Kuna kitu kinaitwa "3:1 Rule of Combat". Invading force inabidi iwe kubwa mara tatu ya defending force kama wana nguvu sawa kwenye front. Russia inahitaji wanajeshi wengi zaidi kupiga Bakhmut kuliko Ukraine. Hivyo hivyo kwenye loss za KIA na WIA Russia inapata wengi zaidi ya Ukraine kwa mathematical model hii ambayo iko proved since WW1 na WW2 na vita mbalimbali.
Russia nayo inapoteza wanajeshi, inatumia resources na budget, inapoteza zana za kivita, wear and tear inaleta logistical nightmare na service, battle fatigue, demoralising the troops watu mnapigana tangu May 2022 mnatokea Luhanks iko chini ya Urusi tangu 2014 na iko kama 150km kutoka Bakhmut ilipo ila hadi leo kuchukua eneo lililo umbali wa 150k mnashindwa wakati mnajiita second strongest army in the world. Nchi ishaanza kutumia vifaru model ya enzi Mwalimu Nyerere anavaa kaptula wewe unadai inaweza pigana miaka 10😂
View attachment 2580719
Kuwazuia Warusi wasisonge mbele sio propaganda, ndio vita yenyewe hiyo, au ulitaka waimbiwe kwaya. Kwani malengo ya Ukraine ni nini kama hilo sio mojawapo.
Urusi haina uwezo kupigana sehemu yoyote miaka kumi, labda wawe waasi wavaa makatambuga. Last time I checked USSR ilipigana na Mujahedeen pale Afghanistan wakashindwa vita wakaondoka 1989, na 1992 wakavunjika muungano. Hapo walijitutumua kupigana miaka mingi wakaambulia kusaga uchumi wao, Russia yenyewe ndio ilikuwa mstari wa mbele kuvunja muungano.