Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Januari 06, 2022 ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ambayo alinukuliwa akisema ipo siku Nchi itauzwa kutokana na madeni

Amesema ameandika Barua ya kujizulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na uamuzi huo ni binafsi na hiari, na ameuchukua kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi, Serikali na Chama

#JamiiForums
View attachment 2070821
Maskini wakina Mdee na Esta Bulaya na covid wao😁😁😁
 
Mbunge wa Kongwa Ndugu Job ndugai amejiuzulu wadhifa wa uspika kwa barua aliyomwandikia Katibu wa bunge na kuomba taratibu nyingine za kumpata Spika ziendelee
Asiwe na hofu kuhusu taratibu tunaye 2lia
 
Shinikizo la kutaka Spika ajiuzulu ktk nafasi yake limeshikiwa bango zaidi na wafuasi wa Mbowe/Chadema.

Niwazi kabisa Spika alikuwa mwiba mkali sana kwa ktk kusimamia sheria na kanuni za mbunge na haswa kwa wapinzani ambao walitaka kuleta mchezo.

Sasa leo hii hatuwezi kushangaa kuona genge la Mbowe likishangilia na kupiga mayowe eti Spika ajiuzulu.

Kamwe wana CCM Makini wasikubali kuingia ktk mtego huuu.

Inatosha na Inatosha sana kwa kitendo cha kiungwana alicho kifanya Spika cha kuomba radhi.

Kamwe tusikubali kuendelea kumdhalalisha Spika wetu aliye fanya kazi kwa umahiri mkubwa na kuisaidia nchi yetu.

Ni vyema wana CCM wakawa makini ktk kipindi hiki cha upepo mbaya, wapaswa kuwa watulivu na nidhamu ya hali ya juu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Kazi iendeleee kama kawaida.
Kibajaji, zungu, gwajima, viongozi wa uvccm wa moshi, mpwapwa, dodoma, singida ni wafuasi wa mbowe/chadema?
 
Hili haliachi alama nzuri kwa Taifa letu! Hata Ndugai awe amekosea kiasi gani lakini ipo mbegu mbaya sana imepandwa ambayo toka uhuru haijawahi kutokea!

Tuna safari ndefu sana na kutokubaliana na Ndugai kwenye mengi hakufanyi nipuuze namna alivyoshughulikiwa pamoja na nafasi yake.
 
Sheria inasema spika anapaswa kujiuzulu mbele ya bunge sasa imekuaje hapa? Afu mbona barua ni kavu
 
Back
Top Bottom