Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Ila wewe bwana nimecheka sana kwa kweli unachekesha mno sina neno la kuongeza apa ila ni unachekesha kaka
 
Ukraine imetelekeza hii launcher ya S-300. Ni hasara kubwaView attachment 2150161

Miaka ya hivi karibuni issue za defense system za Mrusi zili trend sana hasa S 400 na S 300. Sasa huu mgogoro wa Ukraine naona UNAZIUMBUA SANA kumbe zinapigika kirahisi hivyo. Tena kwa ndege vita za kawaida tu. Je zikikutana na F 22 Raptor au F 35 stealth za Mmarekani sizitakuwa majivu tu
 
Marekani wameshaanza kumpiga mkwala Mchina wa kuangushiwa rungu zito la vikwazo endapo atatoa msaada kwa Mrusi. Next wiki mawaziri wa mambo ya nje wa US na China wanakutana Italy na moja ya agenda ni hilo. Lakini Mchina alivyo mjanja mjanja itakuwa ngumu kumsaidia Mrusi bila kificho, asingependa kuutia uchumi wake majaribuni.
 
Ulitarajia wakubali wakati ni mpango wa Siri,Urusi kaomba kisirisiri kwa hiyo lazima mchina amtunzie Siri.

Hahaha hivi unajua hiyo habari katoa nani?? Kama hujui ni Financial Times... na ujiulize ni gazeti lenye mlengo gani... kama hujui na hilo ni gazeti la ki- liberali ambalo linawakilisha taarifa za magharibi. Na mpaka tulipofikia Taarifa za vyombo vya magharibi zinaaminika?? Ukijibu utaacha ushabiki wa kinyumbu.
 
Urusi yupo wima mwenyewe akiwa front kuwakabili Ukraine wanaosaidiwa na West. Marafiki wa Urusi na nchi zisizo za kibepari hawajatoka wazi kusimama na Urusi wakati wenzao wametoka wazi wanaweka vikwazo na kutoa silaha. Kwangu mimi naona kuna woga ambao umesababisha. Najua wapenzi wa Urusi mnaweza nishambulia ila na nyinyi mjiulize, Why?
 
Wawakilishi wa Urusi na Ukraine wanakutana muda mfupi ujao katika juhudi za kumaliza mapigano ya zaidi ya wiki mbili huko Ukraine.

Wakati juhudi hizo zikiendelea, ripoti zinaendela kuonyesha mashambulizi yakiendelea katika maeneo mbalimbali ya Ukraine.

Inaripotiwa kuwa watu wawili wamefariki na wengine 12 kujeruhiwa katika shambulio la anga la Urusi katika jengo la makazi katika mji mkuu wa Ukraine Kyiv.

Mapema Ukraine iliripoti kutungua ndege nne za kijeshi za Urusi katika saa 24 zilizopita.

Katika tukio lingine takriban watu 35 waliuawa katika shambulio lililofanywa katika kambi ya mafunzo ya Yavoriv, karibu kilomita 20 kutoka mpaka na Poland, ambaye ni nchi mwanachama wa muungano wa kijeshi wa magharibi, Nato.

"Kwa hivyo bila shaka Warusi walijua kile walichokuwa wakipiga na walitaka kutishia Nato... Walitaka kutuma ujumbe unaotishia Nato," alisema Naibu waziri wa mambo ya nje wa Poland Marcin Przydacz ameiambia BBC.
 
Amini kwamba NATO wanaijua nguvu ya Russia kuliko sisi wasoma habari mitandaoni ndio maana Russia alisema atakayeingilia atapata pigo la kihistoria na mpaka sasa hakuna aliyeingilia.

Unafikiri kwa nini hawaingilii, wanasema Russia kaishiwa silaha mpaka anaomba china huu ndio wakati mzuri wa kumuingilia mbona hawajaribu?
 
Jamaa ChenChen noumer urusi mwenyewe hana hamu nao hao maana walimpa kichapo heavy na vita alishindwa kama alivyoshindwa afghanstan
mnataka kusema Russia kwa sasa analazimika kuomba msaada kutoka "ChenChen" ili kumaliza hii special operation 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…