Katika historia ya USA toka kuundwa kwao wamejikuta wamepanda mtumbwi wa kibwengo Kwa kuanzisha Vita hapo Ukraine
NATO imekutana na kile ambacho ndiyo sababu ya kuundwa yaani umoja wa kijeshi ulioundwa Kwa lengo la kuidhibiti urusi wakiongozwa na kaka Yao marekani
Kwenye maeneo kama Yugoslavia, Afghanistan, Libya, Iraq n.k walikuwa kama wanafanya mazoezi na kupata uzoefu wa kuja kushambulia urusi, baada ya kuona wameiva na wapo tayari ndiyo wakaandaa hii mbungi ya Ukraine, tahamaki wameingia Choo cha kiume maana wao asilimia kubwa ni mashoga [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Sasa sasa hivi NATO na USA wamejikuta wapi katikati ya bahari kwenye kina kirefu halafu hawana namna mbadala wa kutoka hapo walipo
Mrusi anaendelea kutoa dozi ya kipigo na wala haonekani kama atakuja kupunguza zaidi sanasana kila siku anaongeza mapigo na kibaya zaidi viwanda vyake vinazalisha silaha kupita matumizi, hapa ndipo west wanachanganyikiwa [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Ulaya yote imeyumba kiuchumi, dollar inapoteza udhibiti wake duniani, mchina anakuja Kwa Kasi ya hypersonic kwenye maendeleo na kiuchumi duniani kutokana na nishati ya bei nafuu, Saudia kamwambia mmarekani wazi akifanya ujinga basi atamyumbisha kiuchumi (hapa mmarekani kawa mpole maana anajua nini kitafata)
Juzi Kati Bunge la marekani limeongeza kiwango cha ukomo wa kukopa Kwa lugha nyingine Bunge wameruhusu kuchapisha dollar zaidi [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] swali langu watachapisha Kwa kiasi gani????, Maana hali haitegemei kutengemaa Leo wala kesho, na mrusi anapigana mdogo mdogo Hana haraka maana anataka kuona Vita inachukua muda mrefu lakini uchumi wa west unaweza kuhimili maumivu Kwa muda mrefu?????, Na mrusi anajua mpaka sasa wako kwenye dakika za mwisho za uvumilivu wao, na ndiyo maana mrusi kuna wakati anasema nikimalizana na Ukraine naingia Poland hii kauli haitoki Kwa bahati mbaya au ni kitisho, Ila wanasema hivyo ili ulaya useme kumbe tukishindwa hapa mrusi atatuvamia Kwa hiyo inabidi tupigane kufa na kupona ili tushinde, lakini kipindi wanapigana maana yake muda unasogea uchumi unaanguka pesa nyingi za walipakodi wanakuwa ni kama wamezichoma Moto maana hakuna wakuja kuwalipa, na hata wakija kushtuka uwezo wa kupigana na urusi hawana na kama watashindwa na kukubali matokeo basi haya yatatokea
1) NATO kuvunjika rasmi Kwa kuwa itaonekana haina umuhimu zaidi ya kutumia pesa za walipa Kodi, maana Yule adui ambaye ndiyo msingi wa kuanzishwa kwa NATO kawapiga na kuharibu uchumi wao kabisa
2)USA na EU kuanguka duniani kiushawishi, kiuchumi na kijeshi, hapa ndipo jumuiya ya ulaya itaona kila rangi, walizoea wizi ili watajirike hiyo mirija inaenda kukatwa rasmi
3)vikundi vingi vya kigaidi kupungua duniani, nchi nyingi kuanza kujitambua, mikataba mingi ya kilaghai kufutwa
Ila kuna kitu nataka nione mwisho wake
USA anachapisha pesa halafu OPEC wanaenda kupunguza uzalishaji wa mafuta jumlisha huu mfumuko wa bei pamoja na mdororo wa uchumi wa ulaya
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Naenda kushuhudia ulaya ikipiga magoti mbele ya urusi tena Kwa aibu ya dunia