Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Nimejaribu kumfatilia hata T14 Armata nikagundua kua hata yeye Ni msomaji wa silaha mitandaonitu. Hajui nguvu,mapigo wala shabaha ya silaha anakopi Wikipedia analeta huku. Hapo congoni FIB ilikiwasha kwa pisi12 za single propela bM 21 kwa masaa manne chiniya Lutni general mstaafu wakatihuo akiwa brigadier general Frank Mwakibolwa.

Zilipigwa kuanzia saa 6 usiku saa 12 Lakers battalion na special unit ya 92/Marine Commandos wakaomba yasitishwe mapigo watu wamefika eneo la kumtoa mwali. Maana wakati vyombo vikitumwa watu walikua wakisogelea kambi kuu na bohali kuu la M23. Wazee wakakuta hakuna hata kazi ya kufanya hivyo kukusanya maiti na silaha na kumfahamisha mkuu wa jeshi la UN wakatihuo yule mbrazil watu walibroo. Sasa kwa zana alizoingia nazo mrusi zinauwezo wa kupiga Ukraine na bado kuzisogeza hata huko lviv ili ziwasubirie na wanato Kama wataipenda shoo.

Achaneni kbsa na mrusi hata pafomansi ya K52 sio ya kitoto maana imeonesha maajabu ambayo yalioneshwa na F18 kipindi Cha Libya ya gadafi. Attack Helicopter kwa Aircraft jet fighter. Aloo Russia kiboko wanajua asee usifanye mzaa
Ila wewe bwana nimecheka sana kwa kweli unachekesha mno sina neno la kuongeza apa ila ni unachekesha kaka
 
Ukraine imetelekeza hii launcher ya S-300. Ni hasara kubwaView attachment 2150161

Miaka ya hivi karibuni issue za defense system za Mrusi zili trend sana hasa S 400 na S 300. Sasa huu mgogoro wa Ukraine naona UNAZIUMBUA SANA kumbe zinapigika kirahisi hivyo. Tena kwa ndege vita za kawaida tu. Je zikikutana na F 22 Raptor au F 35 stealth za Mmarekani sizitakuwa majivu tu
 
Marekani wameshaanza kumpiga mkwala Mchina wa kuangushiwa rungu zito la vikwazo endapo atatoa msaada kwa Mrusi. Next wiki mawaziri wa mambo ya nje wa US na China wanakutana Italy na moja ya agenda ni hilo. Lakini Mchina alivyo mjanja mjanja itakuwa ngumu kumsaidia Mrusi bila kificho, asingependa kuutia uchumi wake majaribuni.
 
Ulitarajia wakubali wakati ni mpango wa Siri,Urusi kaomba kisirisiri kwa hiyo lazima mchina amtunzie Siri.

Hahaha hivi unajua hiyo habari katoa nani?? Kama hujui ni Financial Times... na ujiulize ni gazeti lenye mlengo gani... kama hujui na hilo ni gazeti la ki- liberali ambalo linawakilisha taarifa za magharibi. Na mpaka tulipofikia Taarifa za vyombo vya magharibi zinaaminika?? Ukijibu utaacha ushabiki wa kinyumbu.
 
Na hii huthibitisha wazi kwamba Mrusi ana goodwill. Mchawi Mmarekani. Imagine anapump silaha na wanajeshi waende Ukraine, but anadhani siyo haki kwa Putin kufanya hivyo! Madness!

Wanaomsapoti Mmarekani wakapimwe (...)!!! ^You know the thing^ ~ Joe Biden.
Urusi yupo wima mwenyewe akiwa front kuwakabili Ukraine wanaosaidiwa na West. Marafiki wa Urusi na nchi zisizo za kibepari hawajatoka wazi kusimama na Urusi wakati wenzao wametoka wazi wanaweka vikwazo na kutoa silaha. Kwangu mimi naona kuna woga ambao umesababisha. Najua wapenzi wa Urusi mnaweza nishambulia ila na nyinyi mjiulize, Why?
 
Wawakilishi wa Urusi na Ukraine wanakutana muda mfupi ujao katika juhudi za kumaliza mapigano ya zaidi ya wiki mbili huko Ukraine.

Wakati juhudi hizo zikiendelea, ripoti zinaendela kuonyesha mashambulizi yakiendelea katika maeneo mbalimbali ya Ukraine.

Inaripotiwa kuwa watu wawili wamefariki na wengine 12 kujeruhiwa katika shambulio la anga la Urusi katika jengo la makazi katika mji mkuu wa Ukraine Kyiv.

Mapema Ukraine iliripoti kutungua ndege nne za kijeshi za Urusi katika saa 24 zilizopita.

Katika tukio lingine takriban watu 35 waliuawa katika shambulio lililofanywa katika kambi ya mafunzo ya Yavoriv, karibu kilomita 20 kutoka mpaka na Poland, ambaye ni nchi mwanachama wa muungano wa kijeshi wa magharibi, Nato.

"Kwa hivyo bila shaka Warusi walijua kile walichokuwa wakipiga na walitaka kutishia Nato... Walitaka kutuma ujumbe unaotishia Nato," alisema Naibu waziri wa mambo ya nje wa Poland Marcin Przydacz ameiambia BBC.
 
Hizo laptops haziko Russia. Mnato wa Marekani alizipiga sanki (sanctions). Hiyo ni ya mgomvi Joe Biden. Naifahamu vizuri.
Ziko, lakini zinategemea vipuli vya nje.
1647264441066.png
 
Aisee sasa alianzaje kutoa ule mkwara wa kusema nchi yeyote itakayoingilia kati itapata pigo la kihistoria kama hata magazine hana za kutosha

Ukraine yeye anasema mtu yeyote anayetaka kuisupport ukraine aje atapewa silaha, means kwamba ukraine bado wana silaha za kutosha ku handle hii vita

Ila mrusi kama kweli haya mambo ni kweli na sio propaganda ni bora asingeingia kwenye vita ili kuitunza heshima yake na CV ya nchi ambayo ni hatari kijeshi na inayoongoza kwa silaha nzito za maangamizi
Amini kwamba NATO wanaijua nguvu ya Russia kuliko sisi wasoma habari mitandaoni ndio maana Russia alisema atakayeingilia atapata pigo la kihistoria na mpaka sasa hakuna aliyeingilia.

Unafikiri kwa nini hawaingilii, wanasema Russia kaishiwa silaha mpaka anaomba china huu ndio wakati mzuri wa kumuingilia mbona hawajaribu?
 
Jamaa ChenChen noumer urusi mwenyewe hana hamu nao hao maana walimpa kichapo heavy na vita alishindwa kama alivyoshindwa afghanstan
mnataka kusema Russia kwa sasa analazimika kuomba msaada kutoka "ChenChen" ili kumaliza hii special operation 🙂
 
Back
Top Bottom