Ok ..thanks...masahihisho kidogo kwa andiko lako zuri...
USSR...Union of Soviets Socialists Republics.
Nchi zilizounda USSR:
Russia Federation
Ukraine
Kirgzistan
Turkmestan
Azberjan
Armenia
Georgia
Lithuania
Latvia
Estinia
Byerorussia
Kazhstan
Moldova
Uzhbestan
Tajikistan
Hizo ni Jamhuri 15
Poland haikuwa sehemu ya USSR
Poland ilikuwa ni miongoni mwa nchi zilizounda Warsaw Pact yaani umoja wa kujihami wa nchi za Ulaya Mashariki...
Nchi za Warsaw Pact zilikuwa ni USSR, East Germany, Poland, Czechoslovakia, Hungary na Bulgaria....
Rumania, Albania na Yugoslavia zilikuwa Ulaya Mashariki lakini hazikuwa kwenye Warsaw Pact..
Mkuu, ni kweli usemayo lakini pia rejea tena mikataba ya Versailles na Warsaw Pact.
Ni kweli Poland haikuwa ni sehemu ya USSR lakini ilikuwa inafuata sera za USSR na serikali yake kikomunisti ilikuwa ikiwasililiza USSR. Poland iliitwa satelite state na ilifuata mwelekeo wa kisovieti yaani soviet Sphere of interest.
Hii ilikuja baada ya majeshi ya kijerumani na kisovieti kuivamia Poland mwaka 1939 na USSR kuchukua sehemu ya mashariki ya Poland.
Mkataba wa Versailles ulitokana na kuisha kwa vita kuu ya kwanza ya Dunia na kuundwa kwa taifa la Poland maana wakati wa vita mahali hapo ndipo palitumika na majeshi ya Austria Hungary, himaya ya Ujerumani na himaya ya Russia.
Raia wengi wa Poland walikufa vitani (yapata wanajeshi 450,000) maana walikuwa wakitumika na pande zote hizo katika vita na ukichanganya na raia wa kawaida idadi ya vifo ni zaidi ya milioni 1.
Hivyo hapo kabla Poland ilikuwa ni taifa linojitegemea hadi lipoanza vita kuu ya pili lakini ikawa yafuata sera za kisovieti lakini bila kuwa sehemu kamili ya USSR.
Mkataba wa Warsaw ulilenga kuifanya Poland na nchi zingine ndogondogo kuwa upande wa Eastern Bloc kujilinda na upande wa Magharibi ulounda NATO na ilikuwa kuweka uwiano wa kinguvu za kijeshi yaani balance of power.
Matendo ya Warsaw Pact yalifanana na matendo ya NATO kuvamia nchi zingine na Czechoslovakia ilikuwa ni moja ya nchi zilovamiwa na Umoja ulounda Warsaw Pact na hiyo iliitwa operesheni Danube na nchi za Soviet, Poland, Bulgaria na Hungary ziliungana kuitandika Czechoslovakia.