Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,890
- 26,440
Dmitr Medvedev ambae ni makamu mwenyekiti wa baraza la usalama la Russia ametoa mwelekeo kamili wa mashambulizi ya Russia dhidi ya Ukraine kwamba mengine yatafuata ili kuondoa kabisa serikali ya kinazi iliyopo mjini Kyiv.
Medvedev amesema hatari inoletwa na Ukraine ni dhahiri, iliyopo na iliyo wazi hivyio kuvunja kabisa utawala wa Kyiv ndio itakuwa suluhisho.
Wakati huohuo raisi wa Belarus Alexander Lukashenko amekubaliana na raisi Putin kuunda kikosi kazi ambacho kitakuwa na majukumu ya kulinda upande wa magharibi mwa nchi hiyo ambako yapakana na Poland na Lithuania.
Lukashenko amedai Ukraine ikishirikiana na Poland na Lithuania wapanga kuishambulia Belarus kutokea upande wa Magharibi.
Itakumbukwa mapema mwaka huu mwezi February Russia ilitumia ardhi ya Belarus kufanya mashambulizi dhidi ya Ukraine lakini Belarus haijashiriki moja kwa moja kwenye operesheni hiyo ya Russia.