Na kubwa kuliko ni kwamba Ukraine ikiingia mkataba uliokwenda Kwa jina la "mkataba wa Minsk" mkataba huo uliitaka Ukraine iache kuwaua/kuwatesa nk watu wa Donbass ila Ukraine haikutii huo mkataba ndipo kidume Vladimir Putin chuma Cha reli kikaingilia kati Kwa mambo mawili
1)Ukraine isijiunge na NATO
2)kuikombia Donbass na kuwa huru
Na kama hiyo haitoshi Bado Putin Yuko ndani ya reli ya Sheria za umoja wa mataifa, Sheria inasema kama Jimbo linataka lijitenge basi hakuna ulazima wa Jimbo hilo kuombw kibali kutoka makau makuu ya nchi
Ila Cha ajabu marekani na other westerners hawataki hilo, wanataka Donbass iendelee kuwa sehemu ya Ukraine alafu hapo hapo wanataka Taiwan ijitenge na china, wanataka Hong Kong ijitenge na china
Umeona walivyo ndumila kuwili?
Kuna wapuuzi huwa wanakuja na hoja wa mkataba wa Budapest bila kujua undani wa mkataba huo
Mkataba wa Budapest ulisainiwa mwaka 1994 chini ya marekani ukarine Russia na mataifa mengine kuwa urusi haitaivamia Ukraine, ila nyuma ya huo mkataba ni kwamba pindi Ukraine inataka kujitoa kutoka USSR ilipaswa I submit all nuclear warheads Kwa mrusi sababu ililazimika kusaini mkataba wa NPT wa mwaka 1968 Sasa Kwa hofu ya kwamba huenda likatokea la kutokea huko mbele ya safari ndipo ukraine ilipoomba mkataba wa kwamba haitavamiwa na ndo ulipokuja mkataba wa Budapest
Lakini mwaka 1997 Ukraine na urusi ziliingia mkataba kuwa ukarine haitajiunga na NATO
Sambamba na hilo pia mwaka 1990 urusi na NATO waliingia mkataba kuwa NATO hawatajipanua Kwa kuwapa uanachama mataifa ya ulaya mashariki nchi zilizopakana na urusi
Sasa twende tuangalie nani mkorofi
Mwaka 1999 NATO wakaisajili Poland mwaka 2004 NATO wakaisajili kina Lithuania na Latvia na baadae Estonia (hii ilikuwa ni kinyume kabisa na mkataba wa 1990 baina ya NATO na urusi)
Kuanzia miaka ya 2000 mwanzoni mwanzoni Ukraine ilianza ***** ***** za kutaka kujiunga na NATO (***** ***** za kutaka kukiuka mkataba wa 1997)
Mwaka 2008 Georgia ilitaka kujiunga na NATO Russia akaivamia akaipa kipigo kitakatifu ikatuli (hili lilikuwa ni somo Kwa Ukraine iachane na fukunguku za kutaka kujiunga na NATO ila haikutaka kusikia)
Mwaka 2010 mihemko ya Ukraine kutaka kujiunga na NATO ikazidi shamili kiasi Cha kutaka kuikaribisha marekani (NATO member) kuweka Kambi za kijeshi katika rasi ya Crimea(rasi ya urusi ambayo Ukraine walipewa mwaka 1954 bila mkataba)
Urusi ikaona kumbe hunijui Yani nakupa Simu Bure alafu wewe unataka kuwapa maadui zangu wamtongozee mke wangu
Mwaka 2014 urusi ikaamua kuinyakuwa Mali yake (ardhi ya Crimea)
Ukraine kuona hivyo ikajua Sasa huu ushakiwa msaala nikizubaa hapa huenda Kuna makubwa yatanikuta ni Bora nikimbilie polisi (kujiunga na NATO)
***** ***** za kujiunga na NATO zilipamba moto kuanzia mwaka 2019, Putin akaenda Vatican kuonana na papa na kumueleza kuhusu uchokozi wa mataifa ya magharibi namna yanavyotaka kuvunja mkatba wa 1990 na pia Ukraine inavyotaka kuvunja mkataba wa 1997
Papa akapuuzia
Mwaka 2022 mwanzoni ndo mihemko Kwa Ukraine ikapanda sana na kutaka kujiunga na NATO
Na mbaya zaidi NATO wakampa kichwa hakuna wa kukufanya chochote
Putin akatuma Wana diplomasia wake Brussels kujadiliana na NATO kuhusu hizo fukunguku kikao kilifanyika Kwa masaa manne bila kuzaa matunda
Ikabidi Putin amuandikie barua Biden kuhusu hiyo fukunyuku ya westerners kutaka kuisajili ukarine NATO
Ila Biden akaitupa barua kwenye dustbin na mbaya zaidi Hadi ka Estonia na kenyewe kakasikika kakisema "hayo madai ya urusi hayana nafsi na yanapaswa kupuuzwa"
Putin akasema kumbe hamnijui akapeleka mswaada bungeni wa kuivamia Ukraine na wabunge wote bila kujali tofauti zao wakapitisha Kwa sauti Moja tuivamie Ukraine
Ndipo Putin aliposukuma jeshi
Alafu Leo wanaanza kusema ooh Putin mkorofi, huyo papa anajidai eti kuumia sana Kwa mauaji yanayotokea Ukraine wakati alifatwa na Putin akapuuzia alitaka putin afanyaje?
Kwahiyo ukiiangalia kiundani utaona kuwa putina anaonekana kuvunja mkataba wa Budapest (kichaka ambacho wazee wa upinde [emoji304] wanakitumia kuilaumu urusi) ila wasijue aliyefanya mpaka urusi ivunje huo makataba ni hao hao Ukraine Kwa kutaka kuwakaribisha NATO wakae pale Ukraine, lakini pia hata hao NATO wamekuwa wakivunja mkataba wa mwaka 1990 Kwa kuwasajili kina Estonia, Lithuania Latvia na Poland
Sasa iweje NATO wakivunja mkataba iwe sawa lakini urusi ikitaja kuvunja mkataba iwe dhambi ?
Urusi imesukumwa kuivamia Ukraine ila haikuwa na hiyo Nia, wameichokoza wenyewe
Bibilia inasema aonywae mara nyingi akishupaza shingo yake itavunjika vipande vipande Wala hapati dawa na ndicho kinachompata Ukraine
C$P
Sent using
Jamii Forums mobile app