Niliingia humu nikidhani watetezi wa dikteta Putin ni watu wanaofuatilia matukio kwa mapana yake, kumbe hawana hata tofauti na hawa vibozo wa kwetu ambao huvua bongo zao na kuziacha kabatini watu wanapokuwa kwenye mijadala mizito.
Kuna kitu kinaitwa kukurupuka na uzuri wa Marekani, taifa la wahamiaji, ni kwamba hawakurupuki hovyo hata pale papara zinapozidi. Watatoa onyo halafu watakaa kimya kama vile hawapo lakini ikifika siku ya siku hutajua umepigwa na nini kutoka wapi.
Juzi tu nimeaga ili mpate nafasi ya kutafakari kitu gani kilifuatia after the antelope danced herself lame before the main dance! Kwa mbali namkumbuka Sadam wa Iraq akibweka utadhani dunia nzima ingeungua moto kama wa kuthubutu angetokea!
Kama kawaida historia haina aibu; itajirudia na safari hii Sadam hayupo tena lakini yupo pacha wake, Vladimir Putin. Huko USA rafiki yake Putin, Donald Trump ana chezeshwa huku mizizi yote ikikatwa taratibu na mwisho wa siku ni anguko la kishindo, puuu!
Lakini Trump ni wa kwao, wanaweza kumsetiri kwa namna wanayoijua lakini huyu limbukeni ha ha haaa! Tusubiri yale yale yalompata Sadam Hussein aliyeapa kuligeuza jangwa la Iraq kuwa bahari la moto kuwateketeza hao big brother wa dunia!
Eti Russia ilimpiga Hitler single-handed! Kasomeni tena historia.