Rais na kiongozi Bora kabisa katika zama hizi.
Amezifanya nchi dhaifu na nyonge kabisa Sasa hivi zijitambue na ziwe na sauti.
Kazifanya nchi dhaifu kabisa Sasa hivi zijione kua nazo Zina haki katika sayari hii.
Kazifanya nchi dhaifu kabisa Sasa ziweze kuwaambia wale waonevu kua Sasa basi,haya tunayataka na haya hatuyataki bila kupindisha maneno.
Kazifanya nchi zilizofungwa kutoka vifungoni,Iran,Korea kaskazi na Syria.
Kavunja minyororo na kalirudisha ndani ya chupa jini Dola/USD.
Kazipa uhuru wao nchi zilizokua mateka (Saudi Arabia).
Kaamua kupambana nao kwa ajili ya uhuru wa Dunia,Dunia Sasa inaenda kua huru.
Kayavua nguvu magenge yaliyokua yanaitshia na kuwapora wanyonge wa Dunia ( NATO,G7,west).
Kazifanya Dunia imjue mbabe wa kweli na asie mwonevu(Russia).
Kaifanya Dunia ijue kua kumbe wale wababe nao Wana mbabe wao na kua kumbe walikua wanaonea vijidagaa TU.
Kaifanya Dunia ijue kumbe wababe wanaweza kuonywa na kuonyeka.
Kaifanya Dunia Sasa imejua kumbe na wababe nao ni tegemezi TU,na pia wanaweza kuwekewa vikwazo na vikawaathiri pakubwa.
Huyu kiongozi mkubwa wa zama hizi amefanya mengi yajulikane ,nikiorodhesha siwezi kumaliza Leo.
Kama nasema uongo hebu angalia msululu wa nchi zinazotaka kujiunga na BRICS,hizo ni nchi zenye confidence ,je ni nchi ngapi zinazoogopa kujitokeza hadharani lkn zinatamani kujiunga?
Unajua ni kwa Nini nchi zinakimbilia Brics?na hasa zile zilikua watumwa wa USA ?mf Soud arabia.ninkwa sababu Zi uhakika na usalama wao.
Kwa kumalizia Vladimir Putin anauangusha ufalme wa sio TU USA Bali wa west.
Kwa kawaida utawala uliojichimbia chini kwa miongo mingi hauanguki ghalfa au mara moja.lakini ufalme huu umeshaanza kuanguka.