Mgogoro wa serikali na wamasai unakuhusu nini wewe, waachie wamasai na viongozi wa serikali yako uliyo wachagua.
Sasa wote tukianza kushughulika na mgogoro huo, kazi ya viongozi tulio wachagua kufanya kazi zetu itakuwa ipi sasa,
Unacholazimisha tufanye nisawa na mtu amuajiri mtu wa kuchunga ng'ombe halafu bado aendelee kuchunga yeye huku akiendelea kumlipa mchunga ng'ombe huyo alie muajiri.
Kwahiyo mkuu
Mwanafalsafa suala la wamasai lisikupe tabu kabisa. tumewaachia vibarua wetu kina mama samia, Waziri mkuu na mawaziri husika, DC, RC, watendaji wa kata na vijiji ambao tunawalipa kila mwezi kwa pesa za jasho letu, sisi tunasubiri matokeo tu, yakiwa yakipuuzi tutawachinja kwa vichinjio vyetu 2025.
Hivyo basi Acha tuendelee tu kudeal na hii operation kwa masilahi ya dunia na taifa letu pia, tunahitaji dunia yenye mataifa yanayojiamulia maamuzi yake menyewe pasipo kuathili taifa/mataifa mengine. nawenye uwezo wa kuleta hiyo balance of power kwasasa ni Russia na China tu (through millitary and economic power respectively) ndo maana unaona Tunasimama na Russia.
Nadhani nitakuwa nimeeleweka kwako na wenzio ambao bado hamuelewi kwanini tunasimama na Russia katika operation hii.