We Bwana Mkubwa mwenye hekima, unasema kweli Afrika kuna ardhi yenye rutba. Kwa bahati mbaya rutba inajificha wakati hamna mvua. Kwa hiyo mavuno huko Kenya, zaidi Ethiopia na Somalia (pamoja na vita) yalifeli. Tokeo ni njaa na haja la kutafuta chakula nje.
Kama wewe, Bwana wa Hekima, unajua sababu nyingine kwa tatizo la njaa katika nchi hizo, tafadhali utuambie.
Au ukijua habari kwamba taarifa za njaa katika nchi hizo ni uwongo, tafadhali utuelimishe!!
Kwa sasa ninajua tu kwamba njaa iko, najua pia kwamba hawana uwezo kulipa bei za nafaka zilizopanda, kwamba taasisi kama World Food Programme (ambako Urusi inachangia kidogo sana, ilhali mabepari wabaya walipa kiasi kikubwa) haina pesa ya kutosha - na sababu kuu ni vita ya Putin na kufungwa kwa mabandari ya Ukraine.
Nikisubiri hekima yako kuhusu ukame, rutba na bei ya ngano, bado naona Putin analeta njaa na vifo hadi Afrika.