Urusi ilianza kuenea miaka 500 iliyopita, pamoja na Uingereza na wakoloni wengine. Tofauti ilikuwa tu, Uingereza ilienea hasa ikivuka bahari, Urusi ilienea kwenye nchi kavu. Pamoja na yale niliyokopi chini, katika karne ya 19 Urusi ilivamia nchi za kaukazi (Chechnya, Cherkes country, Azerbaijan, Dagestan, Armenia, Gerogia) nchi za Asia ya Kati (leo KAzakhstan, Turkestan, Uzbekistan, Bukhara, Shiva, Tashkent, Tajikistan, Tannu Tuwa, na mengine).
Soma: As the Europeans began their overseas expeditions in the early 16th century, the Muscovites started their expansion to the north and east. They captured the Yugorian lands by 1502 and reclaimed Ryazan by 1520. They conquered the Kazan Khanate in 1552 and Astrakhan Khanate in 1556, abolished the Great Nogai Horde in 1557, and took the Siberian Khanate in 1582. .... But the Russians amassed even more territory, continuing their Drang hach Osten well into the next century: By 1610 they had absorbed the Pegaya Horde, reaching the Yenisey River, and by the mid-17th century they were approaching the border with China. By 1689 they had conquered all of northeastern Eurasia to the Bering Strait.
Kwanza ni uongo mkubwa kusema Urusi aliyakoloni hayo maeneo kwa maana hayakuwa na utawala wa wenyeji.
Kifupi expansion ya Mrusi ilitokana na kuushinda utawala wa Kimungoli ambao ndio ilikuwa super power wa enzi hizo, ikitawala kutokea Uchina mpaka Eastern Europe, kifupi hata utawala wa kifalme enzi hizo wa kirusi(Muscovites) ilibidi ulipe Kodi kwa Khan wa kimongol na ilikuwa inatawaliwa na Wamongoli.
Aliyekuja kufanya mageuzi ni IVAN III MUSCOVITES katika mwaka 1401 katika battle of KULIKOVO na kuwashinda uwanja wa vita na hapo Mongol Empire ikaanza kuzorota huku Urusi ilianza kuwa na nguvu na kujipatia Uhuru wake,kumbuka hii tayari ni Karne ya 15.
Swali la kumuuliza Umshana ulitaka waendelee kutawaliwa milele na Wamongoli?
Je kipindi hiki, kulikuwa na nchi iliyokuwa kolonized na Urusi?
Mpaka mwaka 1547 ikiwa Chini ya IVAN IV a.k.a Ivan the Terrible.
Mwaka 1552 ndio Urusi kwa Sasa wakawashambulia Wamongoli waliokuwa wanaitawala Kazan kimabavu na kuwapiga, nayo haikuwa nchi.
1557 Warusi Tena wakapiga Astrakhan ulikuwa utawala wa Kimongoli.
Kumbuka Mongol Empire baada ya kifo cha Genghis Khan( Mfalme wa Wafalme) ikabidi isambaratike into a small empire.
Hii ndio loophole aliyotumia Muscovites kunyanyanyuka na kuwa falme yenye nguvu kifupi ndio aliyerithi nafasi ya Mongolia Empire hata Western Europeans people wanapenda kuwaita hivyo.
Hapa Sasa ukamfanya IVAN THE TERRIBLE (GREATEST) kuamua kuufuta ufalme wa Kimongolia uliobakia.
Wakati Urusi inazidi kujipambanua kuwa tawala yenye nguvu kikaibuka kitisho kingine ambacho ni Ottoman Empire iliyokuwa inataka kujitanua upande wa Ulaya, hawa nao walionja hasira za kislav na matokeo yako Urusi kukubalika kuwa kiranja wa dunia ya kislav mpaka leo.
1676-1681(Karne ya 17)
Mnamo Karne ya 18, Urusi ikiwa inaongozwa na Empress Katherine The Great iliweza kupambana vita na kuondoa utawala wa mwisho wa Kimongoli pale Crimea(Khanate of Crimea) mnamo mwaka 1771 Crimean Tatars.
Na huyu ndie aliyeanzisha mji wa Odessa.
Je! Ilikuwa nchi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kama ilivyo Mongolia Empire ambaye mrithi wake ni miliki ya Urusi nao wakarithi maeneo yote ya iliyokuwa miliki ya Kimongoli maeneo kama Siberia, wadagestan, Wachechen, Ingushetia kumbuka hata hii Mongol Republic waliombwa waingie kwenye Russia Federation.
Urusi walifuata tamaduni za Kimongolia ikiwemo utaifa wao hautegemei asili.
N.B Mrithi wa Mongol Empire in eastern side ni Mchina kumbuka, Russia ni western side.
Haya tuambie hii inafanana vipi na Utumwa na Ukoloni waliofanya warithi wa utawala wa Rumi ya Magharibi (Western countries)?
Haya tuambie alivamia nchi Gani iliyo huru?