Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Mda umefika wa kufanya marekebisho kwenye vitabu vyetu kuwa wanafunzi wajue toka mda huu super power Ni Russia, Futeni habari za NATO, G7 wekeni BRICS,hakuna Cha US Wala Eu,Wala Pentagon mwamba huyu hapa.
FvN89zjWYAANbZ9.jpg
 
Mkuu najua kwamba wengi wanaamini unachosema - ila hakuna msingi. tafadhali nionyeshe mapatano au mkataba unaodai ulikuwepo. hakuna.
Unachoweza kuonyesha ni mawazo ya wanasiasa kadhaa walioona NATO isipokee nchi ambazo zilikuwa nusu koloni za Urusi kama vile Poland, Baltiki na kadhalika.
Lakini hakuna mapatano wala mkataba.
Kinyume kuna mkataba rasmi wa Helsiniki ambako USSR ilikubali kila nchi ya Ulaya ina haki ya kushirikiana na nchi nyingine.
Kuna pia mkataba wa Minsk ambako Urusi ilitambua mipaka ya Ukraine (pamoja na Donbass na Krimea) na kuahidi itatetea mipaka hiyo.
Ni nani sasa aliyevunja mkataba?

Halafu unaamini kuna sababu gani kwamba nchi za Ulaya zimeacha kushirikiana na Urusi kiuchumi tangu uvamizi za 2014 na 2022???? Ingawa Urusi ilikuwa chanzo cha nishati nafuu na soko kwa makampuni yao??

Kwa nini nchi za Baltiki, Poland, Chek na Slovakia waliombaomba wapokelewe NATO baada ya kuwa chini ya Urusi kwa miaka mingi?? (na hakuna aliyewalazimisha hata kidogo kuleta maombi ya kujiunga na NATO!)
Mkataba unaonyeshwa kwa watu wenye akili tu, wewe na Lusinde mna utofauti gani??
 
Usilete ngonjera mkuu...humu watu wanajua kwa nini hao jamaa wanatwangana.Hakuna asiyejua janjajanja ya USA....Hakuna asiyejua kuwa kikwazo kwa total control ya ulimwengu huu kwa USA ni Russia...Na hata uki-refer wanasiasa wa USA hata huyu Biden, alisema wazi changamoto zitakazotokea baada ya USA kujaribu kuwavuta Ukraine NATO
Hakuna asiyejua kuwa 2014 palikua na coup Ukraine..kupinduliwa kwa serikali iliyokuwa fruendly kwa Moscow na ikaingia serikali iliyo ant-Russia, mambo hayo ndo ya chanzo cha mzozo wa sasa...
Inajulikana tu pia kuwa coup ya Ukraine (2014) ilikuwa ni practice kwa ajili ya kitakachotokea Urusi...ikapelekea kuingizwa kwa sheria ya Foreign agent law ( Russia)...ambayo hata USA wanayo kwa miaka mingi...

Najua utaongea kwa ushabiki na kutumia mgongo wa kila nchi kuwa na haki ya kujiamulia mambo yake lkn ukweli ni kuwa hakuna nchi yoyote duniani itakubali nchi jirani yake ahatarishe usalama wake kisa kuna uhuru wa kujiamulia mambo yake....Wanasema haki yako inaishia pale, inapoanza kuwa kitisho au kikazwao kwa mwenzako...

Nyerere aliinyima Zanzibar kuwa nchi huru kwa sababu ya security reasons pia-Muungano ukalazimishwa..Karume akasaini..Zanzibar ikapigwa pin...na viongozi wa Zanzibar waliokuwa wanajifanya kuwa vocal kwenye masuala hayo ( hata wa CCM)...hawajawahi kuvumiliwa...

USA hawezi kukubali wapinzani wake wakae CUBA au Mexico pale, lazima pachimbike..

Haki inakuwa haki kama haihatarishi usalama wa mwenzako.....

Mkeo/Mmeo akianza tabia ya kulala na kisu chini ya mto- rationally lazima akili izunguke kujua sababu....kama haziekeweki lazima ujipange..

Kwa hali ya kawaida UKRAINE na URUSI wanakila sababu ya kuwa mataifa marafiki...
1.Wanampaka mkubwa sana
2.Ni slavic
3.Wanauhusiano mkubwa sana wa kitamaduni
4.Kuna watu wenye asili ya Urusi wengi sana Ukraine
5.Wanashare familia:Mtu yuko Urusi-babu yaje yuko Ukraine
6.Walikuwa na uchumi unaingiliana sana-viwanda-chain production inaanzia Ukraine inaishia Urusi

Zelensky mwenyewe...mpaka anakuwa Rais alikua anaongea Kirusi pekeee....Kiukraine kaanza kujifunza ofisini..

Zelensky kafanya kazi za commedy Moscow na huko ndiko alikochuma pesa zake za kwanza...

Hivyo hawa watu wanaukaribu mkubwa kuliko ilivyopaswa kuwa...hapo sasa na US kaingia kaanza kuwavuruga....Ukraine kaanza kupandikizwa chuki vurugu likaanza...

Na Urusi haiwezi kukubali Ukraine ikaenda West na kuwa tishio kwake....sababu

1.Ina-pride: Putin akishindwa:Atakayeingia lazima aanzishe vita tena....(Na Putin kasema kushindwa hakupo..labda WW3)

2.Inauwezo wa kuresist pressure za West

3.Inauwezo wa kijeshi kujitetea na kusababisha maumivu makubwa west..

Tuendelee kuangalia huu mchuano...lkn kwa maoni yangu Ukraine kayakoroga na hatoboi
2.
Shukrani mkuu kwa bandiko zuri
 
Nikuulize swali rahisi mkuu, hivi taifa moja linaweza kuwazidi propaganda mataifa 30+ yenye chuki dhidi ya taifa hilo moja?

Kwa mfano... Yaani mtoto wa mchepuko wako ambae sio wako wa kumzaa anaweza kuizidi mirathi familia ya baba yako mzazi?
Acheni hizo basi...
Mkuu propaganda ni swali pana sana . . . Ila sijui umepata wapi habari kuna mataifa 30 yenye chuki dhidi ya Urusi?? Ukiangalia majadiliano mfano katika Ulaya, unapata kila kitu.
Wale walio wakali zaidi dhidi ya urusi ni nchi hizo zilizolazimishwa kuwa koloni au nusukoloni za Urusi - kama vile nchi za Baltiki zilizovamiwa na Urusi miaka 300 iliyopita, halafu tena 1940 (mapatano kati ya Hitler na USSR) halafu tena 1945 . . . . . .
kama vile Poland iliyogawiwa na Urusi pamoja na Prussia halafu kuvamiwa tena 1815, na tena 1920 ilipopata uhuru wake, na tena 1939 (pamoja na Hitler), na tena 1945 .....
Katika nchi nyingine kama vile Ujerumani na Italia hadi leo kuna hisia za urafiki kwa Urusi ila wako pamoja kusema "haiwezekani kubadilisha mipaka kwa nguvu ya kijeshi".......
Kwa nini Wajerumani waliendelea kujenga bomba la Nordstream hadi 2022? Na kuwekeza pesa nyingi sana Urusi??
Kwa nini waliacha sasa ? Tafakari, mkuu...
 
Kwa ufupi unamaanisha ukraine ni shamba darasa.😁😁
Asante kwa mzaha. Labda jaribu sasa maswli yangu:

Ni nani aliyevunja mkataba?

Halafu unaamini kuna sababu gani kwamba nchi za Ulaya zimeacha kushirikiana na Urusi kiuchumi tangu uvamizi za 2014 na 2022???? Ingawa Urusi ilikuwa chanzo cha nishati nafuu na soko kwa makampuni yao??

Kwa nini nchi za Baltiki, Poland, Chek na Slovakia waliombaomba wapokelewe NATO baada ya kuwa chini ya Urusi kwa miaka mingi?? (na hakuna aliyewalazimisha hata kidogo kuleta maombi ya kujiunga na NATO!)
 
Umeshawahi kujiuliza kwanini after cold war,over 50% ya wanachama wapya wengi ni from Eastern Europe??

USA na NATO wanaweka nguvu kubwa kupata wanachama kutoka hilo eneo??
USA ni nchi kutoka Bara la America ,do you think why kwenye Bara la America hakuna mwanachama wa NATO isipokuwa USA?
Mkuu kwanza uniruhusu nikuelimishe huko bara la Amerika Kaskazini kuna wanachama 2 za NATO ambao ni Marekani na Kanada.
Pili ndiyo, nimewahi kujiuliza kwa nini after cold war nchi za Ulaya Mashariki zimejiunga na NATO.
Sababu yake ni kwanza kabisa maarifa ya nchi hizo chini ya utawala wa kikoloni wa Urusi. Angalia nchi za Baltiki (Estonia, lithuania, Latvia) zilizovamiwa na Urusi kwanza miaka 300 iliyopita na kuwa koloni zake, halafu baada ya kupata uhuru mwaka 1919 ziivamiwa tena mwaka 1940, (na tangu 1945 kurudishwa hali ya "jamhuri za USSR" = makoloni) . . .
Nchi hizo ziliombaomba kujiunga na NATO ili zijisikie salama

vivyo hivyo Poland iliyomezwa na Urusi katika historia yake, kushambuliwa tena ilipopata uhuru mnamo 1919/20, kuvamiwa tena na Urusi mwaka 1939 (kwa kushirikiana na Hitler) na kulazimishwa kupokea serikali y akikoloni baada ya 1945 . . . . Nchi nyingine iliyoombaomba kujiunga na NATO.

Je unashangaa kwa nini nchi hizi walitaka kujiunga na NATO?
Au Chek Republic: mara ya mwisho walivamiwa na Urusi / USSR kwenye mwaka 1968 . . .

Unashangaa kwa nini walitaka kujiunga na NATO?
 
US in secret talks with Iran - CNN

The US administration has secretly resumed indirect talks with Iran to contain its nuclear program and release American prisoners, CNN writes, citing sources.
Negotiations began last December in New York and have continued in Oman ever since.

According to US officials, the US goal is to achieve a "political truce."

In return, Tehran demands to unfreeze billions of dollars of Iranian assets abroad.
 
The share of the US dollar in global foreign exchange reserves has fallen from 73% to 58% over the past two decades - Bloomberg

Global de-dollarization is gaining momentum. Especially in the last two years.

The US is still struggling to contain this process, saving the dollar only at the expense of high interest rates, reports Bloomberg.
 
Lada Niva in the hunt for "Leopards"
As part of the Russian army , shock maneuver "hunter" anti-tank teams equipped with modified Lada Niva SUVs armed with portable missile systems 9K111-1M "Konkurs-M" were formed. reconnaissance unmanned quadcopters and connected by high-quality means of communication.
IMG_1394.jpg

IMG_1395.jpg
 
Lada Niva in the hunt for "Leopards"
As part of the Russian army , shock maneuver "hunter" anti-tank teams equipped with modified Lada Niva SUVs armed with portable missile systems 9K111-1M "Konkurs-M" were formed. reconnaissance unmanned quadcopters and connected by high-quality means of communication.
View attachment 2660214
View attachment 2660215

IMG_1396.jpg
 
Back
Top Bottom