Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Zile S-400 hazikuwekwa hapo kisiwani ?
Sometime Ukraine ielewe. Pale kisiwano Warusi wamejiondoa halafu kijinga ukraine wakajakama vile wamewashinda, wasijiulize why hawa wanajiondoa? Matoke mvua ya phosphorus imenyesha wanalalmika anatumia mabomu yasiyofaa. Yaani Urusi atawamaluza tekiniki zake za kuji withdraw mnakuja kujaa anawaua halafu anaendelea

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Maeneo ambayo Urusi inataka kuyachukua ni haya ambayo yamekaliwa na warusi



20220702_231544.jpg
 
Jedwali (Nina imani unamaanisha la kule Wikipedia) lipo wazi. Karibu Kila idadi ya ndege iliyotajwa imewekewa chanzo cha habari hiyo, kwenye jedwali sijaona chanzo kinachoeleza kuwa Kuna ndege zimetoka Bulgaria na kufika Ukraine April. Kwanza kwa ndege zilizotoka nchi za Ulaya kwenye jedwali hilo, sehemu ya remarks wamesema "the undisclosed countries" kuonyesha hawataki kusema Silaha hizo zimetoka wapi.

Hii nimekujibu kabla ya kuingia kwenye makabrasha yangu...maana napenda kuweka ushahidi mara nyingi.
Mkuu nilikuomba kusoma kwa umakinifu. Jinsi unavyosema, jedwali katika makala ya wikipedia lipo wazi. Makala hii ni mfano mzuri maana inaonyesha vyanzo vyake (si vile kote wikipedia, mara nyingi hapa JF haiko kabisa).
Ukiangalia tanbiki na. 58, unapelekwa kwenye chanzo kwenye tovuti ya Oryx. Hapo utasoma "Aircraft
23px-Flag_of_Bulgaria.svg.png
14 Su-25s [April 2022] (Officially delivered to NATO countries for political reasons)". Natumaini kwamba utatambua ishara ya bendera.
 
They should go to the streets.Kiongozi asiyefaa anaweza kuondolewa by Peoples' Power,ni ujinga tu uliokithiri.So wasubiri wafe!!!!!!????
Mkuu, kwa bahati mbaya hueleweki. Nani aende barabarani kwa kusudi gani?

Nilieleza hapo juu ni dhahiri viongozi wa EU wanafuata matakwa ya idadi kubwa ya wananchi wao. Katika mfumo wao wa kisiasa wanategemea kura ya wananchi wao si rahisi kwenda kinyume kabisa.

Inaonekana mashambulio ya Urusi dhidi ya Ukraine yamesababisha hofu na hasira kati ya mataifa ya Ulaya na kuwahamasisha washikamane zaidi, pamoja na kusaidia Ukraine.

Hapo naona viongozi wanafuata, ambayo inaeleza mabadiliko ya ghafla katika mwelekeo wa viongozi wa nchi kama Uswidi, Finland na Ujerumani.
 
Donbass yote imechukuluwa,lysichak has fallen too



Hapana si vile. Kwanza ujifunze kuandika majina ya Kirusi na Kiukraine. Mji unaitwa Lysichansk
pili haikuanguka (wala kutekeleza wala kuruka wala kulala).
Lysichansk bado inatetewa na jeshi la Ukraine. Ingawa kwa matatizo, hatujui watafaulu kutetea kwa muda gani.
Usichafushe jukwaa hii na propaganda ya Kadyrov.
 
Sababu ni moja tu; kata(style za Ngumi) zote anazotumia Master(NATO) wa Ukraine zinapelea mbali dhidi ya Kata za Master Putin(Urusi).

Nisawa uwe mwanafunzi mwenye green belt (Ukraine) ufundishwe na Master mwenye level ya Brown Belt (NATO) harafu utumie hizo mbinu na style za Brown belt kupigana na master wa Black belt (Urusi) Unadhani kipi kitatokea tofauti na kuvunjwa bandama mapema kabisa mwa mchezo.

Wazee wa kung-fu naamini wamenielewa vizuri, Mliobaki naomba mfano hai wetu uhamie kwenye mambo ya kijeshi.

Ni hivi kijeshi Russia yupo juu zaidi ya NATO hapa nikimanisha Mafunzo na mbinu za kijeshi, teknolojia ya kijeshi, na uwezo wa vifaa vya kijeshi kama silaha, mabomu na n.k, hivo basi kama Urusi ipo juu ya NATO kwa vitu tajwa hapo, nidhahili kuwa Ukraine hata angepewa mafunzo ya NATO na silaha zake kwa miaka 20 iliyopita bado tu asingeweza kuwa na uwezo wa kubattle na Russia ambae kiuwezo yupo juu ya mwalimu wake (NATO) na ndo maana unaona jeshi la Ukraine kiuwezo linaonekana kama jeshi la mgambo dhidi ya jeshi la Urusi licha ya kufundishwa na NATO toka mwaka 2014.

References
SYRIA [emoji1238]
VENEZUELA [emoji1263]
UKRAINE [emoji1255]

Kote huko NATO ilipelea/imepelea juu ya nguvu ya kijeshi ya Urusi[emoji635][emoji635]
Umeanza na mifano ya dojo na kumaliza mbinu za kimedani.
Aisee wewe lazima utakua special force TU.
💪😁👏👏👏
 
Back
Top Bottom