Hapa kwetu Tanzania walio wengi wananunua Umeme katika rate ya 26kwh kwa Tsh 10k. Hii bei nikiwa wrong mta-nisahihisha japo kwa Meter nayotumia nagharamika kama hivyo.
Maana ake ni kua kwa bei yetu ya 10k kwa 26kwh (kilo watts hour) itanigharimu kama Tsh 385k ili nipate umeme wa 1,000kwh ambayo ndio 1 Mega-Watt Hour.
Kama wao wanalipia 790Euro per MWH Sie hapa tunalipia 155Euro per MWH (nifahamike kua nime-convert 385,000 Tsh to Euro). Fedha zote hizo ukiziweka kwenye pesa ya Tanzania. Ni kua kwa the same amount of electricity, that's 1Mega-watt Hour. Sisi tunalipia Tsh 385,000/- wao wanalipia Tsh 1,960,000/-. Hii ni mara 5 zaidi kiliko sisi.
Nimeamua kuisherehesha hii post kwa kusudi moja tu. Kuna dhana potofu watu weusi tuko nayo, most of us utasikia tunasema ooh Europe wanalipa mishahara mikubwa n.k. lakini hatuangalii expense kulinganisha na mishahara yao.
Tunashangaa sana number, nimeona
Mr Tyang na
Galip Vrl wamezungumzia kuhusu analysis. Hapa pia huwa kuna tatizo. Europe mtu anaweza kulipwa Euro 1,500 per month, hii ipo around 4Millions za kibongo. Zinaonekana nyingi on Paper ila ukizipeleka kwenye matumizi ni chache mno kwa mazingira yale.
Huezi kupanga chumba cha Tsh 40k, ambazo ni Euro 16 kule kwao. But nje ya Dar kwa hapa Tanzania, Tsh 40k unapata chumba safi mno.
Hii issue ni pana kwani hata concept ya GDP unaweza kuijumuisha pia.
Mfano,
Mimi leo nikilima shamba, kila chakula nikawa najitegemea. Mahindi nalima, Mpunga nalima, Mchicha nalima, Almost kila kitu nakifanya mwenyewe.
Hapa nitanufaika lakini Hizi shughuli zote hazitakuwa reflected kwenye pato la taifa since hakutakuwa na Movement of "Cash" wala Shughuli kutoka kwa kundi moja kwenda kundi lingine.
Mfano wa kwanza huo, wa pili. Imagine katika mazingira kama haya. Mchicha nanunua kwa John, Karanga kwa Ayubu, Mahindi kwa Mabula, Mchele kwa Mwamposa, Mafuta kwa Mangi, Ndizi kwa Rutashobya. Hapa kunakuwa na Movement kubwa ya Cash, kunakuwa na shughuli nyingi. Hizi zote zinakuwa reflected kwenye hii kitu tunaita GDP. Pato la Taifa. So GDP inapea.
Hii mifano miwili sikidhamiria kuileta kwenye reply ya kaka mkubwa hapa. Imenibidi niitoe kwani yafanana na kile nilichokua nataka kukisema kupitia reply yake.
Mifano hiyo miwili inaweza kuwapa majibu katika nyanja hizi.
🔸Kwanini Nchi kama Russia, Kwanini Nchi kama Singapore au South Korea.
🔸Kwanini Mkoa kama Dar es Salaam, na Kwanini Mkoa kama Mbeya, Ruvuma n.k
🔸Of course itawapa majibu kwanini tulisema yule anayejiita Yoda tulimwambia hajui kitu upande huu alipokuwa analinganisha Pato la Taifa GDP na Thamani ya Kampuni Sokoni (Market Cap.)
Dar, kitunguu unanua, Mchicha unanunua, Muhogo wa kutafuna unanunua, Maji Visima hakuna mnanunua kwa kifupi Most katika vitu unahitaji ni kazi za watu. So mzunguko wa fedha na wingi wa shughuli ambazo ndio Uchumi wenyewe ni mkubwa, So there we go, unaambiwa kua Dar ina 17% of Tanzania GDP.
Mind you Uchumi sio Pesa, Uchumi ni shughuli za kibinadam ambazo of course ni issue zinazohusiana na fedha. Lakini Uchumi kama Uchumi sio how much you have bank au mfukoni.
Again ukichimba deep, utakuta all these stuffs zina mahusiano kiasi na flan na Culture, I mean life style ya watu. Anyway tuishie hapa nisije kuwachosha bure issues zenyewe ziko out of topic.