Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Nimeuliza swali very specific. Kama huna jibu, sema sina jibu na acha kuleta flip-flop.

Naona now unaleta ishu mpya ya "Dunia ya Sasa..." Kwa hiyo kama Somalia Kuna njaa na Tanzania kuna njaa pia..?
tatizo una mind set ya,

YES OR NO,
BAD OR GOOD,
TALL OR SHORT

Mambo hayako namna hiyo.

Hili ni tatizo la afya ya akili.
 
Wewe nani kakwambia kwamba Russia ndio muuzaji pekee wa gesi duniani kwamba akigoma ndio nishati ya gesi ife? Na nani kakwambia kwamba dunia nzima haikuwa inawaza kuna siku Russia inaweza tumia gesi kama silaha, Poland na Bulgaria zimezimiwa gesi tangu April mwezi huu kwamba tangu hapo mpaka sasa hawana gesi? Finland imekatiwa gesi mwezi May, wamekufa kisa hawana gesi ya Russia?

Maisha baada ya vita ndio hayo, Russia atafute wa kumuuzia hiyo 40% ya gesi. Na atafute wa kumuuzia silaha zake, Su-35 alizotakiwa kuuza kwa Egypt ikazikataa kwa makosa ya kiufundi inasemekana zitauzwa kwa Iran. Kama soko la gesi sio muhimu basi Russia asingejenga Nord Stream 1, akajenga na 2. Hiyo gesi huwa anatoa bure? Ulaya ilikuwa inalipa zaidi ya dola bilioni moja kwa siku kununua gesi
 
Naomba nitie neno
Jamaa kamaanisha kwamba EU itakua muflis kiasi kwamba haitaweza kumudu gharama za bidhaa tokea US maana zitakua bei juu ukilinganisha na zitakazotoka UCHINA
Na bei itachagizwa na GAS kwamaana uendeshaji wa viwanda utakua juu kwa US gharama kubwa lakini UCHINA gharama itakua chini
Mfano:-Iphone inayotoka us itakua 300sh halaf inayotoka UCHINA iwe 50 zenye ubora na viwango sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nazungumzia existing technology "not under construction technology", hata sisi mbona kipanya anadevelop electric cars.
Ni kweli West wameendelea kwenye Teknolojia ya kuchimba mafuta na gesi. Bahati mbaya awali Russia aliwaamini zaidi West kwa kutegemea zaidi Teknolojia zao. Lakini, toka 2014, West walipombadilikia Russia, Russia naye alianza kuweka mikakati ya muda mfupi na mrefu kukabiliana na hivyo vikwazo vya West. Mikakati hiyo baadhi ni hiyo ambayo imeanza kuzaa Matunda mwaka huu kama article niliyokuelekeza.

Udhaifu huu wa kutegemea Teknolojia za West, Russia waliuustukia pale Crimea ilipojiunga Russia huku West wakiipiga Russia na Lundo la vi kwazo. Ushahidi wa maelezo haya unaweza kuupa kwenye makala hizi chini kama ukizisoma kwa jicho la Tatu.


 
M

Mgogoro wa Syria hauna uhusiano na Israel kama Iran asingeingia. Siku Iran anaondoka Syria na akaacha kupitisha silaha kwenda kwa Hezbollah ndio siku Israel itaacha kuhangaika na Syria
Kabla ya kilichosababisha machafuko SYRIA hao HIZBULLAH walikua wanapelekewa silaha na IRAN kupitia njia gani MKUU ambao waliweza kupigana vita na ISRAEL 2006
Kiufupi ISRAHELL anajipigia SYRIA tokea jamaa waanze kua na migogoro ndani kwao wala sio IRAN
Hapo jamaa waamue kupigana na ISRAHELL ama kupigana na wanaosumbua ndani
Kabla ya kilichotokea 2011 ISRAHELL asingweza kupambana na SYRIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiria yaani Ninadhani, sina hakika kabisa hii Siyo kweli. Kwa sababu Russia anaiweza hiyo kazi. Sema, EU na West kwa ujumla Wana sera fulani hivi ya anti-monopoly kwamba ili kuepusha entity moja kumiliki Kila kitu, wanakulazimisHa uingie mikataba ya namna hiyo kwamba sawa leta gesi lakini matengenezo wafanye wengine! Na mambo mengine kama hayo.
 
Anatumia akili
Ila ajitahid kuacha mahabba nilishangaa sana sasa kama hata la gas na bomba anatupiga chenga
Ila pengne alipitikiwa MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi nchi ni kama zimegeuka kua mikoa ya EU. Hazina maamuzi yao wao kama wao kwa Raia wao.
Ndio maana Uingereza iliomba kujitoa.

Kuwa chini ya Brussels ni kuhand over political power ya nchi.

Kuhand over matumaini na matarajio ya Taifa.

Hivyo ni kamtindo fulani ka kuburutwa unless uwe kama Victor Urban na Hungary yake.
 
Kweli kabisa propaganda za kitoto ni nyingi sana na kama ulivyosema kuna wachangiaji makini wameacha kuchangia huu uzi kwa kuwa kuna wapotoshaji wengi.uzi ulikuwa mzuri sana kuelemishana na kupeana fact za kinachoendelea kwenye hiyo vita.
 
Unajifanya unajua kuliko wataalamu wa Siraha wa Urusi, kisa hapo kihangaiko[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Niseme tu vita ina mkusanyiko wa matukio Mengi kama boxing MWISHO wa siku ni points na rounds zinahesabika
Hapa tunaanza kuona mara Syria mara Somalia hizo mambo zilipaswa kuletwa wakati Russia kaizingira Ukraine vita BADO. Sasa vita inapigwa tujikite kwenye ramani za vita maendeleo ya mstari wa mbele reinforcement , impact za sanctions nk
 
Hawana technolijia?

Au Kuna kitu kwenye learning rate kwamba unamwachia Fulani atengeneze kwa sababu ya efficiency na cost kuwa chini.

Urusi watatengeneza kila spare parts za hayo mabomba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…