Kama pro-Russia nilichojifunza kwa matukio ya leo ni kua inawezekana kabisa kizazi chetu kisishuhudie kamwe wema ukiushinda ubaya.
Chukua mifano ya akina Che Guevara, Fidel Castro, Gaddafi, Sankara, Hugo Chavez, JPM, Trump na sasa Putin na Russia yake kwenye hii vita ya Ukraine.
Imekuaje intelijensia ya Urusi imeshindwa kabisa kujua mipango ya Prigozhin na kuizima au ilikuaje wakaruhusiwa kuwa na nguvu mpaka ya kuweza kutishia kufanya mapinduzi?
Mbona mfano Marekani wanampa Zelensky misaada ya kila aina na bado hawaachi kumdukua kuhakikisha hawezi kufanya kitu nje ya maelekezo yao, na akizingua wanamla kichwa asubuhi tu, Urusi wanashindwaje kwa huyo Prigozhin?
Mbona mutiny za aina hii sijawahi kuzisikia Marekani tokea nimepata akili?
Putin majuzi ametangaza wameshambulia decision-making centers za Ukraine, pro-Russia wengi wakasema Zaluzhny na Budanov waliuliwa kwenye hizo strikes, kama siku tatu nyuma nimeona video zao ni wazima kabisa hawana dalili kwamba wamewahi hata kuumwa siku kadhaa nyuma.
Nitaendelea kuwa pro-Russia kwasababu anasimama kwenye wema lakini from today I'll expect nothing kutoka kwao.
Sent from my SM-A135F using
JamiiForums mobile app