Mr Tyang
JF-Expert Member
- Sep 30, 2018
- 1,727
- 6,807
Wahenga hii tunaisoma hivi; "Mahakama ya ugiriki imetoa amri ya kuiachia mara moja meli ya irani iliyokamwatwa na ugiriki chini ya maelekezo ya USA"The Greek court has ordered that the Iranian oil tanker seized in instruction by the US be released.
Iran seized two Greek tankers in retaliation. They will have to ask nicely for their release.
"Na serikali ya ugiriki itabidi iombe radhi meli zake mbili zilizoshikiliwa na Irani ziachiwe" Mahama Ugiriki.
Funzo; Maamuzi hayo yamefichua Uonevu na uovu wa USA kwa nchi zingine kupitia mgongo wa nchi washirika wake.
Naomba niunganishe na dot, kwa alichokisema mzee wa akili nyingi Mh.Rais V. Putin juzi kama siyo jana (nitatumia lugha yetu)
"Kuna aina mbili za taifa, taifa lililo huru na taifa linalo tawaliwa.Taifa huru hufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na taifa lingine, ukiona taifa haliwezi kufanya maamuzi yake lenyewe basi jua hilo taifa ni koloni(taifa linalotawaliwa na taifa/mataifa mengine)" V. Putin.
Funzo kutoka kwa Putin; katika hii dunia kuna mataifa huru machache sana, mataifa mengi yanafanya uamuzi kwa kufuata shinikizo au matakwa ya mataifa yenye nguvu. mfano ni hayo maamuzi ya UGIRIKI juu ya kukamata meli ya Irani chini ya maelekezo ya USA. Kwa mjibu wa Putin(na ndo uhalisia) mataifa mithili ya Ugiriki siyo mataifa huru bali ni Makoloni.
OMBI: naomba Russia iendeleze operation yake na iendelee kushinda kila aina ya jaribio linalofanywa na hao mabeberu wanao tamani waendeleze uviranja wa dunia, hii itasaidia pia nchi nyingi kuamuka na kuondokana na hii dhana ya ukoloni mamboleo. tuna hitaji dunia iliyo na balance of power, tunahitaji mataifa yajiendeshe na kufanya maamuzi yake yenyewe bila kuingiliwa na taifa au mataifa mengine. Hiyo ndo dunia itakayokuwa salama leo, kesho na hata milele.
Mungu ibariki Urusi na operation yake dhidi ya hayo manyambisi ya dunia.