Ya MotoMoto
Waziri wa uchumi wa Ujerumani, Robert Habeck, leo ametoa msimamo wa Ujerumani juu ya vikwazo vya nishati za Russia (mafuta, gesi na makaa ya mawe).
Waziri huyo amesema Ujerumani haitofuata nyayo za Marekani na Uingereza kususia nishati za Russia (Ujerumani haitosusia nishati hizo). Akaongezea kuwa
kustopisha ghafla kunuunua mafuta, gesi na makaa ya mawe ya Russia kutaathiri vibaya zaidi uchumi na maisha ya wajerumani wote. Kutapelekea gharama za maisha kupanda zaidi, malaki ya wajerumani watapoteza kazi, watu watashindwa kuendesha magari yao kwenda kazini, wajerumani watashindwa kupasha joto majumba yao au kulipia bili za umeme.
Kwa wale waliofika Ulaya watakuwa wanaelewa sana umuhimu wa mfumo wa kupasha joto kwenye nchi za Ulaya. Ila kama hujafika huko wawezachukulia poa tu.
Chanzo ni 'The Wall Street Journal' (au hicho nacho ni cha Russia?!)
View attachment 2150295
View attachment 2150296
BERLIN—Germany reaffirmed its refusal to boycott Russian energy imports because the costs would be too high for the German economy. Economy Minister Robert Habeck said his country wouldn’t follow the U.S. and the U.K. in stopping imports of coal, oil and natural gas from Russia because of its heavy
www.wsj.com