Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Taarifa ya mwisho iliyotoka Russia ni kuwa hawako kwenye mazungumzo yoyote na Ukraine!Sasa wewe hayo umeyatoa wapi?
Zalensky mwenyewe hajasema kuwa amepewa demands hizo,alichosema ni kuwa Ukraine haitakubali mazungumzo ya kumaliza vita yahusishe kuachia sehemu ya ardhi yake!Swali kwako,wewe hizo demands za Russia umezitoa wapi?
Kwa Mykhailo Podolyk, Mshauri wa Rais wa Ukraine. Tazama taarifa zote za habari duniani za vyombo vikubwa wameripoti.
 
Taarifa mbona nimeleta kama ilivyo au hujaisoma umeishia heading tu. Na kama umeishia heading hilo ni tatizo lako huenda labda haina umuhimu kwako.
Bado umeendelea kuandika imetupilia mbali wakati kiuhalisia hakuna kilichotupiliwa mbali kwani hakuna taarifa ya mazungumzo ya pande zote mbili kuendelea!
 
Hapana sijui kwamba Urusi iko mbele katika tekinolojia ya kijeshi.
Mimi si mtaalamu katika mambo haya. Nimefuata habari za roketi kidogo. Hapa naona katika tekinolojia kwamba Urusi inaendelea kutumia vyombo kama Soyuz vinavyoendelea bila mabadiliko makubwa tangu miaka 40 hivi... Vilifanya vizuri, wakati MArekani ilishindwa na Space Shuttle. Lakini sasa kuna tekinolojia mpya ya roketi zinazorudi ili zitumiwe tena na hapa hakuna dalili hata kidogo Urusi kuna kitu kama hicho...

Nimeangalia habari za kifaru T14 Armata. Ilisifiwa kama kifaru bora duniani, kumbe wana mahandisi bora! Ila kifaru hakipo hali halisi walishindwa kukitengeneza, wengine wanasema ni kiuchumi hawana hela,, wengine wanasema ni vipuli kutoka Marekani ambako Urui ilipoigwa vikwazo tangu 2014...

Nimeangalia wachambuzi wanaodai eti Urusi wana mahandisi wazuri lakini tasnia ya silaha ina matatizo kutoa silaha bora, wana matatizo ya kuhakikisha ubora. hii sababu kwamba hawana roketi nyingi za kisasa. Basi kama ni kweli tutaona karibuni kama wataishia roketi na grenedi za kisasa zinazolengwa kwa GPS.
Ila inaonekana kuna tatizo nzito maana Urusi imeshindwa kudhibiti anga. Wengi wanashangaa maana wote walitegemea watamaliza swali hili kwenye siku ya pili au ya tatu baada ya uvamizi (jinsi Marekani walivyofanya Iraki na Afghanistan).
Hapa kuna swali kama ni kasoro za tekinolojia au uongozi??

Kwa sasa wanaendelea kwa kutumia mkakati akma zamani. Wanaleta mizinga mingi mbele, wanasaga kila kitu halafu wanasogea mbele kidogo.
Tuone itakuwaje mara Ukraine wanapeleka idadi ya mizinga ya kimarekani mbele ambazo zipiga mbali zaidi kuliko zile za kirusi, tena wamepata idadi kubwa ya grenedi za GPS.

Ile kujigamba dhidi ya Uingereza ni kitoto. Maana Urusi isingepiga Uingereza peke yake. Ingepata jibu la NATO kwa jumla na hapa isingekuwepo Urusi tena. Wanaijua. kwa hiyo ni kazi ya wanasiasa kupiga kelele tu... (pamoja na usharika wa waumini wa putin kuitikia..)
Hujui unachoandika rocket na anga . Hivi nani anamiliki anga hao Nato wanarusha ndege ama drone ngapi na zinasalimika ngapi. Russia ni baba yao .

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Kwa Mykhailo Podolyk, Mshauri wa Rais wa Ukraine. Tazama taarifa zote za habari duniani za vyombo vikubwa wameripoti.
Mimi mwenyewe nimeangalia BBC na Aljazeera,alichokisema ni kuwa Ukraine haitakubali kuachia sehemu ya ardhi yake kama sehemu ya kumaliza vita!
Hiyo amesema kama precaution tu na sio kwamba Russia wamemwambia demands zake ni hizo!Muwe mnasikiliza vizuri taarifa kabla ya kuja kuandika hapa!
 
Kwanza nashukru umekiri wameripoti , kwahiyo hapa ni unabishana tu.

Wewe ndo usikilizi vizuri, nazani Unatakiwa uongeze umakini zaidi wakati wa kusikiliza, pili usiishie kusikiliza tu, bali isome pia hiyo taarifa.

Mwisho umeambiwa amekataa mpango huo na sababu zake ni hizo, sasa hapo unachobishia ni nini au kipi hujaelewa.
 
Hata wao hii technology wanadai hawaifahamu (wanasema ni imaginary)
Coz inatumia mionzi kuchoma drone iliyo umbali Zaid ya km 5

Hii Vita inaweza kuonyesha uhalisia wa silaha za ajabu walizonazo RUSSIA
Bro USA ndo nchi ya Kwanza kufanya testing ya laser weapons, tatizo nadhan ni sababu jamaa hawapendi Sana kuzinadi silaha zao Kama nchi za kikomunisti wanavyofanya ili kutisha mataifa mengine Kama vile kila siku wanavyotishia nuclear utafikiri wanayo peke Yao

Hii hapa walifanya live demonstration ya laser weapons mwaka 2017

Tafadhali utueleze namna gani ni vikwazo vya magharibi? Urusi inazuia meli za ngano kutoka Odessa. Au ni NATO inayozuia ngano ya Ukraine kufika masoko ya dunia???
Russia ndio mzalishaji namba Moja wa ngano duniani,Ukraine ni wa 5!Russia amezuiwa meli zake kutia nanga kwenye nchi za EU na US!
Canada naye yupo top 5 Kwa uzalishaji ngano,Sasa hapo huoni tatizo linaanzia Kwa muweka vikwazo?
Kama ambavyo Russia amewekewa vikwazo Ili uchumi uyumbe na ashindwe vita,na yeye Ndivyo anvyoiminya Ukraine Ili iwe unbalanced na ashindwe vita kirahisi! Matokeo yake ndio hayo!
 
Putin anaanza kuua Waafrika kwa njia ya njaa kwa sababu ameshambulia Ukraine. Nafaka za Ukraine haziwezi kupelekwa tena kwenye masoko ya Dunia. Bei zinapanda. Watu maskini wanaona njaa. Hasa nchi kama Ethiopia, Somalia na Kenya zinazotegemea misaada kutoka mashirika ya kimataifa ambayo yanakosa hela kulipa bei mpya.

Waumini wake wanaendelea kumwabudu . . .
Unachekesha sana wewe, kwahio atapiga ifakara shinyanga babati mbeya iringa na sehemu kadja Wa kadha kinapo toka chakula cha nchi? Yaani pro NATO mnaongeaga utumbo mpaka mnapitiliza, Mwafrika hategemei ngano pekee kama ndio chakula kikuu
 
Kwanza nashukru umekiri wameripoti , kwahiyo hapa ni unabishana tu.

Wewe ndo usikilizi vizuri, nazani Unatakiwa uongeze umakini zaidi wakati wa kusikiliza, pili usiishie kusikiliza tu, bali isome pia hiyo taarifa.

Mwisho umeambiwa amekataa mpango huo na sababu zake ni hizo, sasa hapo unachobishia ni nini au kipi hujaelewa.
Amesema Ukraine haitakubali Mpango wowote wa kuimega ardhi yake kama sehemu ya kumaliza vita!
Hakuna mahala popote ambapo amesema kwamba Russia wamedemand hivyo!Kumbuka mazungumzo ya Ukraine na Russia yalikwama kuendelea kabla hata Russia hajaikamata Mariupol!
Sasa nauliza,hizo demands za Russia zimepatikana kwenye kikao kipi?
Sio Zalensky Wala mshauri wake waliosema kwamba wameambiwa hayo!
 
Sielewi hata unabishana nini, Majibu aliyoyatoa Mykhailo Podolyk yanathibitisha wameambiwa hivyo kwenye mazungumzo hayo.
 
Kila siku Biden anaomba pesa , unafikiri Iraq ilikua hivi? huyu Ndio Putin kiranja mkuu wa ulimwengu anae pambana na Ukraine pamoja na sponsors wake na bado wanalia lia kama Mbwa

Aguze kataifa kamoja ka NATO hapo ndio ataelewa nini maana ya kupambana, kwa aibu aliyopata Ukraine, amebaki wa hovyoo sana.
 
Unachekesha sana wewe, kwahio atapiga ifakara shinyanga babati mbeya iringa na sehemu kadja Wa kadha kinapo toka chakula cha nchi? Yaani pro NATO mnaongeaga utumbo mpaka mnapitiliza, Mwafrika hategemei ngano pekee kama ndio chakula kikuu
Tafadhali usome ninachoandika na utafakari vema. Tanzania kwa bahati nzuri ina mazao yanayoweza kuuzwa nje. Tunaona matokeo katika kupanda bei ya unga wa ngano (Tanzania inanunua kiasi nje) na mafuta maana Ukraineni namba 1 kuzalisha mafuta ya alizeti duniani.
Hali ni ngumu katika nchi jirani kama ethiopia, Somalia na Kenya (na nchi nyingi nyingine) ambazo hazizalishi chakula cha kutosha zinategemea kuingiza vyakula kutoka nje.
Hasa mamilioni ya wakimbizi wanaotegemea msaada wa chakula kutoka taasisi za kimataifa kama WFP wana matatizo kwa sababu taasisi hizo hazina pesa ya kutosha baada ya kupanda kwa bei.
Angalia nani anachangia, utaona wengi wenaolaumiwa hapa kama watu wabaya... (Urusi inafuata kama donor kwenye nafasi ya 22!!)

Contributions to World Food Programme in 2021
TOTAL CONTRIBUTIONS: US$ 9.555.606.656

as of 28 April 2022
All Donors (including Flexible)
1 USA 3.779.709.324
2 Germany 1.413.997.469
3 European Commission 497.938.815
4 United Kingdom 376.260.054
5 Canada 313.342.498
6 World Bank 272.581.274
7 * Saudi Arabia 259.000.081
8 Japan 226.187.020
9 Private Donors 205.295.029
10 Pakistan 204.123.733
11 Sweden 173.499.276
12 Norway 162.903.799

Shirikisha akili japo kwa mbali, ukraine anatumika Kama Dalali wa aliyejaribu kuwa mwenyeji wa maadu wa urusi, huo ugomvi wanaopigana ni USA wakipiga corabo na NATO VS RUSSIA. Uzuri RUSSIA ina Assumptions zote yanaweza tokea na taadhari zake, ndio maana sanctions na Mambo mengine hayana effects mbaya Kama West walivyofikiri, risks na mitigations hii vita Russia walishafanya..hapo ni kusali tu imalizike kwa adabu.

Hehehe mnatafuta vijisababu vya kufutia aibu, mwambieni aguze kataifa kamoja ka NATO ndio ajue wamemtamani sana.
 
Russia ndio mzalishaji namba Moja wa ngano duniani,Ukraine ni wa 5!Russia amezuiwa meli zake kutia nanga kwenye nchi za EU na US!
Canada naye yupo top 5 Kwa uzalishaji ngano,Sasa hapo huoni tatizo linaanzia Kwa muweka vikwazo?
Kama ambavyo Russia amewekewa vikwazo Ili uchumi uyumbe na ashindwe vita,na yeye Ndivyo anvyoiminya Ukraine Ili iwe unbalanced na ashindwe vita kirahisi! Matokeo yake ndio hayo!
Sijakana Urusi inauza pia . Hakuna anayezuia meli za Urusi kubeba ngano yake isipokuwa kwenye nchi za NATO zinazoweka vikwazo dhidi ya Urusi (sina uhakika kama kuna vikwazo dhidi ya chakula kutoka Urusi - je unazo habari za uhakika??)
Ila kumzuia mwuzaji mkubwa kama Ukraine inatosha kupamndisha bei - hii inamaanisha njaa na vifo.
Kweli au la???
 
Sielewi hata unabishana nini, Majibu aliyoyatoa Mykhailo Podolyk yanathibitisha wameambiwa hivyo kwenye mazungumzo hayo.
Niliwaambia hapa vita Russia kashinda baada ya Mauripol .Russia ameongeza dozi kidogo sio yote tayari wameshika adabu. Ni namna ya kutoa kombe tu . Zelensky atoke mwenyewe au USA wamalize kisha waingie makubaliano na Russia. Zelensky kesha tumia fedha ya Watu lazma awajibike yeye binafsi.Biden katumia fedha ya walipakodi USA lazma awajibike.

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Hujui unachoandika rocket na anga . Hivi nani anamiliki anga hao Nato wanarusha ndege ama drone ngapi na zinasalimika ngapi. Russia ni baba yao .

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
Hujagusa yale nilyosema kuhusu roketi. Kama Urusi ni baba au babu au nini sijali,
Katika tekinolojia ya roketi sijaona mfano unaolingana na roketi za Space-X nilizotaja,. Kama una mfano halisi, ninashukuru kuiona! Karibu kunifundisha!!
 
Hapana sijui kwamba Urusi iko mbele katika tekinolojia ya kijeshi.
Mimi si mtaalamu katika mambo haya. Nimefuata habari za roketi kidogo. Hapa naona katika tekinolojia kwamba Urusi inaendelea kutumia vyombo kama Soyuz vinavyoendelea bila mabadiliko makubwa tangu miaka 40 hivi... Vilifanya vizuri, wakati MArekani ilishindwa na Space Shuttle. Lakini sasa kuna tekinolojia mpya ya roketi zinazorudi ili zitumiwe tena na hapa hakuna dalili hata kidogo Urusi kuna kitu kama hicho...

Nimeangalia habari za kifaru T14 Armata. Ilisifiwa kama kifaru bora duniani, kumbe wana mahandisi bora! Ila kifaru hakipo hali halisi walishindwa kukitengeneza, wengine wanasema ni kiuchumi hawana hela,, wengine wanasema ni vipuli kutoka Marekani ambako Urui ilipoigwa vikwazo tangu 2014...

Nimeangalia wachambuzi wanaodai eti Urusi wana mahandisi wazuri lakini tasnia ya silaha ina matatizo kutoa silaha bora, wana matatizo ya kuhakikisha ubora. hii sababu kwamba hawana roketi nyingi za kisasa. Basi kama ni kweli tutaona karibuni kama wataishia roketi na grenedi za kisasa zinazolengwa kwa GPS.
Ila inaonekana kuna tatizo nzito maana Urusi imeshindwa kudhibiti anga. Wengi wanashangaa maana wote walitegemea watamaliza swali hili kwenye siku ya pili au ya tatu baada ya uvamizi (jinsi Marekani walivyofanya Iraki na Afghanistan).
Hapa kuna swali kama ni kasoro za tekinolojia au uongozi??

Kwa sasa wanaendelea kwa kutumia mkakati akma zamani. Wanaleta mizinga mingi mbele, wanasaga kila kitu halafu wanasogea mbele kidogo.
Tuone itakuwaje mara Ukraine wanapeleka idadi ya mizinga ya kimarekani mbele ambazo zipiga mbali zaidi kuliko zile za kirusi, tena wamepata idadi kubwa ya grenedi za GPS.

Ile kujigamba dhidi ya Uingereza ni kitoto. Maana Urusi isingepiga Uingereza peke yake. Ingepata jibu la NATO kwa jumla na hapa isingekuwepo Urusi tena. Wanaijua. kwa hiyo ni kazi ya wanasiasa kupiga kelele tu... (pamoja na usharika wa waumini wa putin kuitikia..)
Duuh,Kuna eneo umeonekana uko shallow halafu unajiita mtaalam!Hivi unaelewa kinachofanyika Ili hizo rocket engines zije kuwa reused?Ni kwamba zamani Ilikuwa baada ya kufika height fulani,zinaachwa zianguke free fall ,hizo kazi yake ni kuipa shuttle initial take off velocity!Ikifika height fulani zinajitenga na shuttle na kuanguka ardhini hivyo kuharibika!Sasa US walivyofanya ni kufunga mfumo wa parachute kiasi kwamba wakati zinaanguka basi Parachute inajifungua!Ikijifungua,Kwa juu Kunakuwa na kama kile kichuma Cha Cha buchani Cha kutundikia nyama,baada ya hapo helcopter inaenda kudaka kile kichuma na hivyo kuipeleka hiyo engine sehemu salama na kuitua!
Wala sio kitu Cha ajabu sana,ni simple tu!
Sasa hapo unapoweka utafikiri ni binge la teknolojia unakuwa unakwama!

NB,:Kazi ya parachute iliyofunga ni kupunguza weight ya hiyo rocket Ili iweze kubebwa na helcopter!Kazi ya pili ni kufanya slower descend Ili helcopter iweze kuidaka Kwa kamba maalumu!
 
Niliwaambia hapa vita Russia kashinda baada ya Mauripol .Russia ameongeza dozi kidogo sio yote tayari wameshika adabu. Ni namna ya kutoa kombe tu . Zelensky atoke mwenyewe au USA wamalize kisha waingie makubaliano na Russia. Zelensky kesha tumia fedha ya Watu lazma awajibike yeye binafsi.Biden katumia fedha ya walipakodi USA lazma awajibike.

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
Angekuwa kasha shinda Putin angekuwa kashatangaza kumalizika kwa Vita. Vita bado inaendelea.
 
Back
Top Bottom