Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Wabongo bwana... mgogoro wa Urusi na Ukraine unatuhusu nini sisi? Sisi tuhangaike na mgogoro wa serikali na wamasai Ngorongoro; na mgogoro wa M23 Kongo.
Mgogoro wa serikali na wamasai unakuhusu nini wewe, waachie wamasai na viongozi wa serikali yako uliyo wachagua.
Sasa wote tukianza kushughulika na mgogoro huo, kazi ya viongozi tulio wachagua kufanya kazi zetu itakuwa ipi sasa,

Unacholazimisha tufanye nisawa na mtu amuajiri mtu wa kuchunga ng'ombe halafu bado aendelee kuchunga yeye huku akiendelea kumlipa mchunga ng'ombe huyo alie muajiri.

Kwahiyo mkuu Mwanafalsafa suala la wamasai lisikupe tabu kabisa. tumewaachia vibarua wetu kina mama samia, Waziri mkuu na mawaziri husika, DC, RC, watendaji wa kata na vijiji ambao tunawalipa kila mwezi kwa pesa za jasho letu, sisi tunasubiri matokeo tu, yakiwa yakipuuzi tutawachinja kwa vichinjio vyetu 2025.

Hivyo basi Acha tuendelee tu kudeal na hii operation kwa masilahi ya dunia na taifa letu pia, tunahitaji dunia yenye mataifa yanayojiamulia maamuzi yake menyewe pasipo kuathili taifa/mataifa mengine. nawenye uwezo wa kuleta hiyo balance of power kwasasa ni Russia na China tu (through millitary and economic power respectively) ndo maana unaona Tunasimama na Russia.

Nadhani nitakuwa nimeeleweka kwako na wenzio ambao bado hamuelewi kwanini tunasimama na Russia katika operation hii.
 
1.Weka ya hiyo treaty ya ya NATO kutosogea hata nchi moja kuelekea east, sema ilisainiwa lini wapi na viongozi gani wa NATO na USSR walisaini.

2.Rais wa Marekani hachaguliw na electors, anatokana na electoral votes college votes za majimbo . Electoral college votes zinatokana na popular votes. Kama Rais ameshinda jimbo anapewa Electoral votes za hilo jimbo, hakuna namna Electoral votes za mshindi wa jimbo zitaenda kwa mtu aliyeshindwa popular votes katika hilo jimbo, na hii iliwekwa hivyo makusudi na waandishi wa katiba ya US ili kuyapa sauti majimbo ambayo yalijiona ni madogo.

3.Ni Upumbavu kusema waziri mkuu wa Uingereza anachaguliwa na Malkia wakati kila mtu huwa anashuhudia uchaguzi mkuu wa Uingereza ukifanyika mara kwa mara na mawawziri wakuu wakiondolewa kuwa kura za kutokuwa na imani nao au kupoteza kwenye uchaguzi.

4.Uingereza, Canada, Japan, Israel, Ujerumani na nchi nyingine nyingi zina mfumo wa DEMOKRASIA wa waziri mkuu, kansela au kiongozi mkuu wa nchi kutoka katika chama kinachoshinda kwa kura nyingi au chama chenye kura nyingi kwenye uchaguzi kinachoweza kutengeneza coalition ya kuongiza nchi. Sijui kwa nini mfumo huh wewe unauona sio demokrasia! Sioni point wala mashiko kwa criticism yako, nafikiri ni uelewa wako finyu tu wa demokrasia ya uwakilishi.

5.Ni UONGO mtupu kwamba asilimia 90 ya ardhi ya Canada inamilikiwa na malkia. Huwezi kuthibitisha huu uongo wako kwa namna yoyote ile.
 
Utawafanya CHADEMA na ACT waukimbie huu uzi.
Demokrasia imara au ufisadi imara na unyonyaji? Awamu iliopita ilikuwa na uafadhali kwa asilimia 90% ukilinganisha na hii ya Oligarchs toka Msoga na cartels zao.
 
Chanzo cha hii taarifa ya Yericko Nyerere kuhusu Nicaragua, nyuklia za Urusi nchini humo na Rais wake muuza dawa za kulevya ni kipi?
 
Nchi zilizukwa zinaunda USSR zitajiangamiza zenyewe kabla ya kurudi au kurudishwa na Russia katika iliyokuwa jehanamu ya mateso ya USSR.
Unaishwawishije Ujerumani Mashariki au Poland kurejea zama za USSR??
 
Anao pia mpango wa kuwaachia Bobi Wine na Kizza Bisigye wafanye kampeni bila kuwafungia majumbani mwao?

Anao pia mpango wa kuweka tume huru ya uchaguzi?
Hapo kwny mifumo ya kuchagua viongozi M7 nae ana Mpango kwny uchaguzi ujao wabunge (wawakilishi) ndio watachagua Rais, wananchi hawatapiga kura kuchagua rais.Kumbe Basi M7 amewaiga wale waanzilishi wa demokrasia [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Wasingeweza kuishi bila Russia na hawawezi,or else Europe as we know it will be no more.
 
Hollywood haiko centralised, kuna studio kubwa zaidi ya 10 tofauti ambazo kila moja inazalisha kwa soko na maudhi yake, tena zinashindana.

Hakuna chama cha filamu kule kama cha kina Wema sepetu na Steve Nyerere hapa bongo.
Umeitazama kwa upande wa kuongozwa na market forces, okay....... je umeitazama pia upande wa yenyewe kuwa ni force to the market, marketting something influencing the 'masses markets'

Ipo pande zote
 
Ukiwa kwa Putin ukizoda au ukikosea uvamizi wake unaenda jela au unapotea kabisa.
Raha sana mwamba... Hii ya ndani tutaanza kupekuliwa IP address kutafutiana sababu za kupotezana kusiko julikana.

Hizo za nje unazodoa tu na kuzungumza utakalo.
 
hamna kitu hapo ni jitu moja linabadili id tu. Ingekuwa ni watu tofauti mda mwingine wangekuwa online pamoja. Akili zao Kama za kondoo tu
 
Mwanangu sote warusi ila rangi ya mwandiko inaumiza macho kausha kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…