Mkuu unasema kweli haisaidii kuweka tu jumla zote mbili kandokando.
Kama kwenye picha hiyo:
View attachment 2538683
Jinsi alivyosema mtazamaji mmoja: "
Why Russia Gets More Bang for the Ruble"
(jisomee Why Russian Military Expenditure Is Much Higher Than Commonly Understood (As Is China’s) - War on the Rocks)
Ila ukifungua budgets hizo, unaweza kuanza kuliganisha kidogo. Matumizi ya US kwa "procurement" (ununuzi) peke yake ilikuwa bil. 140 (2010) hadi 97 (2013). Tena kiasi kinacholingana (takriban) kwa "Research, Development, Test, and Evaluation (RDT&E)". Hata ukiona Urusi inazalisha vitu nafuu zaidi, sioni kwamba inakaribia viwango hivyo. Tofauti ni ukubwa wa uchumi na hivyo uwezo wa kuwekeza (na kupoteza).
Sababu ya kutoona silaha bora za Kirusi kwenye uwanja itakuwa katika tofauti hiyo. Mfano kutoonekana kwa Armata 14, au ule mfumo wa kulinda vifaru
unaoitwa Arena. Watazamaji wengi wa kimataifa waliona ni bora - lakini karibu hauonekani uwanjani.
Ila ukipendelea kuamini kwamba Urusi kwa sababu zake bado hakuchukua silaha zake bora (ilhali inatazama tu vifo vya askari na uharibifu wa vifaa) - basi si mantiki ninayoelewa.