Hawe
USA kapata dhaifu wake wa kumpumulia kisogoni, miezi mitatu maneno haya hayajazungumza Ukraine. Mjerumani mwanzoni kabisa alikuwa na maneno ya vitisho kwa Russia kilichotokea Mrusi akasema maneno ya ujerumani ni tishio kwa usalama wa Urusi na warusi tutawapa jibu, muda si mrefu mbabe wa vita PUTIN akaagiza vikosi vyote viwe tayari kwa uvamizi kutoka Ujerumani hapohapo Germany akafyata mkia.
Ujerumani akaona hatari kubwa Russia ana hasira na WANAZI na Russia anapoiona Ujerumani taswira inayomjia ni HATARI YA WANAZI kwa ajili ya usalama wa nchi ya Urusi watakuwa tayari kutumia biological,chemical,nuclear na laser weapons kujilinda dhidi ya WANAZI.
China anapumuliwa kisogoni anakubali kweli USA kapata saizi yake.
Hawezi thubutu kwenda huko, kawaida ake na tamaduni ya US ni kuingiza wengine kwenye machafuko. Hata Ukraine alipewa ahadi kede kede wako wapi hivi sasa?
Kama walishindwa kumnyamazisha North Korea seuze China?
Kuna jomba mmoja alielezea sifa za hawa watu kiundani katika Psychology ya tabia.
Majigambo, ubabe wa mdomoni, Kupenda vurugu na mfanano wake ndio hulka zao ila katika Action hata kama wakipaka mkongo, wakanywa Viagra hata zile sekunde tatu hawatoboi....
Western size yao kule Somalia walikoelekea hapo wanampamba Taiwan aendelee kua mteja wao ila maafa yakiwakuta ndipo watajua ngozi halisi ya US.
Printers bado ziko active na bahati nzuri miti ya kutengenezea karatasi haijaisha. Wata print as much as they need wafungashe wapeleke.
AFAIK (As far as I know) ni kua China ni third katika world nuclear power, na ni Third katika world Most Powerful Country in term of Military power only behind Russia and US.
Kuna hii SCO inawajumuisha Russia and China, wana military alliance pia, wote tunamjua Russia hajawah na hana historia ya kuwatupa rafiki zake. Kama alifanya Venezuela na Syria just kwa kupokea maombi tu je kwa huyu China aliye karibu nae wanaeshare the same enemy zaidi huku akijua kuanguka kwa China kutamuathiri kama ambavyo China anaona kuanguka kwa Russia kutamuathiri?
Kwa kifupi US hawezi na hatoweza ataishia kubweka bweka kila leo na wapuuzi wenzao wataendelea kujinadi ma kujisifu kwa upuuzi huo.