Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Haya Makombora ya Islander c Armenia alipewa na Urusi ili aipige Azerbaijan lkn yalitunguliwa na air defenses za Israel.

Hiyo NI habari toka chombo cha habari cha Urusi, The Moscow Times.View attachment 2152218View attachment 2152219

Unajua Israel na Russia ni marafiki unajua hicho kitu? Hapo wenzako unakuta walikua wanatangaza biashara, kinachoendelea ukraine umeona sehem yyte ambayo israel ametoa shit kuhusu russia?? Amemshauri Zelenskyy afate anachotaka Russia.
 
S300 destroyed by Lora missile
 
Narudia tena usikariri kuwa S-300 ndio kila kitu, kwa maana yaweza kudungua kila aina ya silaha.

Ukitaka kujua waliozichambua na kuzigrade hizo air-defense systems, pitia hapa Top 10 Best Air Defence System In The World Β» AutoJournalism
 
Narudia tena usikariri kuwa S-300 ndio kila kitu, kwa maana yaweza kudungua kila aina ya silaha.

Ukitaka kujua waliozichambua na kuzigrade hizo air-defense systems, pitia hapa Top 10 Best Air Defence System In The World Β» AutoJournalism
Mkuu hao wanagrade hizo air defense system kutokana na specification zake za kwenye karatasi lakini hapa tunajadili uhalisia wa kwenye Vita ambazo zilihusika.

Mfano,ni kama vile kwenye paper unakuta Simu Camera yake ina 50MP na nyingine ina 12MP kutokana na hizo specifications hapo unaweza dhani hiyo yenye 50MP ndo ina camera nzuri lkn ukija kwenye uhalisia unakuta Ile yenye 12mp inapiga picha nzuri kushinda hiyo ya 50MP
 
Sasa kama wewe wajadili kitu ambacho hukijui wala hujui undani wake kwa kutumia tu fikira zako na propaganda unazomezeshwa nyakati za vita, endelea hivyo. Mie huwa nawaweka mbele wataalamu wa jambo husika ktk mijadala yangu.

Halafu hizo stori kuwa S-300 ya Armenia iliharibiwa na Azerbaijan ni madai tu ambayo hayana uthibitisho.




 
Sasa kama wewe wajadili kitu ambacho hukijui wala hujui undani wake kwa kutumia tu fikira zako na propaganda unazomezeshwa nyakati za vita, endelea hivyo. Mie huwa nawaweka mbele wataalamu wa jambo husika ktk mijadala yangu
Kwahiyo siku hizi mpaka vyombo vya habari vya Russia Kama Sputnik na The Moscow times zinamezesha watu propaganda kwamba silaha za Urusi sio bora zinalipuliwa na drones za west?! DUH!
 
Hii vita kwa Mrusi ni ndogo sana. Ikiwa kama tukifanya marejeo utagundua kuwa mambo mengi Russia ya Putin wanayafanya kwa mbinu. Mbinu ni tofauti na sera. Ndiyo maana kwa wamagharibi Putin kwao wanamuona hatabiriki.

Tukubali au tukatae, vyombo vya habari kwa sasa ni silaha kwa nchi husika. Kila mahali kuna propaganda. Vyombo vya magharibi navyo vina malengo yake na vyombo vya kwao vya habari vinasukuma propaganda zao. Tukija kwa Russia, China nako ni vivyo hivyo isipokuwa zinatofautiana uzito kulingana na maslahi ya nchi husika.

Russia na Marekani zimekuwa zikipambana kwenye nyanja za kijeshi na kijasusi kwa muda mrefu. Kwa miaka mingi, tena inawezekana ikazidi miaka yangu na miaka yako. Tujiulize: Pengine sisi tunafikiria hivi je, Russia kwao itakuwaje?

Russia kwake alitangaza kama special military operation. Ni kama sisi Tz kipindi cha JK tulivyokuwa na Operation dhidi ya M23 iliyoitwa Operation Chakaza nchini Kongo. Russia naye ametangaza operation yake kwa Ukraine ikiwa na lengo la denazify na demilitarize jeshi la Ukraine.

Ikiwa hilo ndilo alilolisema inabidi turudi na kufuatilia mwenendo wa mashambulizi anayoyafanya Russia nchini Ukraine. Je, yanaendana na alichokisema? Kama yanaendana yanaendana ni kwa asilimia ngapi amefanikiwa? Na ikiwa ni kinyume chake ni kwa asilimia ngapi amekwama? Haya nayaandika hivi kwasababu ndiyo taarifa aliyoitoa Putin kuhutubia Taifa lake.

Putin alinusurika kufanyiwa assassination mara 5 tangu aliposhika madaraka Russia. Alipokwenda kumtembelea Fidel Castro, Castro akamuuliza kwa nini unajua nipo hai mpaka hivi sasa? Castro akajibu mwenyewe akamwambia ni kwa sababu usalama wangu unaanzia na mimi kwanza. Hivyo Putin licha ya kuwaamini walinzi wake ila usalama wake unaanzia na yeye kwanza ijapokuwa anaiamini sana timu ya ulinzi wa kwake. Alishawahi kuwa director wa FSB ambao ni ya kijasusi pia.

Nikimwangalia Putin naona mission zake anazipeleka mbinu za kijasusi na inakuwa ngumu kutabiri. Tofauti na wamagharibi wanatumia sera katika utekelezaji wa mipango yao hivyo inakuwa ni rahisi kutambua mustakabali wa maamuzi watakayoyafanya.

Kingine: Wachangiaji wengi tunachangia hili suala ilihali hatujui nguvu ya silaha zinazotumika kwenye huu mtifuano. Wachangiaji wengi wanazungumzia kwa kile walichokifahamu kupitia google. Ufahamu wake wa silaha unabaki kinadharia. Ila ukija ulingoni hafahamu. Akitokea atakayewaelewesha wanakuwa bado wabishani. Hivyo kwenye hii idara inabidi tuiache hivyo kwa sababu ya kanuni na nidhamu ya wabongo; tuna ujuaji mwingi.
 
Kwahiyo siku hizi mpaka vyombo vya habari vya Russia Kama Sputnik na The Moscow times zinamezesha watu propaganda kwamba silaha za Urusi sio bora zinalipuliwa na drones za west?! DUH!
Hizo stori kuwa S-300 ya Armenia iliharibiwa na Azerbaijan ni madai tu ambayo hayana uthibitisho. Hata vyombo vya Russia viliporipoti viliripoti kama madai ya Azerbaijan: Majeshi ya Azerbaijan yanadai kuharibu mfumo wa ulinzi wa anga wa Armenia in Karabakh


 
Israel ina silaha za kisasa sana na mbinu nzuri. Ila systems za air defence zinategemeana, S-300 haiwezi tumika kuzuia helicopter au kadrone ka $40,000. Kuna systems zinatakiwa ziwepo nyingi kufanya tasks ndogo ndogo za medium na low range. Waasi wa Houthi walivyotumia drones za kiraia wakazifunga explosives kwa gundi za mafundi walizirusha angani zikapita air defence systems za Saudi Arabia zikaharibu miundombinu ya mafuta.

Ukisoma specifications za S-300 hakuna sehemu ambayo mtengenezaji alilenga ziharibu UAV au loitering munition. Hata Marekani anazo MIM Patriot kwa medium na long range ila anazo systems mpya kwa ajili ya drones, loitering munitions na swarn ya vyote. Radar, wavelengths, bands vinavyotumika kwa kazi hizo ni tofauti havikai pamoja
 
Ndo maana nashangaa huyo jamaa anayeshangaa na kuona Jambo la ajabu Kwa system ya S300 kuharibiwa na drones za Israeli.

Pia Azerbaijan ilitumia tactical ballistic missile Kama Lora kuharibu hizo S300 za Armenia.
 
Ndiyo maana pale UN China alimute kupiga kura,tabu uanzishe wewe halafu uanze kuwasumbua wengine.
Hivi mna akili sawasawa kweli?? Yaan nchi imekuwa magofu ila huku mlioko bunyokwa mnaona Urusi anapigwa [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] we unadhani vikao vya kila siku ni kwa ajili ya nini?? UKRAINE MIJI MINGI IMEBAKIA MAGOFU.
Wengi mna utoto sana, fuatilieni vita za URUSI anavyoifanya miji anayoishambulia, SYRIA, GEORGIA, CHECHEN nk.
Urusi akifika sehemu anatoa tahadhari ya Raia kisha anaharibu mji wote.
Tatizo hamjipi muda kufuatilia, hata BBC hao huwa wanaonesha namna gani URUSI wakiingia na namna wanaacha hiyo MIJI.
 
πŸ˜†πŸ˜„πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Mkuu hivi unaijua S-300 ilivyo? Au ndio waisikia sikia tu hata kuiona walau kwenye video hujaiona?

Je kwenye hiyo video uliyoweka ni wapi pameoneshwa S-300 inaharibiwa? (nitajie sekunde ya ngapi hadi ya ngapi)

Video hiyo yaonesha vifaru vikiharibiwa, lakini hakuna S-300 popote imeoneshwa, sembuse kuharibiwa.

Siku nyingine usiwe waishia kusoma title ya video, angalia vyema kilichomo kwenye video kujua kama kinasadifu title yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…