Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

1. GDP haina maamuzi kwenye kushika uchumi wa dunia. Nchi zote zinazoongoza GDP ni zenye watu wachache hata hii Tanzania mtembeza bakuli yenye watu milioni 60 ukifukuza watu wote maskini ukabakiza wenye hela milioni moja tu utakuta Tanzania iko among nchi zenye GDP kubwa na hapo haina maamuzi yoyote kiuchumi duniani. Nchi zote zenye GDP ndogo ndio zile zenye watu wengi sana kina India na China.

2. Marekani kuongoza katika matumizi ya mafuta na nishati kwa ujumla ni ishara ya kuwa na uchumi wa viwanda. Nchi yenye uchumi mkubwa hutumia nishati kubwa sana ya ndani na nje, Russia anahitaji nishati kidogo kwa kuwa uzalishaji ni mdogo.

Russia nchi kubwa ila population ndogo, maisha ya kawaida. Unaweza nitajia Mmarekani gani amehamia Russia? Sasa Marekani kuna Warusi kibao kina Sergey Brin co-founder wa Google. Uliwahi sikia billionaire wa Uingereza anaenda kuishi Urusi, sasa London pale kuna hadi mtaa ni oligarchies Warusi kibao. Hata wewe hapo ukute unatamani kwenda Marekani au Western Europe kuliko Urusi

3. Kuwa world manufacturing hub hakukufanyi uongoze uchumi wa dunia. Huawei wakati inawekewa vikwazo ilikuwa inakuwa ya kwanza au ya pili kwenye uuzaji wa units nyingi za simu duniani. Leo ya ngapi? Hata top 10 haipo. Huawei ilizalisha kuliko kampuni yoyote ya Marekani ila teknolojia zote za uzalishaji wa simu karibia zinaanzia kwa Mmarekani. Kama uzalishaji unakufanya uongoze Huawei isingeshuka uzalishaji zaidi ya 80% tangu ipigwe vikwazo 2019. Watu kama nyinyi mlikuwa mnajifariji leo hii hata mkipewa latest Huawei mtalazimika muwe na nyingine pia.

India imefanya outsourcing ya technology na wanaenda uko kwa sababu kuna cheap labour wakutumikishwa bila gharama kubwa. Wafanyakazi wa Marekani na Ulaya wanalindwa na sheria nyingi zinazofanya gharama za uzalishaji ziwe kubwa. Hata China ilianza hivyo ingawa inatoka uko sasa. Ukichukua S&P 500 unakutana na makampuni 500 ya Marekani yaliyowekeza dunia nzima na ukiyalinganisha na hizo India, China na Russia utakuta hawakaribii hapo. Makampuni ya Marekani yameajiri dunia nzima, yanamiliki patents na yanazalisha dunia nzima wewe ukija unaangalia nchi zinazozalisha kwa uwekezaji wa nje. Mbona mojawapo ya sababu ya wazungu kutafuta makoloni Afrika ni kupata cheap labour? Bila mzungu kuja kutumikisha watu Tanganyika isingeongoza kwenye katani, wala Ivory Cost na Ghana zingeongoza kwenye cocoa
Kwamba GDP haina maamuzi kwenye kushika Uchumi wa Dunia? Hapa ndipo unaboronga.

Nchi gani yenye kushika Uchumi wa Dunia bila kuwa na GDP kubwa? Nchi gani ina GDP kubwa na haijashika uchumi wa Dunia?

Huyo Russia na South Korea nani ana share kubwa kwenye uchumi wa Dunia?
 
Neno " ant" kwenye maandishi ya lugha ya Kiarabu hakuna Ila kwenye matamshi lipo.
Maneno "anta" you (male) na "anti" you (female) yanapokuwa mwisho wa sentensi au popote ukiamua kuweka kitua hapo, hutamkwa hivyo yaani " ANT"
Hujuwi Kiarabu, wacha porojo. Nikusahihishe halafu ujidai wewe ndio Mwalim, huu ujuha mwengine ni wa ziada.
 
Halafu Mkuu yaani wewe huwa wanichukuli poa sana aisee!

Yaani huwa wajitahidi kunipiga kamba si mchezo. Jana umenipiga kamba nyingi, nikazichomoa. Leo ukaona kamba hazitoshi, umeamua kuja na minyororo kunifunga.

Hiyo stori kuwa leo hii '1 USD = 420,000+ Venezuela bolivar (VES)' [emoji15][emoji15][emoji15], umeiokota wapi mkuu?!


Mie nijuavyo ni kuwa leo hii 1 USD = 4.22 Venezuela bolivar

Wakati 1 USD= 2,314.42 TZS (Tanzania hatuna vikwazo vya Marekani)

Mkuu T14 Armata jitahidi uwe makini ktk kuchukua taarifa zako unazoziweka hapa jamvini...ingawa mwenyewe wajiona uko makini mnooo [emoji38][emoji1][emoji23][emoji1787][emoji2960]

View attachment 2149936

View attachment 2149937
Bloomberg wanasema hivi:
"...It’s another maneuver aimed at propping-up the national currency, even though President Nicolas Maduro’s government is permitting the use of the U.S. dollar as a way to cope with runaway inflation and shortages. The government has implemented two other currency changes since 2008, dropping eight zeroes. Hyperinflation, among the highest in the world, has slowed to 2,146% per year from more than 300,000% in 2019, according to Bloomberg’s Cafe Con Leche index.

Under Friday’s change, the largest former banknote, for 1 million bolivars -- worth about $0.23 --will be replaced by a 1-bolivar coin. One dollar will fetch around 4.2 bolivars instead of 4.2 million bolivars at the official exchange rate.

“This is useless. Prices will continue to rise and, in a few months, the new bills will be useless,” said Leida Leon, a 37-year-old cleaning worker at a Caracas school...."

Hapo nimesema Bolivar na wewe umesema Sovereign Bolivar kwahiyo NIMEKOSEA kwa kuwa hiyo Sovereign Bolivar ndio inatumika. Ila hawa Bolivia waliupiga mwingi kufuta zero 8 tangu wapigwe vikwazo. Mwaka jana mwishoni hapo ndio walifuta zero 8, huu ujanja kina Zimbabwe waliukosa. Sikuwa sahihi kutumia exchange rate ya zamani. Picha ni banknote ya milioni moja iliyofutwa ikiwa na banknote ya 10 na ya 5
1200x-1.jpg
 
Majeshi ya Russia yakitumia ndege za kivita yamefanya mashambulizi makali ktk mji wa Zhytomyr unaopakana na Kyiv, BBC imeripoti.

SmartSelect_20220314-130316_Chrome.jpg
 
Kila mtu anakuja na hoja kutoka source yake, na mwingine anakuja ku disprove hiyo source kupitia source yake

Sielewi yupi ni yupi, yupi mkweli yupi muongo

Yani kiukweli mnazidi kuniacha highway kwenye hili swala
Huku ni tofauti kidogo na kule kwa mechi za simba. Huku ni suala la utiifu kwa taifa. Utakutana na wazalendo kamili wa mataifa husika.
 
Kwamba GDP haina maamuzi kwenye kushika Uchumi wa Dunia? Hapa ndipo unaboronga.

Nchi gani yenye kushika Uchumi wa Dunia bila kuwa na GDP kubwa? Nchi gani ina GDP kubwa na haijashika uchumi wa Dunia?

Huyo Russia na South Korea nani ana share kubwa kwenye uchumi wa Dunia?
Hapo nimesema GDP per capita kama aliyosema yeye niliyemquote. GDP ni mada kubwa yenye vipengele vingi ukiingia mjadala wake ujue walioanza wamesema nini kuhusu GDP. Hatujasema nominal, tumesema per capita ambayo top ya nchi zenye per capita kubwa humo kuna nchi ambazo hazina maamuzi yoyote makubwa ya kiuchumi duniani. Kuanzia #2 mpaka #5 kuna Macao, Luxembourg, Singapore na Brunei hawa watagomea nini duniani? Alafu Marekani kakaa #13 na hao top 10 wote hawawezi mfanya chochote kiuchumi
IMG_20220314_130856.jpg
 
Mkuu kwani tatizo liko wapi kwa Urusi kuomba silaha anazo ona zinamfaa kwenye vita tena kutoka kwa mshirika wake wa kijeshi ,kiuchumi na kisiasa?

Kwann kila anacho kifanya Russia kinaonekana ni kitu cha ajabu wakati ni kitu cha kawaida kwa washirika kusaidiana vitani hata Marekani huwa anafanya hivyo?


Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
Hakuna ajabu kwenye Russia kuomba silaha, kuna ajabu pale watu wanapokataa kwamba Russia hawezi omba silaha
 
Waziri wa Ulinzi wa Ukraine amekiri miundo mbinu mingi ya Kijeshi imelipuliwa wanajeshi 1200 Drone 180, Vifaru 1000, majukwaa ya kurushia makombora 160, ndege 160 na ukiona mpaka waziri wa Ulinzi wa Ukraine anakiri ujue muda so mrefu atatangaza kusalimu amri kwa Wasoviet
Kiswahili kigumu kumbe, majukwaa ya kurushia makombora sijajua ni nini. Labda ni artillery pieces, howitzers au rocket launchers. Anayejua aniambie
 
Hatujasema nominal, tumesema per capita ambayo top ya nchi zenye per capita kubwa humo kuna nchi ambazo hazina maamuzi yoyote makubwa ya kiuchumi duniani. Kuanzia #2 mpaka #5 kuna Macao, Luxembourg, Singapore na Brunei hawa watagomea nini duniani? Alafu Marekani kakaa #13 na hao top 10 wote hawawezi mfanya chochote kiuchumiView attachment 2149981

Hivi unakielewa ata unachokizungumza vizuri????

Hivi ata tofauti ya GDP capita na GDP nominal inaijua?????

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Hichi kirefu cha PPP kwe jedwali ya kwanza unakijua????

Ukiambia GDP per Capita (Nominal) na GDP per Capita (PPP) unaelewa????

Em tupunguzeni ujuaji jaman sio lazima tujue kila kitu [emoji847][emoji847][emoji847][emoji847] hakuna tuzo apa JF...
 
Back
Top Bottom