Mr Tyang
JF-Expert Member
- Sep 30, 2018
- 1,727
- 6,807
Mkuu ni mashujaa ndiyo na watakumbukwa kwa harakati zao za kupambania uhuru wa mwafrika, lakini hiyo pia haitubani sisi kujadili kiundani baadhi ya mbinu za kijinga walizo kuwa wanatumia kupigana Vita.Hizo ni motisha/morali ili watu wasikimbie waendelee kupambana ukizingatia tulitumia mishale,mawe,mkuki na simple tools zingine vs magobore.
Mbona hata huko Ukraine wanatumia simple tools vs heavy tools za kirashia ila wanapambana kutetea taifa lao.
Tuwape heshima mababu zetu walitupambania tofauti na sisi tunaona /tunajua ila ni ma keyboard warriors.
Narudia tena wale ni mashujaa kwa kipindi chao mpaka sasa hakuna mwenye uthubutu waliokua nao.
Mfano moja wapo wa mbinu za kijinga ni hiyo ya Mwamba Kinjekitile yakuwambia wapiganaji risasi ikipigwa watamke maji itayeyuka nakuwa maji. HIYO ILIKUWA NI MBINU YA KIJINGA KABISA iliyopelekea wapiganaji wetu wapatao 90,000 kumalizwa ndani ya muda mfupi (2yrs) na jeshi la Wajerumani lenye wapiganaji almost 2000tu.
Na miongoni mwa Vita iliyokuwa rahisi kabisa kwa wajerumani basi ni hiyo ya majimaji war (1905-1907), kwasababu ya hiyo mbinu ya kijinga kabisa ya maji dhidi ya risasi. Na inasemekana ni wajeruman wasiozidi 20 ndo walikufa kwenye hiyo vita.
Mjeruman mwaka 1891 alikutana na moto wa wahehe mpaka maji akayaita "mmaa" kipigo kilichopelekea Ushindi wa wahehe mnamo 17/08/1891 na kuendelea kudhibiti uvamizi wa mjerumani kwa muda wa miaka saba 1898 pale Mkwawa (Shujaa wa Vita) alipo kufa kwa kujipiga risasi baada ya kuzingirwa na vikosi vya kijerumani. Kwa zama hizo naweza sema kuwa Mkwawa ndo alikuwa Putin wa kipindi hicho.
Maoni yangu; Kama mababu zetu wangetumia mbinu dhabiti kama za wahehe chini ya mkwawa (the hero) kupambana na wakoloni basi Tanganyika tungepata uhuru wetu mapema sana, ila hizo mbinu za MAJI kupambana na Risasi pengine ndo zilituchelewesha kufika hapa tulipo na hizo ndo miongoni mwa historia zinazodhihilisha Ujinga walio kuwa nao mababu zetu.
Tukirudi kwa hiki kizazi chetu hasa Tanzania; Sisi hatuna ujinga kama mababu zetu ila tuna uwoga wa kijinga na kipumbavu sana kuwahi kutokea kwenye ardhi ya Tanzania, laiti mababu zetu wangekuwa waoga kama sisi basi mpaka leo tungekuwa chini ya wakoloni, Taifa limejaa wanaume waoga, wanawake wambea, Vijana wa Hovyo, Wasomi wa hovyo, viongozi wa hovyo na waoga. Leo hii watu hata kusimama kudai Katiba mpya tunaogopa tena kwa viongoz tulio waweka sisi madarakani, je tungeweza kudai uhuru mbele ya mabeberu ya kijerumani kweli?
#Ok Heshima kwao wote mababu zetu walio tupigania enzi za ukoloni na roho zao ziendelee kupumzika mahali pema Peponi.