali yote ilianzia 2008.


Kisha rudi tena mwaka 1992 "German Reunification" makubaliano yao. Hii itakuongoza kuona unachokiamini hakiko sahihi. Na hakuna shaka hakipo sahihi. Kisha rudi tena kipindi US alipoweka makombora yake ya nuclear Ugiriki na Uturuki hali iliyomlazimu USSR kuweka makombora ya nuclear Cuba. Mataifa makubwa yapo serious na usalama wa nchi yao. Kwa mambo jinsi yalivyo ilibidi wawekeane mipaka ya kutokusogeleana ili kila mtu awe na amani na usalama wa Taifa lake.
 
Haya mambo yanahitaji akili nyingi sana kuyaelewa, naweza kusema ushabiki sio tatizo maana kila mtu hubaki na kile anachoamini ila ushabiki na mahaba yakifikia kushinda uwezo wa kufikiri hilo ni tatizo. Kiasi cha kuanza kubadili uhalisia kuuweka katika mtazamo wa kuifurahisha nyoyo.

Ni sahihi kabisa katika siasa za kimataifa hakuna adui wala Rafiki wa kudumu isipokuwa kwenye masilahi.

Wakati Russia akisaidiana na Serikal ya Afghanistan kipindi hicho kupigana na kundi la Mujaheed hapo US, EU hii ya leo hadi China walikuwa wakitoa support kwa hilo kundi la Mujaheed dhidi ya Russiana serikali ya Afghanistan iliyokuepo wakati huo. 1979 hadi 1989... hii miaka itazame vizuri.

Kwenye vita ya Iran na Iraqi, Iraqi alipoivamia Iran alikuwa akipewa back up na US na kundi lake lote, hapo Soviet Union nao walikuwa upande wa Iraqi. West Germany na East Germany ya kipindi hicho nao walikaa upande wa Iraqi. Maajab Israel alikuwa upande wa Iran... 1980 hadi 1988.

Hapo Sadam Husein akitumika upande wa Iran huku Osama akitumika wa USSR. Ambao wote hawa waliopewa support mwanzo wakaja vamiwa na US akidai ni makundi ya Ugaidi.

Sasa angalia vizuri hiyo miaka... wakati huku anapigwa vita huku kule wanashirikiana on the same course...

Leo hii 2022... angalia mahusiano ya Israel na Iran waliosaidiana kuzuia Uvamizi wa Iraqi. Angalia mahusiano ya Russia na US walioshirikiana ku-support uvamizi wa Iraqi hapo Iran.

Angalia tena uhusiano wa West and East Germany ya kipindi hicho, Upande wa Afghanistan East Germany alikuwa akisupport Soviet huku West Germany akisupport wale Mujaheed. Upande wa Iraqi-Iran wakasimama pamoja upande wa Iraqi.

Dunia yetu hii ina Illusions kibao, kile unachokiona nje sio kile kilichomo ndani. Yawezekana n Blue Box ndani ya Chumba cha mwangaza wa Blue kumbe ni White Box ukilepeka kwenye chumba cha mwangaza mweupe.

Unapata tafsiri ya kitu kutokana na mazingira uliyopo au kitu hicho kilipo. Ila haina maana kua ndio ukweli bali perceptions that need to be weighed with free mind ili ukihukum ni sawa au si sawa.

Ushabiki kawaida ila ushabiki wa kujitoa akili ni UZUZU na UPUMBAFU wa hali ya Juu.
 
True
 
Mwanangu Ku Google vitu randomly kutakuchanganya. At no given point wanajeshi wa Amerika walifika zaidi ya 550,000 ndani ya Vietnam. Hio 2.7m ni idadi ya wanajeshi waliokua deployed kwa ujumla.

Alafu ukisema Amerika ilipigwa vibaya kwa kupoteza majeshi 50,000 nataka ujue adui alipoteza takriban wanajeshi millioni moja, hapo ratio ni 1:20, ama kweli Amerika ilipigika vibaya.
 
Jomba kama ni kitabu hiki nikusumbue unitumie ase...
 
Unasema us hakupigana ddirect, hivi unajua kisa cha muhamad ally kuvuliwa taji kwa kukataa kupigana vietnam. Ndio maana tunasema pronato ni weupe hamna hoja zaidi ya ushabik
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…