Well said mdau!
Naomba nikazie ule mfano niliosema nimeupenda. Nataka niushereheshe kwa manufaa ya Pro-Russia lakini sio hao Makima msemo wa flani hapa.
Katika maeneo uliyoyataja nitatumia ramani tuelekezane vizuri.
View attachment 2257108
Hayo maeneo niliyoyawekea "black mark" ni machache kieneo na kiidadi ukilinganisha na ukubwa wa TZ. Lakini katika hiyo mikoa 9 hapo Juu ndipo kuna 43.5% ya Pato la Taifa (GDP) la Tanzania.
Kwenye hiyo Mikoa, ie. Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Morogoro, Lindi na Ruvuma... Dar es Salaam peke ake inachangia 17% percent ya Total Tanzania GDP. Dar yenyewe kwenye ramani iko hivi.
View attachment 2257119
Again tuongezee Zanzibar (Uliyoitolea mfano kama Snake Island) Zanzibar inachangia 5 point kadhaa asilimia za Pato la Taifa. Ukiongeza kwenye hiyo mikoa 9 means eneo la pwani kwa pamoja linachangia around 49% of Tanzania's GDP. Lakini Zanzibar yenyewe ndio hii
View attachment 2257120
Hivi leo namna tunavojiendesha hilo eneo la ukanda wa pwani likikaliwa na asiye rafiki basi Tanzania ina Collapse. Source ya nishati, Viwanda, na vingine viiingi vipo upande huo.
Kilimo Morogoro, Itabaki mbeya tu nao ambao kulingana na Idadi ya watu wanategemea kuzalisha kuuza nje ya Mkoa. Consumers wengi wapo upande huo.
All big Companies Headquartered in Dar es Salaam. Finacial service Zote makao makuu yapo huko. Kiasi ukiivuruga Dar tu umeivuruga Tanzania. Gas inasafirishwa kutoka mtwara kuja dar kuzalisha umeme. Ubungo ile ikizimwa Tanzania tunaenda gizani.
Sasa Pro-NATO kama wanashindwa kung'amua Ukubwa wa Pua sio wingi wa kamasi, Ama Ukubwa wa kichwa sio wingi wa Maarifa mtawaeleza nini waelewe?
Naandika haya kunufaisha Pro-Russia wenzangu, naaamini mmejifunza kitu na mnaeza tumia the same principle kwenye maisha yenu ya kila siku.
Kua na Afya sio kwa kula kilo 2 za mchele kila siku bali kwa kuupatia mwili lishe bora in a desirable quantity!
Sasa ndio kama hii Map!
View attachment 2257143
Huezi kuhusudu misaada ya ARV na Ndom za bure plus Vyoo ukaielewa.