Mkuu, natafuta matiki katika maelezo yako.
Yote ninayoona kuhusu utaratibu wa jeshi ni dalili ya uongozi mbaya ukishambulia bila kuandaa nguvu ya kutosha. Tumeona sote jinsi Urusi ilivyoshambulia Ukraine bila kujipanga ipasavyo, hapo sababu za kulazimishwa kukimbia Kyiv mwanzoni, baadaye kutoka jiji la Kharkiv, juzi katika Donbass.
Vilevile zoezi la mobilization ambako maandalizi yalikuwa hovyo.
Naomba sana tusiamini propaganda, wala ya Zelenski au ya Putin.
Naona kasoro hizo zilionekana kwa wote na hapo sababu ya kutoogopa jeshi la Putin tena. Finland waliogopa sana - tangu kuona udhaifu wa jeshi la Putin waliamua kujiunga na NATO, Sweden vivyo hivyo.

Baba jeshi la Urusi ni moja ya majeshi makali sana hata bila nyukilia.
Mnachokiona ukraine Iko hivi;
Urusi inapeleka askari Wachache sana mfano tufanye imepeleka askari 150000 wanapambana na askari wa nchi nzima ya Ukraine,Tena waliofunzwa na NATO kwa miaka zaidi ya minane.
Tufanye Ukraine Ina askari zaidi ya 300000 yaani ni marabili ya askari wa Urusi walioko kwenye op hii.
Ukraine ilikua na silaha nyingi sana za kwake na inazipewa na NATO.
Urusi ulikua inapigana kistaarabu na kiungwana sana yaani haikutumia uwezo wake wote.
Hadi Sasa hivi Ukraine haina silaha zake za zamani,zote zililiwa na Urusi.
Upinzani anaoupata Urusi ni Halili na WA kawaida kwa sababu Ukraine wanapigana wakiwa kwao kujihami na kile wao wanakiita uvamizi kwa hiyo wanapigana kufa na kupona.
Urusi wanafanya op maalum kuondoka kitisho Cha silaha na uwezekano wa kuja kuvamiwa baadae na NATO.hivyo spirit walionayo Ukraine sio walionayo Urusi.
Lkni ikatokea nchi yoyote kuivamia Urusi katika ardhi yake ndo utajua kama Urusi ni Urusi ama ni Urusi ya kinondoni Moscow.
Upinzani anaoutoa Ukraine kwa Urusi ni mkubwa kwa kweli kama nilivyosema ,wao wanapigania nchi yao.Lakini huo uwezo unaouona wa Ukraine ni uwezo wa NATO na nchi zote za west.
Tumeshuhudia michango ya silaha ya kujirudia,hizo silaha walizokua wakipewa mwanzo zinzenda wapi?zinaliwa na moto wa Urusi.
Ukraine wanapewa taarifa zote muhimu za kiintelijensia ya kijeshi na kiraia kutoka nchi zenye uwezo mkubwa mno katika nyanja hizo.
USA,UK,Fr, German,Poland,Canada,Estonia,Lithuania,Italy,Sweden,Denmark,Finland,Turkey,burgaria, Australia,Austria etc.
Taarifa za Kijasusi kijeshi ni muhimu mno,ndio zinaonesha adui Yuko wapi,ana silaha kiasi Gani,umballi Gani,idadi ya askari na hata ushauri I silaha Gani itumike kumpiga.
Ukraine inapewa vifaa vya mawasilia I na njia za kudukua mawasiliano.
Inapewa misaada ya fedha kula kukicha.
Kwa uchache ni hayo.
Sasa.
Hebu fikiria hayo yoote yanafanyika Urusi Iko peke yake inapigana vita peke yake.
Urusi Ina wanajeshi karibu 900,000.
Wengi hawajaingia vitani,wanasubiri kama vita itakua kubwa ama NATO wataingiza majeshi ndio na wao wataingiza.
Kumbuka kwa akili ndogo TU ya kawaida huwezi kupeleka askari wote hodari na muhimu katika vita,unaanza naseto kwanza ,mambo yakizidi kua magumu nawe unaongeza dozi.
Hapa Urusi hawezi kupeleka askari wake wote vitani wala silaha zake zote muhimu vitani kwa kuangalia NATO watafanya Nini.
Ikiwa NATO wataingiza Mazuma nae Urusi ataingiza mazima maana hatutegemei kua na vita zaidi ya NATO na Urusi.
Huwezi kuweka mayai yote mazuri kwenye kapu moja.
Urusi sio nchi nyepesi Braza.