Kwa nini wanasitasita kupeleka hivo vitu ulivyovitaja hapo kumsaidia Ukraine?Wewe unafikiri West wangekuwa na uhakika 100% kuwa hivyo vyuma vingekuwa game changer wangekuwa wanaviangalia tu??
Nyie pia mmekuwa mnawa-over-estimate sana hao WEST, mkiamini wanaweza kufanya watakavyo..au kuwapinga wao ni sawa na kumpinga Mungu.
Mnaamini katika Western based rules and values instead of International based rules and values...Dunia inaenda kuwa multipolar..watu wajifanyie maamuzi yao bila kuangalia agenda ya west.
Russia kafungua njia...na nchi nyingi tu zinaamka na kuwa na misimamo yao dhidi ya ujinga na kujipendelea kwa West, mfano India, China..kuna Arabia pale...wameanza kuonesha misimamo yao, achilia mbali Iran..hata sisi Africa..hatutaki ujinga wa kupelekeshwa...Zelensky alipoomba kulialia kwa AU...watu walimpuuza...aliongea na viongozi 4 tu kati ya 52.....
Kule South America ndo kwanza hawana habari na mgogoro huu...wamekausha kabisa..wanaendelea na issues zao..sababu wanajua ujinga ujinga wa hawa Wazungu.
Wazungu wataelewa tu..in 50 years to come balance of power itashift kupita maelezo...
"Mfa maji hakosi kutapatapa" Ulimwengu umebadilika....mambo ya West kujiona miungu watu yanaenda kuisha...
Sent from my SM-A205F using
JamiiForums mobile app