Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hongera kwa kuungana nao... Mshahara wa mwisho w mwezi ukagawane na wanao maisha magum...
Kiboko ya Putin 👇

Screenshot_20220314-065133.png
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mjomba unajitekenya na kucheka mwenyewe...

Kwani alyeanza kuzuia vitu au kuweka viwazo ni Russia au Western? Nimekuuliza swali jepesi tu ka lengo lla Western ni kuua uchumi wa Russia na kuhakikisha hakuna thumuni inayoingia pale why bdo wanaendelea kulipia every day 1USD Billion kwa delivery ya Gas kwenye nchi zao mpk dakk hii naandika apa.

Unaenda kunyanganya Club kwa mtu aliye karib na Putin... Club yenye value ya less than 3Billion Dollars akat huo huo mnapeleka pesa kila uchao kununua Gas yake...

Hivi na kwa akili ako unawaza China India Brazil na wa kupokea Command kutoka western wa nn wafanye? Hyo Gulf regions yote wataungana na Russia kumuekea vikwazo...?

Kwa akil ako ilivo programmed unaamin USA ndo Dunia, unaamin Europe ndo dunia...

So mbay lakin [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] endeleeni kujifariji... Mda ni mwalim mzuri sana....

Ata mtoto wa darasa la pil ukimuuliza baba mmoja analipwa Mil1. Ila ana wake watatu... Na kuna mwingine Analipwa Mil1. Ila ana mke mmoja. Je ukigawa kipato kea matumizi nani atabaki na akiba haraka haraka atakwambia mwenye familia moja.

USA anazalisha about 11Million barrer per day ila ana population ya mara tatu zaid ya n ana Demand ya energy mara 16 zaidi kuliko Russia anaezalisha kiwango kile kile kwa population one third ya Marekan na Demans ya energy nchini kwake just as little as 6.25% ya nishati anayoihtaji Mmarekan na apo kwa upande mmoja tu wa nishati viwandani sijazungumzia mahitaji ya Raia katika Umeme na vifaa vya moto....

Chambua data zao vizuri Gas and Oil inatumika wapi... Why Germany why China?

Among the top manufacturing Hub ni hizi nchi apo chini...

1. China 28%
2. USA 16%
3. Japan 7.5%
4. Germany 5.3%
5. India 3.1%


Ndani ya Top 5 tu apo BRICS kuna nchi 2 ambazo kwa pa1 zinachukua More than 32% of the world Manufacturing hub af bado waidharau BRICS?

Hivi western kawapa nini nyie watu...? So kufeed hzo industry nishati utegemee Mchina na India kuungana na huyo baba enu kumpiga vita Russia?

Hujiulizi kwanini Gerrmany kaacha kufata mkumbo yeye na Rais wa Ufaransa wameanza kuzungumza na Xin Jinping kutafuta suluhu ya kidiplomasia kwenye huo Mgogoro?

Haya kwe hizo nchi 10 hakuna Russia... Maana ake nn? Demand ya Nishati kwake ukilinganisha na walioko nje ya mipaka yake iko tofauti kbs.

Hesab zingine za kitoto sana... Em chukulia mfano GDP ya Mmarekan ni Trillion 20 hivi dollars but GDP per capita ni just 63kUSD...

Total GDP ya Singapore ni 340Billion Dollars ambayo ni just 1.21% ya GDP ya mmarekani... But GDP per Capita ya Singapore ni 62kUSD ambapo wako on Par na USA

Note hyo (Hii ni GDP nominal sio GDP kwa PPP)

Sa kutoka apo kuna point hamtaki kuichukua... "Population"... "Demand"... "Supply". Mnabak mna analyze kisiasa...

Sasa siasa na Uchumi wapi na wapi... Number hazidanganyi mjomba. Kaa kwa kutulia tu tusichoshane Mjukuu wa Yahaya... Endelea kusimamia hicho hicho kilichomo akilini mwako huu mjadala tuufunge...
1. GDP haina maamuzi kwenye kushika uchumi wa dunia. Nchi zote zinazoongoza GDP ni zenye watu wachache hata hii Tanzania mtembeza bakuli yenye watu milioni 60 ukifukuza watu wote maskini ukabakiza wenye hela milioni moja tu utakuta Tanzania iko among nchi zenye GDP kubwa na hapo haina maamuzi yoyote kiuchumi duniani. Nchi zote zenye GDP ndogo ndio zile zenye watu wengi sana kina India na China.

2. Marekani kuongoza katika matumizi ya mafuta na nishati kwa ujumla ni ishara ya kuwa na uchumi wa viwanda. Nchi yenye uchumi mkubwa hutumia nishati kubwa sana ya ndani na nje, Russia anahitaji nishati kidogo kwa kuwa uzalishaji ni mdogo.

Russia nchi kubwa ila population ndogo, maisha ya kawaida. Unaweza nitajia Mmarekani gani amehamia Russia? Sasa Marekani kuna Warusi kibao kina Sergey Brin co-founder wa Google. Uliwahi sikia billionaire wa Uingereza anaenda kuishi Urusi, sasa London pale kuna hadi mtaa ni oligarchies Warusi kibao. Hata wewe hapo ukute unatamani kwenda Marekani au Western Europe kuliko Urusi

3. Kuwa world manufacturing hub hakukufanyi uongoze uchumi wa dunia. Huawei wakati inawekewa vikwazo ilikuwa inakuwa ya kwanza au ya pili kwenye uuzaji wa units nyingi za simu duniani. Leo ya ngapi? Hata top 10 haipo. Huawei ilizalisha kuliko kampuni yoyote ya Marekani ila teknolojia zote za uzalishaji wa simu karibia zinaanzia kwa Mmarekani. Kama uzalishaji unakufanya uongoze Huawei isingeshuka uzalishaji zaidi ya 80% tangu ipigwe vikwazo 2019. Watu kama nyinyi mlikuwa mnajifariji leo hii hata mkipewa latest Huawei mtalazimika muwe na nyingine pia.

India imefanya outsourcing ya technology na wanaenda uko kwa sababu kuna cheap labour wakutumikishwa bila gharama kubwa. Wafanyakazi wa Marekani na Ulaya wanalindwa na sheria nyingi zinazofanya gharama za uzalishaji ziwe kubwa. Hata China ilianza hivyo ingawa inatoka uko sasa. Ukichukua S&P 500 unakutana na makampuni 500 ya Marekani yaliyowekeza dunia nzima na ukiyalinganisha na hizo India, China na Russia utakuta hawakaribii hapo. Makampuni ya Marekani yameajiri dunia nzima, yanamiliki patents na yanazalisha dunia nzima wewe ukija unaangalia nchi zinazozalisha kwa uwekezaji wa nje. Mbona mojawapo ya sababu ya wazungu kutafuta makoloni Afrika ni kupata cheap labour? Bila mzungu kuja kutumikisha watu Tanganyika isingeongoza kwenye katani, wala Ivory Cost na Ghana zingeongoza kwenye cocoa
 
Ashakumu si matusi 98% ya Pro Putin wanashida ya kuchambua vitu critically.

Yaani wanabishia uwezekano wa Russia kuomba msaada kwa China.

Kabla ya Russia kuivamia Ukraine, Marekani ilisema kabisa kuwa Russia itaivamia Ukraine na zaidi ya yote ikasema hadi siku.

Sasa inakuwaje ishindwe kuwa na Intel kama hii?
 
Mkataba wa kiusalama tu mkuu, zenji hawezi kualika maharamia kwa kuwa ati yeye ni sovereign wakati ni memba wa muungano na sisi! Tuna act kama protectors na wao lazima watu protect pia ila wakianza kukaribisha mamluki haipendezi na ni lazma tuhoji.

Ni sawa na mkeo aamue kupanda kitandani akiwa ameshika kisu kisha umuulize kwanini anafanya hivyo akwambie ana uhuru wa kufanya anachojiskia usimpangie. Sijui kama unaweza ukapata hata lepe la usingizi😅
Mkuu,
USSR Ilishaanguka na Gorbachev uko 1990's sasa kilichobakia ni ujirani na common grounds, sasa Ukrain ni free sovereignty kama ilivyo Russia, Lakini pia cold war ilishaisha.
Russia anaogopa nini wakati ana NUKES kama zote?
 
Sasa wanapata nini kutoa uongo kama huu?

Ila Us ni wajinga sana, afu biden wananchi wake wanalia gas imepanda anaacha mambo ya msingi anaenda kupoteza muda kwenye vitu vya kijinga
Hivi kwa akili ya kawaida ulitegemea China itakubali huku Marekani ilishatangaza Secondary Sanctions kwa yoyote atakaemsaidia Russia?
 
Mkuu,
USSR Ilishaanguka na Gorbachev uko 1990's sasa kilichobakia ni ujirani na common grounds, sasa Ukrain ni free sovereignty kama ilivyo Russia, Lakini pia cold war ilishaisha.
Russia anaogopa nini wakati ana NUKES kama zote?
🤣🤣
 
Hivi kwa akili ya kawaida ulitegemea China itakubali huku Marekani ilishatangaza Secondary Sanctions kwa yoyote atakaemsaidia Russia?

Kila mtu anakuja na hoja kutoka source yake, na mwingine anakuja ku disprove hiyo source kupitia source yake

Sielewi yupi ni yupi, yupi mkweli yupi muongo

Yani kiukweli mnazidi kuniacha highway kwenye hili swala
 
Back
Top Bottom