Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Zelensky aache madaraka mambo yaende …CIA wanaweza kula kichwa ..sio watu
Naaam
FUpbVkEXwAEhMw7.jpg
 
Wabongo bwana... mgogoro wa Urusi na Ukraine unatuhusu nini sisi? Sisi tuhangaike na mgogoro wa serikali na wamasai Ngorongoro; na mgogoro wa M23 Kongo.
Mgogoro wa serikali na wamasai unakuhusu nini wewe, waachie wamasai na viongozi wa serikali yako uliyo wachagua.
Sasa wote tukianza kushughulika na mgogoro huo, kazi ya viongozi tulio wachagua kufanya kazi zetu itakuwa ipi sasa,

Unacholazimisha tufanye nisawa na mtu amuajiri mtu wa kuchunga ng'ombe halafu bado aendelee kuchunga yeye huku akiendelea kumlipa mchunga ng'ombe huyo alie muajiri.

Kwahiyo mkuu Mwanafalsafa suala la wamasai lisikupe tabu kabisa. tumewaachia vibarua wetu kina mama samia, Waziri mkuu na mawaziri husika, DC, RC, watendaji wa kata na vijiji ambao tunawalipa kila mwezi kwa pesa za jasho letu, sisi tunasubiri matokeo tu, yakiwa yakipuuzi tutawachinja kwa vichinjio vyetu 2025.

Hivyo basi Acha tuendelee tu kudeal na hii operation kwa masilahi ya dunia na taifa letu pia, tunahitaji dunia yenye mataifa yanayojiamulia maamuzi yake menyewe pasipo kuathili taifa/mataifa mengine. nawenye uwezo wa kuleta hiyo balance of power kwasasa ni Russia na China tu (through millitary and economic power respectively) ndo maana unaona Tunasimama na Russia.

Nadhani nitakuwa nimeeleweka kwako na wenzio ambao bado hamuelewi kwanini tunasimama na Russia katika operation hii.
 
1.Weka ya hiyo treaty ya ya NATO kutosogea hata nchi moja kuelekea east, sema ilisainiwa lini wapi na viongozi gani wa NATO na USSR walisaini.

2.Rais wa Marekani hachaguliw na electors, anatokana na electoral votes college votes za majimbo . Electoral college votes zinatokana na popular votes. Kama Rais ameshinda jimbo anapewa Electoral votes za hilo jimbo, hakuna namna Electoral votes za mshindi wa jimbo zitaenda kwa mtu aliyeshindwa popular votes katika hilo jimbo, na hii iliwekwa hivyo makusudi na waandishi wa katiba ya US ili kuyapa sauti majimbo ambayo yalijiona ni madogo.

3.Ni Upumbavu kusema waziri mkuu wa Uingereza anachaguliwa na Malkia wakati kila mtu huwa anashuhudia uchaguzi mkuu wa Uingereza ukifanyika mara kwa mara na mawawziri wakuu wakiondolewa kuwa kura za kutokuwa na imani nao au kupoteza kwenye uchaguzi.

4.Uingereza, Canada, Japan, Israel, Ujerumani na nchi nyingine nyingi zina mfumo wa DEMOKRASIA wa waziri mkuu, kansela au kiongozi mkuu wa nchi kutoka katika chama kinachoshinda kwa kura nyingi au chama chenye kura nyingi kwenye uchaguzi kinachoweza kutengeneza coalition ya kuongiza nchi. Sijui kwa nini mfumo huh wewe unauona sio demokrasia! Sioni point wala mashiko kwa criticism yako, nafikiri ni uelewa wako finyu tu wa demokrasia ya uwakilishi.

5.Ni UONGO mtupu kwamba asilimia 90 ya ardhi ya Canada inamilikiwa na malkia. Huwezi kuthibitisha huu uongo wako kwa namna yoyote ile.
Hili nakubaliana na wewe 99%


Sure, na mie naamini hivyo...


Vita ya US ipo dhidi ya Putin wala hawana haja na Russia. Wanajua wakiweza kuicontrol Russia basi wametimiza agenda zao. Kuna kimoja hiki always huwa kinafanyika kwa kujirudia. Mikakati ikianza kila kitu huwa kinapelekwa kwa siri hadi pale kinapokaribia tamati ndio wanatangaza ujio wa 1 mbili 3.

Mfano, rejea kwa Walker Bush, baada ya kuvunjika ndio wakaliweka wazi issue ya USSR. 1991 up to 1999 ni kipindi ambacho mahusiano ya US na Russia yalistawi under Yeltsin.

Ni katika kipindi ambacho Russia ilianza kujazwa madeni. Kutoka 1991 hadi kufikia 1999 walikuwa na National debt over 134% ratio to GDP. Kwa wenye uelewa wanaelewa maana ya deni kwa Taifa ni nini.

Walipoweza kumjazia Russia madeni ndicho kipindi NATO walichaonza kuvunja treaty waliyoifunga ya kutosogea even an inch kuelekea East.

Kabla ya kuvunjika USSR, NATO ilikuwa na nchi 16 tu. 1999 wakati Yeltsin anatoka madarakani wakaongeza nchi 6 kwa mpigo zote hizi ikijitanua kuelekea mpakani mwq Russia. Waliongeza Bulgaria, Estonia, Latvia, Lithuania, Roma na Slovakia.

Kiu haikuishia hapo tu, 2004 wakamsogeza Slovenia... 2009 wakawasogeza Albania na Croatia. Kinachofurahisha ni kua Nchi hizo zinaongezwa NATO kwenye kipindi cha mabadiliko ya uongozi hapo Russia.

ie. Angalia 1999... Putin anaingia kama Acting President kabla ya 2000 kua Raisi Rasmi. 2004 kwa Slovenia ilikuwa ni mwisho wa term ya kwanza kwa Putin. 2009 ilikuwa ni enzi za Medvedev enzi hizo akichukuliwa poa poa. Hizi media za Magharibi zikawa zinatuambia kua Medvedev hana Itikadi za Putin.

2017, huo mwaka nao ukariri vizuri, NATO wakamsogeza Montenegro na 2020 wakamaliza na North Macedonia. Wakati huo huo wanampiga chapuo Ukraine kujiunga NATO.

Mind you kua ni kipindi chote hicho Russia chini ya Putin ilikuwa ikijijenga ndani kwa ndani. Na hatua ya kwanza aliyoifanya Putin ni kupunguza deni la taifa lake huko WB na IMF... Hizi taasisi sizani kama kuna haja ya kuzieleza naamini wazijua hata kwa uchache.

Alipofanikiwa kulishusha kutoka 134% hadi below 10% ratio to GDP, Ndipo alipoanza sasa rasm kuzimua aliyoyabeba. Kurejeshha Sovereignty halisi kwa Taifa lake... Georgian walijarib 2008 wanajua kilichotokea. Na ukubwa wa deni kwa mtu akitaka kuuelewa akaangalie kilichotokea SriLanka. Na ambacho US wanakilazimisha kwa Russia.

"Default" kitu ambacho ni ngumu kutokea kwasabau deni analoadaiwa Russia anaweza kulilipa na chenchi zikabaki. Je ingekuwa zile enzi deni linazidi pato la taifa kwa Yeltsin ingekuaje?

Sasa ukisema wanataka nini Ukraine, rejea kwenye hii Video Chini na ile uliyoisikliza jana. Shida yao ni Putin, na walikua wakiamini kumpelekea chokochoko kupigana na jirani yake.
View attachment 2256161
Vikwazo watakavyoweka kuushambulia uchumi wa Russia utapelekea machafuko ya ndani ambayo yatamgeukia Rais wao na kutaka kumuondoa. Na hii Putin na Lavrov wameizungumza mara kwa mara wakidai kua Western kwa hilo wamefail kinyume chacke Sanctions zina wa backfires.


UN kwangu ni Umoja wa mchongo na upo kutimiza matakwa ya US... Wanyoosha vidole kote ila sio hapo walipoweka makao makuu yao.

Hawa niliwatupa kapuni nilipowasikia wanamkoromea Eritrea kua na hii Citizenship tax system wakidai ni ya kinyonyaji while US naye anayo na hanyooshewi kidole. Ten bora Eritrea wana flat tax rate ya 2% kwa walio nje ya nchi yao kuliko US anayetembea na avarage ya 23%.


Faida kwa Marekani wa kawaida haipo. Ipo kwa wale unaowasema. Wale wa nyuma ya pazia. Walio tingwa hegemony na uchu wa kuitawala dunia.

Hapo US, wagombea wengine are elected directly by popular vote. Lakini president and vice president are not elected directly by citizens. Badala ake, they're chosen by “electors” through a process called the Electoral College.

Wananchi ndio wapige kura ya kuchagua Electors, kisha Electors waende wakafanye yao. That's fate ya Rais iko kwa 538 electors. Ikishindikana kwao kwa House of Representatives na Vice Prezda kwa House Senate. That's ni kama kusema US citizens hawachagui Raisi wao bali wanachaguliwa.

UK hali ni ile ile. Hawa nao wanachagua wabunge tu. Wawakilishi wa majimbo. Ila waziri mkuu ambae ndie mkuu wa serikali anateuliwa na Malkia. Hadi hapa kwa wengine watakuwa wamepata majibu kwanini approval rate ya viongozi hawa ukienda kwa wananchi wa kawaida inasoma number ya kiatu cha mtoto.

Canada nako mfumo ni ule ule, wanachagua wawakilishi tu ila waziri mkuu, Yule mkuu wa serikali anachaguliwa na kikundi cha wachache wanaojiita wawakilishi. Hii mifumo imekaa kimchongo sana na ni easy kui-munipulate kwa kuweka viongozi wanaomataka.

Sawa na Bongo tuishie kuchagua wabunge tu halafu hao wabunge ndio wakatuchagulie kiongozi wa nchi... Yes hiyo nayo ni Democracy [emoji45]

Nyongeza: Asilimia 90.3% ya Ardhi ya Canada ni mali ya Queen Elizabeth II, 9.7% ndio ipo Privately owned. Maana ake kua katika watu Mil 38 waliopo Canada wamepanga kwenye ardhi ya Malkia Elizabeth. Haishtui akili hii?

Tutasemaje sasa Raia wa kawaida ananufaika na hiyo migogoro wanayoitengeneza nje.
 
Utawafanya CHADEMA na ACT waukimbie huu uzi.
Demokrasia imara au ufisadi imara na unyonyaji? Awamu iliopita ilikuwa na uafadhali kwa asilimia 90% ukilinganisha na hii ya Oligarchs toka Msoga na cartels zao.
 
Chanzo cha hii taarifa ya Yericko Nyerere kuhusu Nicaragua, nyuklia za Urusi nchini humo na Rais wake muuza dawa za kulevya ni kipi?
Moscow imesimika manowari yenye makombora ya Nyuklia (Balistic Missiles) huko Nicaragua nchi iliyoko America Kusini upavuni kabisa mwa Marekani, Rais wa Nicaragua, Daniel Ortega, aliruhusu kuingia kwa wanajeshi wa Urusi, meli na ndege nchini kwa madhumuni ya kibinadamu kutoka nusu ya pili ya 2022. Marekani kwa muda wote iliamini ni misheni zote ni kwa shughuli za kibinadamu, Nyambizi kubwa kabisa za makombora ya Nyuklia bzimesimika nanga katika nchi hiyo na sasa ni kitisho kikuu kwa Washington.

Katiba ya Nicaragua inaruhusu uwepo wa vikosi vya kigeni nchini na shughuli zake zote zitakuwa halali. Amri inayolingana ya rais Ortega inafanywa mara kwa mara. Wadadisi wa Ujasusi wanaashiria kuwa kupungua kwa msukumo wa Washington katika mgogoro wa Kyiv ambapo ahadi zimekuwa zikisuasua tofauti na miezi mwili nyuma ambapo Washington ilijaza shehena ya sila kila jua lichomokapo, Basi ni kiashiria cha uzito wa kitisho hiki kipya miguuni mwa Washington.

Kusuasua kwa Marekani na Ulaya kupeleka silaha za kisasa ukiachilia mbali silaha dhaifu za kizamani zilizokwisha muda wake na zinazolalamikiwa na makuruta kwamba hazina uthabiti wa kupambana na zile za Moscow, kumeifanya Moscow kutimiza misheni yake kwa haraka zaidi, ambapo hadi leo imefika 97% ya kazi ya ulombozi. Awali tathimini ilionyesha kwa mwendo wa Oparesheni na hatua za kimafanikio kwa Moscow, ingefika August na kutamatisha kwa usahihi oparesheni yake, lakini siku tano za nyuma kuanzia leo, Moscow imepiga hatua kubwa ikiteka maeneo makubwa na kukamata makuruta zaidi ya 6000 hali inayopunguza zaidi muda wa ushindi na pengine kutangazwa siku 14 tu zijazo.


(Yericko Nyerere)
 
Nchi zilizukwa zinaunda USSR zitajiangamiza zenyewe kabla ya kurudi au kurudishwa na Russia katika iliyokuwa jehanamu ya mateso ya USSR.
Unaishwawishije Ujerumani Mashariki au Poland kurejea zama za USSR??
Urrraaaa.
Wanangu Pro Russia Mim nina jambo natak kufhamu baada ya kukamilisha hako ka mkia kaliko baki hapo Ukraine. je tunaimeza Ukraine na kuwa ndani ya mipaka ya russia au Tunafanya michakato ya kuirudisha ile United Socialist Soviet Republic USSR
 
Anao pia mpango wa kuwaachia Bobi Wine na Kizza Bisigye wafanye kampeni bila kuwafungia majumbani mwao?

Anao pia mpango wa kuweka tume huru ya uchaguzi?
Hapo kwny mifumo ya kuchagua viongozi M7 nae ana Mpango kwny uchaguzi ujao wabunge (wawakilishi) ndio watachagua Rais, wananchi hawatapiga kura kuchagua rais.Kumbe Basi M7 amewaiga wale waanzilishi wa demokrasia [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Mambo si mambo [emoji23][emoji23]. Ooh EU wanaachana na Oil na gas ya Russia. View attachment 2256538

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wasingeweza kuishi bila Russia na hawawezi,or else Europe as we know it will be no more.
 
Hollywood haiko centralised, kuna studio kubwa zaidi ya 10 tofauti ambazo kila moja inazalisha kwa soko na maudhi yake, tena zinashindana.

Hakuna chama cha filamu kule kama cha kina Wema sepetu na Steve Nyerere hapa bongo.
Umeitazama kwa upande wa kuongozwa na market forces, okay....... je umeitazama pia upande wa yenyewe kuwa ni force to the market, marketting something influencing the 'masses markets'

Ipo pande zote
 
Ukiwa kwa Putin ukizoda au ukikosea uvamizi wake unaenda jela au unapotea kabisa.
Raha sana mwamba... Hii ya ndani tutaanza kupekuliwa IP address kutafutiana sababu za kupotezana kusiko julikana.

Hizo za nje unazodoa tu na kuzungumza utakalo.
 
Wakina nyambizinyo na huyu dogo aliyeingia zam sasa ***** mistress.

Hivi Pro-Russia kuna pattern hapa mnaielewa kweli? Namna pro-Nato wanavyopokezana zamu kushiriki kwenye huu uzi?

Anasumbua huyu, akichoka anaingia mwingine, then mwingine tena na tena. Zam ya Mwanamkiwi itajirudia lini [emoji23] nimemiss fujo zako.

Utasikia "mpendwa unajua....."
hamna kitu hapo ni jitu moja linabadili id tu. Ingekuwa ni watu tofauti mda mwingine wangekuwa online pamoja. Akili zao Kama za kondoo tu
 
Mkuu mi nafikiri ni aibu tu ya NATO, lakini njia pekee ya kumaliza vita hivi ni diplomasia na Ukraine kukubali vigezo na masharti ambayo naamini kwa ungwana wa Russia yatakua ni very friendly na integrity kwa Ukraine na Russia just kwa ajiri ya usalama wa Nchi zao wote leo, kesho na siku zote zidi ya malengo ovu ya mda mrefu ya USA yaliyofichwa kwenye propaganda za Democracy na Human rights
Mwanangu sote warusi ila rangi ya mwandiko inaumiza macho kausha kwanza
 
Back
Top Bottom