Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Viongozi wa Urusi hawalii-lii,ila they are warning the World.Maneno ya Putin ya hivi karibuni kabisa ni haya,very chilling indeed,"Those seeking to defeat Russia on the battlefield apparently do not realize that a modern war with Russia would be entirely different for them. We’re not sending our tanks to their borders. Yet we have something to respond with, and it would not be limited to armor use only, everyone must realize that."
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Yani anamaanisha mashoga mjiongeze silaha ni nyingi sana
 
Siku itafika hii vita itakwisha, Amani itarejea... Ardhi inawezekana isirudi tena Ukraine lakini itakapokwisha suala la kuimega Ukraine halitakuwa maamuzi rahisi tena kama ilivyokuwa SMO.
Kusema maamuzi ya SMO yalikuwa ni marahisi ni opinion yako tu na sio lazima iwe kweli! Pengine yalikuwa ni maamuzi magumu. Unajuaje kama yalikuwa marahisi!?

Unafikiri vita vikiisha atakayekuwa amepata funzo ni urusi na sio Ukraine!? Pengine tynafikiria kitu kimoja kutoka pande mbili tofauti.

Wakati wewe unafikiria Urusi atapata funzo kuhusu kuivamia tena Ukraine mimi nafikiri Ukraine ndio atakuwa amepata funzo kuhusu usalama wa Urusi.
 
Hali huko mbele inazidi kuwa ngumu, ni ngumu sana sasa huko Bakhmut, Vuhledar, Limansky na pande zingine, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema katika hotuba yake ya jioni ya kawaida.

"Wakati wa siku 346 za vita hivyo, mara nyingi nililazimika kusema kwamba hali ya mbele ni ngumu. Na kwamba hali inazidi kuwa ngumu. Sasa ni wakati tena. Wakati ambapo mtekaji anazidi kuleta majeshi yake kuvunja ngao yetu.

"Bakhmut, Vuhledar, Limansky na maeneo mengine. Lakini sasa, kama kila siku kati ya hizi 346, ujasiri wa askari wetu ni kila kitu," Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema.

==================
Huu moto sio mchezo 🤣🤣🤣🤣
Asubirie upepo wa Abram na 🐆
 
Inakuaga hivi, leo umemnyang'anya mtu fedha akalia tu, kesho ukarudia akarusha ngumi, keshokutwa ukienda utaenda kwa tahadhari. Kadri unavyorudi inakuwa ngumu zaidi na zaidi mpaka mnaheshimiana au umuue kabisa ili usipate upinzani.

Vita vitakapokwisha vitaacha makovu kwa Ukraine, makovu ni kumbukumbu. Kumbukumbu huzaa maandalizi ya kujilinda, maandalizi ya kujilinda husababisha ugumu zaidi wa adui kufanikiwa kwenye tukio linalofata.
Vita hii haiwezi kuisha ila mpk imuache Ukraine akiwa prorussia au Neutral kbs.

Katika mapendekezo ya Urusi kwenye meza ya mazungumzo ni pamoja na kuweka ukomo wa nguvu za kijeshi za Ukraine.

Hiyo itaifanya Ukraine izidi kuwa dhaifu sana. Mahesabu yanayopigwa kremlin ni makali.

Hii vita kuisha ni ngumu sana. Maana anachokitaka Urusi Ukraine na washirika wake hawawezi kumpa na anachokitaka Ukraine na washirika wake Urusi hawezi kuwapa.

Wakati tunasubiri iishe inaweza kuwa ndio inaanza.
 
Pro upinde wa jf akili zao cjui Nan anawashikia ..yaan mpk zele anasema hali mbayaa ila huku wanakuambia bdo wako vizur ..jamaa kila cku anaangaika kuomba msaada hii inaonyesha kua hali yake mbayaa mnoo ila hapa jf bdo washenzi kazaa wanaendelea kueneza uongo
 
Vita hii haiwezi kuisha ila mpk imuache Ukraine akiwa prorussia au Neutral kbs.

Katika mapendekezo ya Urusi kwenye meza ya mazungumzo ni pamoja na kuweka ukomo wa nguvu za kijeshi za Ukraine.

Hiyo itaifanya Ukraine izidi kuwa dhaifu sana. Mahesabu yanayopigwa kremlin ni makali.

Hii vita kuisha ni ngumu sana. Maana anachokitaka Urusi Ukraine na washirika wake hawawezi kumpa na anachokitaka Ukraine na washirika wake Urusi hawezi kuwapa.

Wakati tunasubiri iishe inaweza kuwa ndio inaanza.
Uzuri mfumo wa hii vita si kama vya middle East, Hatua ya kwanza itakuwa ni mabadiliko ya vizazi. Kina Zele watakufa, kina Putin nao watakufa, kuna kipindi itafika watatokea watu wa kujiuliza kwann tunapigana na watakuwa na jibu na amani itarejea.
 
Ila sasa huo muda utafika!? Tukumbuke Kuna option ya further escalation.

Leo hii Ukraine anapewa vifaru bora sana na mizinga ya masafa marefu. Kesho watapewa ndege vita zitaanza f16 na kuendelea. Itachukua muda gani mpk mstari wa hatari uvukwe!?
 
Ni kweli, hali ni mbaya na haionekani kuwa nzuri, ila muda utakuja silaha zitawekwa chini tu hata ikiwa kwa gharama ya vita vya dunia.
 
Uzuri mfumo wa hii vita si kama vya middle East, Hatua ya kwanza itakuwa ni mabadiliko ya vizazi. Kina Zele watakufa, kina Putin nao watakufa, kuna kipindi itafika watatokea watu wa kujiuliza kwann tunapigana na watakuwa na jibu na amani itarejea.
Ndio, lakini kwa bahti mbaya mara chuki imeenea, kupungua kwake kunaweza kuchukua vizazi kadhaa...
 
Shirika la kijasusi la israel, Mossad" limeripoti juu ya hasara ya Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine: karibu400,000 wameuwawa na kujeruhiwa, pamoja na wanajeshi wa NATO

Sidhani namba hizi i kweli za Mossad. Kwa kawaida yale yanayosambazwa na shirika za ujasusi (hata kwa njia ya panya) husambazwa kote. Namba hizi zinazodaiwa kutokea Mossad, naona hapa tu kwa kurejea tovuti moja ya Kituruki. Waturuki si maarufu kwa ushirikiano wa karibu na Mossad. Biila chanzo cha pili (yaani chanzo ambacho hakikopi Mturuki yeye yule) sidhani ni kweli.
 
Back
Top Bottom