Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

NATO hiyo inayopigwa Kama ngoma? Saizi hata ikisogea hakuna tatizo kumbe mdabwedo tu.
Ukweli hata Mimi kabla ya SMO hii,nilikua naiona NATO kama kiboko ya Urusi,aisee SMO hii imenifunza kitu kikubwa mno ambacho nilikua sijui.
Aisee nimegundua Urusi anaidharau mno NATO,nayo NATO inaiogopa mno Urusi.
Aisee kumbe NATO ni kwa vi nchi dhaifu TU kama vi kina Iraq,Libya,serbia Watalaban na Syria..

Maana kwa misaada anayopewa Ukraine haikustahili kabisa kupelekewa silaha peke yake, Bali ilistahili kabisa NATO kuingia full force.

Kwa kifupi "NATO was overated" 😃
 
Ukiwa na pesa nyingi hivi kama Musk kila badiliko la pesa fulani linamaanisha ama faida au hasara kubwa kwenye akaunti yako.

Ila mataifa kujitenga na USD?? Ni ndoto. Nchi nyingi zinapunguza kiasi matumizi ya USD lakini hazijitengi. Miaka kadhaa iliyopita wengi waliofikiri Euro itapita USD lakini haikutokea.
Ona China: In July 2019, China's State Administration of Foreign Exchange announced that at the end of 2014, US dollar assets accounted for 58% of China's total reserves, down from 79% in 2005; adding that its share of US currency assets was lower than the global average of 65% in 2014.[13]
Maana hawakupunguza matumizi ya USD, ila kuongezeka kwa akiba ya forex, waliongeza zaidi Euro na Yen kuliko USD hivyo asilimia ya USD imepungua kwa jumla.

Ona Uhindi: India's foreign exchange reserves are mainly composed of US dollar in the forms of US government bonds and institutional bonds.[5][6] with nearly 7.34% of forex reserves in gold.
Uhindi bado sehemu kubwa kabisa ni USD.
Una namba zozote zinazoonyesha Ruble?? Katika nchi gani?
Urusi pekee kwa sasa imeweka asilimia kubwa kwa dhahabu 8ambayo ina hatari yake kiuchumi) na Renmin ya China. Ila wanafanya vile kwa sababu akiba za USD zao zimekamatwa na akaunti kufungwa.
Ona wastani wa nchi 149:
View attachment 2574290
Uwezekano mkubwa Dolar itaendelea kupungua polepole. Ila Ruble haitakuwa sarafu ya kimataifa.
Soma:
In the last two centuries, the world has seen three significant reserve currencies. The pound sterling dominated in the 19th century. In the course of half a century, the US dollar gradually overtook sterling. In the last decade, the euro has emerged with 27 percent of global currency reserves, while the dollar still holds two-thirds. Sterling and yen account for 3 to 4 percent each, leaving less than 1 percent for other currencies.

The real question is whether the dollar will disqualify itself as a reserve currency and give way to the euro, or possibly the Chinese renminbi in a few decades.
But the ruble hardly complies with any of the arduous demands for a reserve currency, having become convertible as late as July 2006.

Boss, Urusi hajawahi Sema anataka Ruble iwe fedha ya kimataifa, nilichosikia na kuona machapisho ni kuwa; Kila taifa linalofanya Biashara na taifa fulani basi watumie sarafu za Nchi zao...kama wewe ni British unanunua simu Ufaransa, tumieni Pound na franc kwa mauziano yenu...huku bongo tunanunua Sana vitu kutoka Kenya India China na Japan, tunazo exchange zao hapa chin, kwanini tuhangaike kuweka Akiba ya makaratasi ya nchi ambayo haihusiani? Ndicho Urusi anataka kukitoa..kila mtu Anunue kwa fedha za Nchi unayonunua kitu chako, no uza kwa fedha ya nchi yako.....Unayajua malengo ya Euro? Lengo ni kuipa nguvu dollar, siku akikupiga sanction yaani ndan ya siku Moja keshakumaliza...Tumewashtukia wahujumu uchumi wa nchi Nchi zetu ni nyie mnaoipigania Dolar iwe medium of exchange
 
Mkuu, hilo pori si ndio linaleta mgogoro? Gesi Mafuta makaa mbolea, mashamba....si ndio yanayowatoa udenda US had anaanzisha cold war? Au sababu ya Ukraine 'kuvamiwa' ni nini haswa...labda hatujajua kwanini Urusi 'imeivamia' ukrain
Hilo pori ninaposema ni Urusi wana eneo kubwa na republics maskini kibao kama Tuva kwa kina Shoigu. Maeneo uelekeo wa kwenda Mongolia sijui Tatar na Ulan Ude wana umaskini na hayajaendelezwa, kukosa rami kawaida na population ni sparse. Kwenye machimbo kidogo na gesi ndio kuna unafuu na yakiisha madini wanabaki na ghost towns. Siberia eneo kubwa. In short Russia is uneccessarily big na pupulation yake ya karibia milioni 150.

Sasa bado wanahangaika na Ukraine badala waendeleze nchi yao. Nani avamie yale mapori, Russia halisi iko Western uko St. Petersburg, karibia na kati uko Moscow na kusini kina Sochi. Mashariki uko Chechnya ndio maana walipigana kujitenga, ni kama hawapo.

Ukraine imevamiwa kwa sababu zilezile za kuivamia Georgia na ujinga wa Urusi ni kuvamia jirani tena waliokuwa nao Soviet block. Hutoona Marekani inaivamia Canada au Mexico
 
Mtu anayesema maneno kama haya unawezaje kumuunga mkono!!

“We’ll defeat everyone, we’ll kill everyone, we’ll rob everyone we need to. Everything will be as we like it,”
 
haya maneno ya kwenye Kanga ndio yanayokuonyesha uko wa kawaida kiasi gani??...!!!...Super Power Uchwara ... Europe yote inayumba sababu yake...., kuna nchi inayoweza kuonyesha direct threat kwa US hapa duniani na ikabaki salama kama anavyofanya Russia..???....hata China na uchumi wake mkubwa ... hawez onyesha umwamba namna hii..mbele ya US na akabi salama...!!
Mbona huzungumzii ile Shadow Military Command ya NATO...iliyofunuliwa na Kinzhal hypersonic missile.. na kuteketeza 100's ya NATO Specialists...??

Marekani....hana uwezo wowote wa Kijeshi wa kuifanya Russia...hana...combined na NATO yote...,,, kama ni Conventional Millitary Hardware...kwenye SMO hii.. Russia ameonyesha ni Mwamba kiasi gani..,,Nuclear hata tusiongee sababu iko wazi nani ni mwamba...!!!

Silaha kubwa ya Marekani kwa Russia ilikuwa ni 'Sanctions'...ndio maana mwanzoni mwa Vita .. BIDEN alikuwa anampiga mikwara PUTIN...waziwazi kwamba atajuta...sasa ni mwaka zaidi...US hana cha ziada kwenye Sanctions...amemaliza vikwazo vyote...hadi kwa michepuko ya PUTIN todate hakuna kilichofua dafu...!!!

hv nchi kama Russia kwa yote inayoyafanya kupambana na Collective West.... huku akiwa the most ever sanctioned Country on Earth..
na bado anawakilisha namna hii...unawezaje kumuita Super Power Uchwara...!!!...lazima either Mahaba ya West yamekuzidi au unajitoa ufahamu...

Issue ya Finland...PUTIN alishasema wazi hana tatizo na hzo nchi kujiunga NATO..but issue itakuja hao NATO watafanya kitu gani baada ya kuingia hapo...!!!


Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Umetema madini adimu sana Mkuu.
Pongezi kwako.
Umeandika fact tupu mwamba.
 
As a result of the terrorist attack in St. Petersburg, two people died - in addition to Vladlen Tatarsky, an unknown woman was killed.

18+ The footage of the first minutes after the explosion shows the bloodied body of a woman - she lies on the sidewalk near the cafe
1680460520240.png
 
MBULAMATALI ukiona mtu anatishia ni dhaifu!!

Urusi haitishii Ulaya kutokana na uwezo wake bali kutokana na Rasirimali anazozimiliki za nishati. Nje ya mambo ya nishati, Urusi inaweza kuiambia nchi gani ya ulaya isifanye kitu fulani na nchi hiyo ikatii isifanye kama Marekani inavyoiwekea vikwazo Urusi na nchi zote zinatii!!??
 
Hajaishiwa ndio maisha yake yalivyo kwake, ila kwa mtazamo wa kimagharibi kaishiwa. Niliwahi andika tatizo la rushwa, kutojali na wizi wa mali za umma kwa Urusi ni kubwa na lipo sana jeshini. Unategemea nini kwa nchi ambayo matajiri wake wakubwa karibia wote ni oligarchies, nchi zingine kubwa utasikia huyu kakusanya mitaji kuanzisha kampuni ya magari ya umeme, huyu kaanzisha kampuni ya kuuza vitu online, huyu ana kampuni ya teknolojia ndio matajiri hao. Urusi matajiri wake ni huyu alibinafsishwa kampuni ya mafuta USSR ilipoanguka, huyu alibinafsishwa machimbo ya makaa ya mawe, huyu aluminium.

Urusi on paper ina vifaru vingi sana, doctrine yao ni kuwa na namba kubwa haijalishi performance na serviceability ikoje. Wana vifaru kama T-54 vimetengenezwa miaka ya 1950s kabla Stalin hajafariki na walifanya upgrade unakuta miaka ya 1960s ndio navyo wanahesabu. Wakati Ujerumani ina Marder IFV ambayo ya kwanza ilianza tumika 1971 (vifaru vya T-72 vimeitangulia Marder kutumika). Ujerumani imeshastaafisha Marder inaziona outdated ila ilizihifadhi kwenye maghala ya ndani. Wakati Urusi kwa T-72 ni vifaru havitarajiwi kuondoka, T-64 yenyewe bado inatumika. Au Ujerumani jinsi imeziondoa Gepard SPAAG jeshini inaziona za kizamani ila Ukraine imepewa na zimesaidia. Urusi yeye ndio wale watu wanatumia iPhone 7 hadi leo.

Maghala ya silaha ya Urusi mengine hayatunzwi kama haya na hivi vifaru kwenye makaratasi wanavihesabu, hapa wakienda ni kuongeza explosive reactive armour, electronics na marekebisho kadhaa kisha kuwapa wapiganajiView attachment 2574014View attachment 2574015
Basi ndo maana hawavionei huruma kama pale Vulhedar walikuwa wanavijaza tu hawaoni tatizo.

Kwa ufupi communists hawana uoga kwa wanajeshi wake kuuliwa.
 
Pamoja na kubadilisha makamanda wa vita mara tatu bado superpower uchwara anapuyanga. Na si mjajifanya mnaifukuza NATO sasa Finland inakuja inaongeza mamia ya kilomita za mpaka, kapigane na uko tena ndio wako jirani zaidi na Urusi.
Mwezi March kilichoongezeka ni 0.01% ya ardhi ya Ukraine, akili kisoda nguvu nyingiView attachment 2574038
Hii vita imesaidia tujue mambo mengi sana.

Hii vita imeonesha jinsi West walivyokuwa wakiiogopa Russia
Imeonesha jinsi Poland asivyo mwoga
Imesababisha Finland kuwa Mwanachama wa NATO
Imesababisha drone zionekane hatari sana
Imeonesha jinsi Russia asivyo kama tulivyomtarajia

Imeonesha pia kuwa China hana uwezo wa kuivamia Taiwani
 
Usijali boss, Ukraine itaishinda Urusi, US ataendelea kuitawala dunia, West wote watamsapoti Ukraine, US ataingia Indopasific kuvuruga awake ufalme wake, ameshaweka miguu afrika Ref: Kamala's trip....maombi yako yatatimia dunia kuwa utumwani.
US hajavuruga Indo-Pacific. Japan, South Korea na Taiwan ziko bega kwa bega na US na zinafanya vizuri sana kiuchumi na kila kitu. Huwezi nitajia nchi tatu zilizokuzwa kiuchumi na Urusi dunia nzima.

Nchi inavamia majirani ingekuwa na uwezo si ingevamia nchi za mbali ila uzuri ndio uwezo haina. Kwa Urusi hii uwezo wa kuvamia mfano Brazil haina kabisa kabisa
 
Mkuu bila shaka athira ya Marekani itaendelea kupungua polepole. Ila naona kwa miaka inayokuja USDollar itaendelea kuwa sarafu kuu duniani.
China imewekeza kiasi kikubwa cha pesa yake kwenye USD ili haiwezi kuachana karibuni.
Ujue China sarafu yake haiendeshwi na soko, bali CPC wakiamua ifanya iwe au isiwe na thamani ni kitendo cha dakika tu

Dollar inaaminika sababu inaendeshwa na soko
 
Dah!...hivi outdated T-54 ndio vitakavyopambana na Vifaru vya Challenger, Abrams na leopard ?....

T14 Armata zipo wapi ?au ni kwa ajili ya gwaride tu ? Urusi kwa man power na silaha nyingi walizonazo hapo Bakhmut bado pamekuwa pagumu ....... ... hii counter offensive huenda ikashangaza dunia.
Walileta T90 zimeharibiwa vibaya hapo Bakhmut
 
Boss, Urusi hajawahi Sema anataka Ruble iwe fedha ya kimataifa, nilichosikia na kuona machapisho ni kuwa; Kila taifa linalofanya Biashara na taifa fulani basi watumie sarafu za Nchi zao...kama wewe ni British unanunua simu Ufaransa, tumieni Pound na franc kwa mauziano yenu...huku bongo tunanunua Sana vitu kutoka Kenya India China na Japan, tunazo exchange zao hapa chin, kwanini tuhangaike kuweka Akiba ya makaratasi ya nchi ambayo haihusiani? Ndicho Urusi anataka kukitoa..kila mtu Anunue kwa fedha za Nchi unayonunua kitu chako, no uza kwa fedha ya nchi yako.....Unayajua malengo ya Euro? Lengo ni kuipa nguvu dollar, siku akikupiga sanction yaani ndan ya siku Moja keshakumaliza...Tumewashtukia wahujumu uchumi wa nchi Nchi zetu ni nyie mnaoipigania Dolar iwe medium of exchange
Mkuu unaota ndoto nzuri lakini umeshajiuliza kwa nini nchi nyingi (zote?) zimeweka akiba ya sarafu chache, hasa USD, Euro, Pauni, pia Yen na Renmibi?
Labda kwa sababu wameona faida kufanya vile? (maana hakuna anayekulazimisha kununua pesa fulani..).
Labda pia ukifanya leo mkataba na nchi nyingine kununua mafuta yao au gesi yao au labda madini au pia vipuli vya mashine KWA MWAKA UJAO unataka kuwa na uhakika kuhusu gharama? Na hivyo hupendi kupatana kwa aina ya pesa inayojulikana kuchezacheza thamani yake?? Na kupendelea pesa ianyojulikana kuwa na thamani thabiti zaidi?
Unaonaje?
 
MBULAMATALI ukiona mtu anatishia ni dhaifu!!

Urusi haitishii Ulaya kutokana na uwezo wake bali kutokana na Rasirimali anazozimiliki za nishati. Nje ya mambo ya nishati, Urusi inaweza kuiambia nchi gani ya ulaya isifanye kitu fulani na nchi hiyo ikatii isifanye kama Marekani inavyoiwekea vikwazo Urusi na nchi zote zinatii!!??
Isipokuwa siku hizi nchi za Ulaya hazitaki tena nishati za Urusi... (ukiacha jitu kama Hungaria na Serbia..)
 
Isipokuwa siku hizi nchi za Ulaya hazitaki tena nishati za Urusi... (ukiacha jitu kama Hungaria na Serbia..)
Hili jambo tulijadili bila ya kuleta ushabiki. Kiuhalisia Marekani ina uwanda mpana zaidi wa kuaminika kuliko Urusi linapokuja suala la uchumi, kijeshi hata mahusiano ya kimataifa. Uimara (Stability) wa Marekani kwenye nyanja mbali mbali hautiliwi shaka sana kuliko Uchina au Urusi.
 
Hilo pori ninaposema ni Urusi wana eneo kubwa na republics maskini kibao kama Tuva kwa kina Shoigu. Maeneo uelekeo wa kwenda Mongolia sijui Tatar na Ulan Ude wana umaskini na hayajaendelezwa, kukosa rami kawaida na population ni sparse. Kwenye machimbo kidogo na gesi ndio kuna unafuu na yakiisha madini wanabaki na ghost towns. Siberia eneo kubwa. In short Russia is uneccessarily big na pupulation yake ya karibia milioni 150.

Sasa bado wanahangaika na Ukraine badala waendeleze nchi yao. Nani avamie yale mapori, Russia halisi iko Western uko St. Petersburg, karibia na kati uko Moscow na kusini kina Sochi. Mashariki uko Chechnya ndio maana walipigana kujitenga, ni kama hawapo.

Ukraine imevamiwa kwa sababu zilezile za kuivamia Georgia na ujinga wa Urusi ni kuvamia jirani tena waliokuwa nao Soviet block. Hutoona Marekani inaivamia Canada au Mexico
Kilichoiangusha USSR 1991 nadhani huwezi kukitenga na hiki kinachoendelea pale Ukrain Mkuu..
 
Back
Top Bottom