Dah!
Sikutegemea kama Kuna watu mna mawazo finyu namna hii,wala sikutegemea kama Kuna watu mna upeo wa chini namna hii.
Kwa maelezo Yako hapo juu ya habari uliyoikopi unaonesha kuipa sifa USA kuwa USA hua haikurupuki,aisee hapo ndio nimekutoa thamani kabisa,ingawa simaanishi kukutukana.
Nilitegemea ungekerwa na taarifa hiyo lkn naona kama umevutiwa na kufurahishwa.nadhani ni muendelezo wa kudhani kua USA Ina akili na uwezo kuliko nchi zote duniani lakini si kweli ndugu yangu.
USA inaongoza kwa propaganda na uongo kuliko nchi zote duniani na nadhani mtego huo hata wewe ndo umenasa.
Napenda kukufahamisha Kila alichonacho USA na nchi nyingine wanacho,ila wamezidiwa kw propaganda TU na USA.
Sasa kwa hiyo taarifa uliyoileta ni taarifa ya aibu kwa taifa la Marekani.
Ni aibu kwa sababu huo ni ushahidi wa wazi kua yeye ndie alie na anae chochea vita hii.
Hata hivyo napenda nikufahamishe kua pamoja na aibu hiyo lakini napenda kukuhakikishia kwa kutenga bajeti hiyo unayoisifia kwa ajili ya Ukraine Marekani AMEKURUPUKA pakubwa sana, na siku zote Marekani ndio mkurupukaji mkubwa kuliko taifa lolote hapa duniani,ila propaganda ndio Huwa zinawapumbaza nyie mnaoishabikia.
Ntakueleza.
Unajua kua Marekani pamoja na sifa zote mnazompaga kuhusu ujasusi ,je unajua kua ilikua haiufahamu vizuri uwezo wa kijeshi na kiuchumi wa taifa la Urusi kabla ya vita hii?
Kwa maelezo hayo kwenye hiyo note uliyoikopi na unajua kua USA ilishapanga miaka zaidi ya minane kuiprovoke Urusi ili ipigane na Ukraine kisha Urusi ishindwe.
Kwa taarifa walizokua nazo juu ya Urusi walijua vita ikianza na kwa kua walishajipanga Hawa USA na NATO basi Urusi haitachukua muda itakua imekwisha anguka.
Lakini haikua hivyo kwa sababu kama nilivyosema hapo juu kuwa pamaoja na masifa yote mnayompa Marekani lakini hakua na taarifa za kutosha za uwezo wa kijeshi na kiuchumi wa Urusi.Na pia Marekani ilikurupuka sana tofauti na unavyoisifu wewe.
Sababu zangu ni hizi:
Baada ya vita kuanza Marekani aliziamsha nchi zote za magaharibi ziiwekee Urusi vikwazo nazo kwa ujinga zikaiwekea,hapa Marekani alilenga kuharakisha kuiangusha haraka sana Urusi kijeshi na kiuchumi,nadhani mpango huu ulipangwa kabla hata ya vita huko kwenye corridor za Marekani,lakini huu ni mpango ambao Marekani alikirupuka pakubwa sana,kwa sababu nadhani wewe ni shahidi vikwazo vinawala wenyewe Sasa hivi kuanzia Marekani mwenyewe, na washirika wake.
Hii maana yake Marekani hakua na taarifa za kutosha za uchumi wa Urusi.
Kurupuko la pili.
Marekani ilitenga fedha kibao kwa ajili ya kuisaidia kijeshi Ukraine pamoja na nchi za NATO.sasa je unaweza kupima mafanikio ya fedha hizo kijeshi katika vita hii inayoendelea ?
Je Ukraine na NATO wanafanikiwa au wanapoteza?
Maana Ukraine tayari keshapoteza ardhi.
Lakini je ulishawahi kufikiria maisha ya askari na raia wa ukraine?
Je hauumiii kuona wanakufa kama nzige waliopuliziwa sumu?
Je ulishawahi kufikiria kuhusu miundombinu ya Ukraine kama miundombinu ya umeme,mafuta,majengo mazuri,vifaa vya kijeshi vya mabilioni jinsi vina yoteketezwa na Urusi?
Je bajeti hiyo imeisaidia Nini Ukraine?
Je hujawahi kusikia nchi za NATO zinavyolalamika kuishiwa silaha?,silaha hizo zinakwenda wapi?
Kwa kifupi USA ilidhani kwa michango hiyo ya silaha Urusi ingekata moto.lkni wapi Hadi Leo Urusi mambo ni shwari kabisa na inazidi kuzichoma moto silaha za NATO.hilo lilikua kurupuko la pili.
Kurupuko la Tatu.
Mara baada ya SMO kuanza USA ilipita Dunia nzima kuzishawishi,kuziamuru na kuzitisha nchi eti zisijaribu kuisaidia Urusi.
Hapa Tena inaonesha kua dhahiri kua USA haikua na taarifa za kutosha juu ya uwezo wa kijeshi wa urusi.walidhani Urusi itaonba msaada kwa nchi nyingne hasa walidhani kwa china.china ilisema Haina mpango wa kuisaidia Urusi kwa sababu Urusi inajitosheleza na kweli Urusi haijachukua msaada wa nch yoyote.
Sasa hili kurupuko la Tatu ndio limekuja kinyume na USA ,kwani nchi nyingi zimegoma kumtenga Urusi kisiasa kiuchumi na kidiplomasia,zaidi zimeamua kumtenga USA mwenyewe kwa kuanza kukataa fedha yake USD na kuanza kutamani kushirikiiana na umoja ulioasisiwa na Urusi yaani (BRICS).
Hilo lilikua kurupuko na Sasa linaila Marekani yenyewe.hebu fikiria nchi kama Saudi Arabia nayo inaikataa Marekani na kuungana na urusi.nadhani hapa intelligensia ya USA haikuona athari hii
Makurupuko mengine ya zamani.
Nakuonesha makurupuko ili kupinga hoja Yako kua Marekani hua haikurupuki.lkni USA ndio mkurupukaji mkubwa hapa duniani.
Makurupuko mengine:
Kurupuko la nne.
USA alipoona Ufaransa kachukua kichapo Vietnam akakurupuka kwenda eti akidhani yeye ataimudu Vietnam,kilichotokea wote tunakijua na historia imeshaandikwa.
Kurupuko la Tano:
Aliwachukua waasi wa Cuba akawafundisha,akawapa silaha na yeye akaongozana nao,kichapo alichokula kutoka majeshi hatari kabisa hapa Duniani ya Cuba hata kuja kukisahau,huyu Marekani huyo!
Kurupuko lla sita:
Alisema Iraq Inamiliki silaha za maangamizi,kapeleka wanajeshi wakauana na hawakukuta hata sumu ya panya.Aibu hii na imeshaingia katika historia Leo huko USA wanajuta TU.
Kurupuko la Saba:
Walikwenda kwa mbwembwe zote Afghanistan kutaka kuwaangamiza, kuwashinda na kuwatoa Watalaban madarakani.
Walikaa miaka 20 na matumizi makubwa na bajeti ya miaka 20 kama hiyo hapo uliyoweka ,matokeo yake wamarekani wakafurushwa kwa kukimbia na kuacha silaha ambazo hakuana nchi ya Afrika yenye silaha kama zile,na kichekesho kikubwa ni kwamba watalabani wamerudi madarakani.
Hili kurupuko linaambatana na aibu.
Kurupuko la nane:
Walienda Somalia,kuingilia vita za wababe wa vita wa Somalia,akina General Morgan, General Mohamed Farah Aideed na ma Warlord wengine,kitu walichofanyiwa huko ilibidi wanachi wa Marekani waandamane ili majeshi ya Marekani yarudishwa nyumbani.hili kurupuko haltakaa lisahaulike huko USA.
Aisee kwa hakika USA kakurupuka katika mambo mengi sana,na safari hii kaingia chumba Cha wacheza "chess",atatulia TU.
Kumbuka Dunia Sasa inaelekea Kwa akina BRICS,na USD Sasa inaenda kua fedha kama fedha nyingine TU,mfano Franc ya Ufaransa.
Ufalme wa USA kidunia unaenda kua wa kawaida kama wa Muswati wa Zwaziland.
Ujasusi wa USA ulishindwa kuiona nguvu ya Urusi.
Licha ya vikwazo vyote,michango yote ya silaha,Na mabajeti ya ulinzi yote lakini vyote vimeshindwa kuilemaza Urusi.
Kumbuka NATO wakiingia rasmi jua kua bila kukaribishwa China,Korea kaskazini,Iran,Syria na wengi tusiowajua wataingiza majeshi.
Sababu yangu ni ileile kua wanajua kama Urusi akishindwa na NATO kituo kinachofuata ni wao,kwa hiyo wanaona ni Bora wafe wakiwa wamesimama kuliko kufa wakiwa wamepiga magoti.
Je unadhani mziki wa Urusi,china ,Korea Kaskazini,Iran,Syria na mataifa mengine yaliyokaa kimyaa ni wa kitoto?
Hizo bajeti za USA hazitaisaidia kitu Ukraine,zaidi zitapelekea kupoteza vijana wa kiukraine TU.