Unaweza kuiweka hapa hizo picha ya vufaru 1800!?
Taarifa zote za kuwa Urusi imepoteza vifaru 1000 - 1800 zinatoka kwenye vyanzo vya magharibi. Wa kulaumiwa ni Oryix. Na hapo wanasema hiyo idadi ni nusu au zaidi ya vifaru vyote vya Urusi. Taarifa za namna hii ni nyingi kutoka upande wenu kudai Urusi amepoteza kiasi kadhaa au amebakiwa na kiasi kadhaa ambacho hakitoshi. Bila kutoa vyanzo kutoka Urusi taarifa hii hatuwezi kuichukulia maanani kivyovyote vile ni kama tu taarifa za kwamba Urusi imepoteza wapiganaji laki mbili, au urusi imebakiwa na chakula cha siku tatu, au urusi inaishiwa makombora, au Majenerali wengi wa Urusi wamefia Ukraine Nk.
Dalili za kuwa hizi ni propaganda ni, moja, wanaotoa taarifa za loss kwenye jeshi la Urusi wanaclaim wako 'independent' lkn hapohapo hawatoi taarifa za loss kwenye jeshi la Ukraine. Ilitakiwa watuambie Urusi amepoteza kiasi kadhaa na Ukraine kapoteza kiasi kadhaa ili tupate picha halisi ya nani anapoteza zaidi. Je, Unaweza kutuonesha wapi Oryix wametaja kiasi cha vifaru vya Ukraine vilivyopotea hadi sasa!? Kama hawajatoa za Ukraine kwa nini!? Ina maana wao wako commited kuhesabu tanks za urusi zilizoharibiwa tu bila ya kutilia maanani za Ukraine!?
Mbili, Hakuna uwiano mzuri wa namba zinazotolewa na hivyo vyanzo, mf. Taarifa ya Oryix kuhusu vifaru vya Urusi imenukuliwa na WSJ lkn kuhusu vifaru vya Ukraine WSJ wamenukuu taarifa ya IISS ambapo wamesema Ukraine imepoteza kati ya vifaru 450 mpk 700 huku vifaru 950 vikibakia operational. Sasa kama Ukraine wamepoteza vifaru 700 tu na Urusi 2000 inakuwaje Ukraine ndio anaomba apatiwe vifaru kutoka west!? Ukraine hajapoteza hata nusu ya vifaru alivyokuwa navyo kama kweli 950 bado vinapiga kazi lkn urusi tyr ameshapoteza zaidi ya nusu Logic ni kwamba Urusi anapoteza kwa speed kubwa zaidi ya Ukraine na hivyo angepaswa yeye kuomba na sio Ukraine maana kama ataendelea kupoteza kwa kasi ileile basi ataishiwa kbl ya Ukraine. Cha ajabu Ukraine ndio analalamika kutaka apatiwe vifaru zaidi.
Tatu, Mashambulizi yanayofanywa na urusi na mafanikio yake hayaungi mkono madai ya kwamba Urusi amepoteza zaidi au anakaribia kuishiwa. Mf. Kwenye mashambulizi ya juzi Ukraine wanasema urusi amerusha hypersonic 6 hii si dalili ya kuwepo na makombora ya aina hiyo 30. Una makombora 30 na production imesimama alaf kwenye shambulio la siku moja tu unarusha 6 kwa mpigo!? I am not buying! Kuzingatia level ya technology na ugumu wa kuzalisha hayo madude na umuhimu wake na hofu ya kuwepo na further escalation.
Nne, mnataka kutuhamisha kwenye jambo la msingi ambalo ni ushindi kwenye uwanja wa vita. Wakati Ukraine wamefanikiwa kdg kwenye counter offensive yao mwaka jana hakukuwa na taarifa nyingi za Urusi kapoteza tanks ngapi au risasi ngapi bali taarifa za kukombolewa miji ya Kharkiv na mingineyo na jeshi la Ukraine ndio zilitamalaki. Sasa hv hakuna progress yyt ya maana ambayo wanaifanya so wamerudi kureport habari za vifaru, ndege, makombora nk. ambazo Urusi amepoteza. Sisi hatusahau msingi ni progress kwenye uwanja wa mapambano na wala sio nani kapoteza nini wala nini. Km unapoteza vifaa kdg lkn kwenye mapambano umezidiwa unapigwa haina maana. End of the day Urusi wanareport kuchukua kijiji after kijiji after mji after jiji Ukraine wanareport loss za vifaa kwenye jeshi la Urusi kana kwamba wao lengo lao ni kulitia hasara jeshi hilo hata kama linazidi kuchukua maeneo ya nchi yao zaidi. Lets get back to the main agenda. Territory!!! Urusi atolewe Ukraine au Ukraine atolewe East Ukraine. Sio vifaa wala silaha.