Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Nakunya hapa hapa kama kweli yupo Bakhmut.ameingia kwa njia gani iyo Bakhmut[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hiyo ya kukataa ni lugha ya kawaida sana kwenye vita kama hii ya sasa.

Iran wanatuma mzigo wa UAVs lakini wamekataa.

US wamelipua bomba la gesi la Russia Nord Stream 2 na wamekataa.

China nao watapelekea mzigo baada ya Russia kufanikiwa zoezi hili la sasa ili mzigo huo uwasaidie kujilinda kwa siku zijazo, na China watakataa hivyohivyo.

Hivyo kukanusha taarifa au kukataa ni kawaida wewe simamia unachokifahamu na kukielewa.

Tatizo ni kwamba sasa hivi vyombo vya habari vya nchi za magharibi vyote vimeweka uandishi wa habari pembeni na kutumia zaidi uongo, kudanganya na habari nyingi za propaganda lakini zote zabuma.

Hivyo kazi kwako ndugu, sikiliza, angalia, chambua na fuatuilia habari hizi kwa umakini.

Ukraine kuna wapiganaji wa kila aina, vyombo na vifaa modern kabisa vya kivita vyatumika na ndo maana yaitwa hybrid war.

Sasa tuje kwa Hezbollah na wapiganaji wengine wa Wagner na wengine kwa upande wa Russia.

Hawa wa Hezbollah wana utaalam wa "urban warfare" au "urban combat" na warusi si wajuzi sana wa vita kama hii ndo maana imewachukua muda mrefu kukamata Bakhmut.

Huo ni ujuzi yaani "skill" na kwa kuwa Russia sasa yaanza kuingia katika miji yawabidi kuwa na wapiganaji ambao ni wana ujuzi wa urban combat na Hezbollah wana ujuzi huo.

Russia imekuwa Syria tangu 2015 hivyo wanaelewa kwamba hawa militants wana ujuzi huo na waliwasumbua sana Russia pale Syria.

Hivyo ndege za kivita za Syria tayari zikikwishawapeleka wapiganaji hawa mapema mno kwa ahadi ya kulipwa dola 200 hadi 300 kwa siku.

Hizi taarifa zipo na weye una kazi ya kuzitafuta chambua na uelewe.

Nao Ukraine pale mwanzoni mwa vita waliwaingiza vitani wapiganaji wapatao 20,000 kutoka barani Ulaya na hii alithibitisha bwana Dymitro Kuleba kwa CNN ambae ni waziri wa mambo ya nje wa Ukraine mapema mgogorop ulipoanza.

Mimi ingawa nipo kivulini hapa Kibaigwa, lakini najitahidi kuchambua kwa makini na sehemu zingine naingia kwa ruhusa maalum, hivyo nikileta hapa huwa ni kwa faida ya wafuatiliaji makini.
 
Kwanza ni uongo mkubwa kusema Urusi aliyakoloni hayo maeneo kwa maana hayakuwa na utawala wa wenyeji.

Kifupi expansion ya Mrusi ilitokana na kuushinda utawala wa Kimungoli ambao ndio ilikuwa super power wa enzi hizo, ikitawala kutokea Uchina mpaka Eastern Europe, kifupi hata utawala wa kifalme enzi hizo wa kirusi(Muscovites) ilibidi ulipe Kodi kwa Khan wa kimongol na ilikuwa inatawaliwa na Wamongoli.

Aliyekuja kufanya mageuzi ni IVAN III MUSCOVITES katika mwaka 1401 katika battle of KULIKOVO na kuwashinda uwanja wa vita na hapo Mongol Empire ikaanza kuzorota huku Urusi ilianza kuwa na nguvu na kujipatia Uhuru wake,kumbuka hii tayari ni Karne ya 15.

Swali la kumuuliza Umshana ulitaka waendelee kutawaliwa milele na Wamongoli?

Je kipindi hiki, kulikuwa na nchi iliyokuwa kolonized na Urusi?

Mpaka mwaka 1547 ikiwa Chini ya IVAN IV a.k.a Ivan the Terrible.
Mwaka 1552 ndio Urusi kwa Sasa wakawashambulia Wamongoli waliokuwa wanaitawala Kazan kimabavu na kuwapiga, nayo haikuwa nchi.

1557 Warusi Tena wakapiga Astrakhan ulikuwa utawala wa Kimongoli.

Kumbuka Mongol Empire baada ya kifo cha Genghis Khan( Mfalme wa Wafalme) ikabidi isambaratike into a small empire.

Hii ndio loophole aliyotumia Muscovites kunyanyanyuka na kuwa falme yenye nguvu kifupi ndio aliyerithi nafasi ya Mongolia Empire hata Western Europeans people wanapenda kuwaita hivyo.

Hapa Sasa ukamfanya IVAN THE TERRIBLE (GREATEST) kuamua kuufuta ufalme wa Kimongolia uliobakia.

Wakati Urusi inazidi kujipambanua kuwa tawala yenye nguvu kikaibuka kitisho kingine ambacho ni Ottoman Empire iliyokuwa inataka kujitanua upande wa Ulaya, hawa nao walionja hasira za kislav na matokeo yako Urusi kukubalika kuwa kiranja wa dunia ya kislav mpaka leo.
1676-1681(Karne ya 17)

Mnamo Karne ya 18, Urusi ikiwa inaongozwa na Empress Katherine The Great iliweza kupambana vita na kuondoa utawala wa mwisho wa Kimongoli pale Crimea(Khanate of Crimea) mnamo mwaka 1771 Crimean Tatars.
Na huyu ndie aliyeanzisha mji wa Odessa.
Je! Ilikuwa nchi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kama ilivyo Mongolia Empire ambaye mrithi wake ni miliki ya Urusi nao wakarithi maeneo yote ya iliyokuwa miliki ya Kimongoli maeneo kama Siberia, wadagestan, Wachechen, Ingushetia kumbuka hata hii Mongol Republic waliombwa waingie kwenye Russia Federation.

Urusi walifuata tamaduni za Kimongolia ikiwemo utaifa wao hautegemei asili.

N.B Mrithi wa Mongol Empire in eastern side ni Mchina kumbuka, Russia ni western side.

Haya tuambie hii inafanana vipi na Utumwa na Ukoloni waliofanya warithi wa utawala wa Rumi ya Magharibi (Western countries)?

Haya tuambie alivamia nchi Gani iliyo huru?
 
Chechnya ni sawa sawa na Mkwavinyika na nchi yake ya uhehe.

Vipi Tanzania imeifanya nchi ya uhehe kuwa koloni lake?

Niambie lini Chechnya lilikuwa Taifa huru?
 
Kwaiyo kwa mantiki yako Urusi ilishinda vita vya ww1 na ww2 kwa kutumia au kutegemea silaha za nyuklia. Hahaha we jamaa wacha ushabiki wa kwenye migahawa I wonder kama hata unajua hii vita imeanza lini na nn na nani ni chanzo come on man be objective what's wrong with you?? Wachana na channel za propaganda alafu la mwisho kasome UN act no.
Kumbekeni hao magaidi wa ukraine hata waliojisalimisha watakuwa wafungwa wa kivita chini ya ulinzi wa Urusi maana wengine msidhani wanarudi nyumbani choice ni mbili tu kufa kwenda kwa bandera na kujisalimisha kuwa mfungwa
 
Mtan'gong'a Sana huu mwaka but Leutenant Colonel Putin anazidisha TU dozi kutegemeana na Aina ya ubishi unaojitokeza.
Nb
Hakuna a
Kama ilivyo kwa Ant Air Defences systems Hakuna Mfumo wa kujilinda wa
kifaru wenye effectiveness ya 100 %

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Tupe sababu kwa nini Barbados iliamua kujitangazia Uhuru wake?

Unafahamu influence anayokuwa nayo Mfalme Charles kwa nchi ambazo zipo chini yake?
 
Ndio maana nikaangalia amejiunga lini JF na pia kumshauri akajifunze Geopolitics

Ningeweza kumuuliza tu swali rahisi kama ili, Je Hezbollah walivyokuwa wanapigana pale Syria walukuwa wanapigana kwa maslahi ya nani?

Anachotakiwa kujua ni kwamba, Hezbollah wanapigania maslahi ya Iran.

Sasa kama Iran wapo Ukraine, hao Izbollaha wanashindwa nini kuwa na maslahi hapo Ukraine?

Sometimes tuna deal na soft brain humu JF.
 
Pro-NATO wamelevya ujinga usibishane nao utapatakio hovyo
 
Huyo jamaa mkimsoma mnadhani ni Mtanzania?? Hiyo lugha anayoandika ni dhahiri anatumia translator..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…