Narumu yetu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 2,448
- 5,146
Mkuu ukiwa na idadi - utaje tu! Menginevyo sioni kosa kuangalia vyanzo yva silaha. Kwa Ukraine ni wazi: akiba zake zimepungua sasa, hasa kwa sababu sehemu ya viwanda vyake vimeharibika. Hivyo inapata grenedi na roketi nyingi kutoka nje.
Tukiona Urusi inachukua sasa grenedi kutoka Korea Kaskazini - basi ni dhahiri kuna tatizo. Ukiwa na akiba ya kutosha huhitaji kutumia pesa kununua nje. Pia grenedi na silaha zote za Korea Kaskazini zinajulikana kuna kiwango cha hitilafu (kumbuka taarifa nyingi kuhusu roketi zao zilizolipuka au kuanguka mapema...); kwa jumla si ajabu ukizingatia hali ya njaa katika nchi ile (isipokuwa kiongozi mnene akisimama bele ya majenerali wembamba sana...)
Putini achore mstari mwekundu tens,Ile imefutikaHuu mkeka wa hawa Majasusi Upo Mezani. Ndo maana jana Kremlin walisema wana ushahidi kuwa UK wapo deep in Ukraine.
Hii imevujishwa makusudi kuwapa alert MI5 wachange plan au kuwithdraw au litawakuta zito kupitia Air Strikes mahali walipo wakiamini pameshajulikana.
Wamechanganishwa hapo!
Putini kichaaaaKwahiyo urusi baada ya kuvamia nchi ya watu anataka Ukraine asijishughulishe kabisa kuilinda nchi yake???
Mkuu bila shaka ungeweza kufanya utafiti makini zaidi kuliko kile ulicholeta. Ona hapaRussia kununua silaha nje haionyeshi kwamba kuna tatizo, nikukumbushe US alienda kununua air defense system NASAMS kutoka Norway na kuzipeleka Ukraine. Kwa nini US anatengeneza PATRIOT na THAAD air defense system alafu hazipeleki Ukraine ila anaenda Norway kununua NASAMS ndio azipeleke Ukraine??
US kwenda kununua silaha nchi nyingine za kupeleka Ukraine wakati ana viwanda vyake vinatengeneza haimaamishi kwamba kwenye viwanda vyake vya kutengeneza air defense system kama MIM Patriot au THAAD kuna tatizo, wenye kujua mambo yao ya kivita watakua wanajua kwa nini anafanya hivyo.
Russia anatengeneza drones zake ila alienda Iran kuchukua shahed 136 drones, ulijiuliza pia ni kwa nini?
Na ni uongo kusema silaha zote za North Korea zinakua na hitilafu, ukifuatilia majaribio ya silaha ya North Korea mengi yanafanikiwa, zilizotesiwa juzi zote hakuna ripoti inayoonyesha zimefeli.
Hitilafu kwenye majaribio ya silaha ni kawaida sana hata US kafeli mara nyingi kwenye hypersonic missiles.View attachment 2408824View attachment 2408825View attachment 2408828
Halafu Mkuu, ukipenda kujielimisha kidogo: soma hii:Russia kununua silaha nje haionyeshi kwamba kuna tatizo, nikukumbushe US alienda kununua air defense system NASAMS kutoka Norway na kuzipeleka Ukraine. Kwa nini US anatengeneza PATRIOT na THAAD air defense system alafu hazipeleki Ukraine ila anaenda Norway kununua NASAMS ndio azipeleke Ukraine??
US kwenda kununua silaha nchi nyingine za kupeleka Ukraine wakati ana viwanda vyake vinatengeneza haimaamishi kwamba kwenye viwanda vyake vya kutengeneza air defense system kama MIM Patriot au THAAD kuna tatizo, wenye kujua mambo yao ya kivita watakua wanajua kwa nini anafanya hivyo.
Russia anatengeneza drones zake ila alienda Iran kuchukua shahed 136 drones, ulijiuliza pia ni kwa nini?
Na ni uongo kusema silaha zote za North Korea zinakua na hitilafu, ukifuatilia majaribio ya silaha ya North Korea mengi yanafanikiwa, zilizotesiwa juzi zote hakuna ripoti inayoonyesha zimefeli.
Hitilafu kwenye majaribio ya silaha ni kawaida sana hata US kafeli mara nyingi kwenye hypersonic missiles.View attachment 2408824View attachment 2408825View attachment 2408828
Mzee naelewa NASAMS ni project ya Kongsberg Defence & Aerospace (Norway) and Raytheon (USA)Mkuu bila shaka ungeweza kufanya utafiti makini zaidi kuliko kile ulicholeta. Ona hapa
"NASAMS: The weapon is manufactured as a joint venture between U.S.-based Raytheon Technologies and Norway’s Kongsberg Defence and Aerospace, though the principal contractor on the Kuwait sale is Raytheon. The United States itself uses NASAMS to protect the airspace over the White House and the Pentagon."
Pia habari ninazoona zinasema NASAMS zilizopelekwa Ukraine zilitoka Marekani ambako zilitengenezwa na Raytheon - Marekani.
Kwa hiyo sioni kwamba US walinunua silaha hizi kutoka Norwei.
Ushirikiano katika kubuni na kutengeneza silaha kati ya nchi mbalimbali si jambo jipya. NASAMS ilikuwa mfumo uliobuniwa Norwei na kampuni ya Marekani ilijiunga kwa sababu waliona ni bora, nadhani (sikuchungulia) kwamba Norwei ilikubali kwa sababu RAytheon ilileta pesa katika ushirikiano wao.
Naona tofauti na grenedi kutoka Korea Kaskazini. Korea inatengeneza grenedi zinazofaa kwa mizinga ya Urusi kwa sababu Korea ilifuata mfumo wa silaha za Umoja wa Kisovyeti.
Silaha hizo hazina tabia mpya, ni ile saizi ya 152 milimita iliyo kawaida Urusi na pia Ukraine (mizinga ya kale walioyorithi tangu siku za ukomunisti).
Kama Urusi inapaswa kuchukua grenedi kutoka huko (zinazojulikana kuwa na hitilafu) ni dalili dhahiri kwamba tasnia ya Urusi haiwezi kuendelea kutoa grenedi za kutosha kwa matumizi makubwa ya jeshi lake.
Hawapati silaha mpya, wanapata nakala (zenye ubora duni) za silaha zao wenyewe.
Ukiona sababu tofauti, tafadhali utueleze!
Asante mkuu, lakini chanzo changu kinasema mifumo miwili iliyopelekwa Ukraine ilitoka Marekani. Nadhani habari uliyonukuu haikufanyiwa utafiti makini. (Si vigumu kuona kwamba nchi yenye watu milioni 5 kama Norwei si rahisi kutengeneza bidhaa zozote kwa idadi kubwa tukiacha tasnia ya mafuta mbali)Mzee naelewa NASAMS ni project ya Kongsberg Defence & Aerospace (Norway) and Raytheon (USA)
Kwenye screenshot nikiyoweka nilihighlight sehemu ya Norwegian made-NASAMS makusudi ili upaone hapoView attachment 2408859View attachment 2408860
Juz MK254 kaasema umeme na maji vimerudi kiev[emoji1787]
Kwambaaaaa kutumia watu waliotoka gerezani ni sawa naaaaa!!!?? Unajisikiliza kweli ulichoandika!!?? Ukraine alipoachia wafungwa na kuwaingiza kwenye mapigano si mlipiga vigeregere na mbinja hapa!!?? Au ilikuwa bado unakula mihogo na matobolwa!!? Au haujui kwamba Zele hakufanya hilo!!??? Mtulie .....Mkuu, sina uhakika kuhusu akili ya bwana Muhozi.
Ila kutegemea watu kutoka gerezani vitani???
Sawa ukiwatumia kama lishe ya risasi (sijui tunayo canon fodder kwa Kiswahili?) utapata faida si wengi vile watakaopinga wakifa wengi.
Kwa upande mwingine, labda hao watu ni wabaya lakini si wajinga. Siyo wanaweza kutumia nafasi za kufurahia (kubaki, kupora, kuiba) lakini pia nafasi ya kutoroka? (mfano wakiona uwezekano wa kuishi ni mkubwa wakijisalimisha kuliko kuwa mashujaa???)
Kwa hiyo zile ndege na vifaru mnavyosifia kutungua waliviokota kama Tanzania ilivyookota vichwa vya treni bandarini!!!!? Your not that low bro.... Hayo Bora uwaachie kina KENTA Fuso huko.. BlessWarusi wanakufa wengi sababu Rais wao anaamini katika wingi, hajawapa vifaa zaidi ya Risasi
Si amepoteza ushawihishi huyu.... !!??
Si amepoteza ushawihishi huyu.... !!??
Source: Niamini Mimi HIMARS....Kuna mwanajeshi 1 wa Urusi kasema siku 3 zilizopita kwenye platoon yake waliuawa watu 500+ sababu hawakuwa na silaha.
Walipewa kazi ya kuchimba trenches ndipo mvua ya artillery toka Ukraine ikaanza wamiminikia.
Yeye na wenzake waliopona wakakimbia kurudi kwa aliyewatuma. Walipofika wakaomba kutopelekewa frontline. Wakapewa silaha wakarudishwa nyuma kidogo sababu hawakujisalimisha.
Walikaa siku 3 bila chakula wala msaada
Lazima wabondwa ipasavyo..,ni mwiko kuwapa pumziko wavamizi [emoji91][emoji1255][emoji123]Hali ni tete kwa Ukrusi
Wakati vikosi vya Urusi vinakimbia ,Majeshi ya Ukraine yanalipuwa msafara wa magari yao ya kivita[emoji848]
....
Hajui hata utofauti wa platoon na company.... Platoon wanajeshi 500+ ..... Aseeee hata company kufika 500+ ni mtihani mostly ni 200-300.Na nyinyi mnaona habari hizi niza kweli? Hata maelezo yenyewe ni highly flawed - mtu aliyewahi kupitia jeshini anajua platoon ina wanajeshi wangapi - eti Ukraine iliwapiga na mizinga kwenye matrech karibu wote wakafa lakini yeye kapona kimiujiza na kufanikiwa kuja kusimulia the tale the morning after - na stori anayo simulia inahusu wanajeshi wa Urusi wanavyo uwawa kama nzinge na wasivyo kuwa na ujasiri ni waoga, sijui kaja kupewa AK47 sijui na mfadhili gani mtoa stori hii anajifanya ni mwanajeshi wa Urusi, hii wapi na wapi.
Yaani stori nzima inaonekana wazi wazi kuwa imetungwa na vyombo vya propaganda vya Serikali/jeshi la Ukraine, lakini kwa bahati mbaya baadhi ya members wala hilo hawalioni kabisaa!!