Mbona unakuja tena na ule uwongo kuhusu dhahabu ya Iraki? Hauna ukweli wowote. marekani walifanya mabaya mengi kule Iraki lakini hawakuiba dhahabu!
(Kinyume: jeshi lao lilikamata lori lenye dhahabu, watumishi wa Saddam walijaribu kuiba. MArekani walifanya utafiti na kurudisha yote Baghdad)
Alicholeta
FUSO ni sahihi kabisa, tena huyu anaelewa kanuni za vita kushinda wewe. Kuiba ni marufuku, kuna mikataba ya kimataifa kibao. Inaonekana wewe bado uko zama za mawe; ukimwita "mtoto" unaonyesha tu elimu yako.
Nchi za dunia zimekubali mikataba ya Hague tangu 1899. Hivyo ni marufuku kwa askari kuiba mali katika nchi nyingine (looting), ambayo ni
jinai. Kisheria tofauti ni amri ya mkuu wa jeshi anayeagiza kuchukua mali (requisitions). Hatua hii inahitaji tangazo rasmi halafu ni lazima kutoa risiti kwa vitu vinavyochululiwa, vinapaswa kufidiwa baadaye.
Tena kitu kingine ni fidia (reparations) zinazokubaliwa baada ya vita wakati wa mkataba wa amani .
Walichofanya Warusi Ukraine hadi sasa yote ni mwizi mtupu na hivyo jinai. Sheria iko wazi.
Wakifauli kuificha kama mfano wako waKongo hakuna anayeshtaki hivyo hakuna kesi. Lakini sheria iko wazi. Mahakama ya Kimataifa ya Haki ilihukumu Uganda ilipe $ milioni 325 kwa DRC kama fidia ya wizi wakati wa vita.
Achana na mawazo yako ya kishamba, Bwana, nyakati zinabadilika.