Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Things fall apart
IMG_20210818_212439_263.jpg
 
Hili haliachi alama nzuri kwa Taifa letu! Hata Ndugai awe amekosea kiasi gani lakini ipo mbegu mbaya sana imepandwa ambayo toka uhuru haijawahi kutokea!

Tuna safari ndefu sana na kutokubaliana na Ndugai kwenye mengi hakufanyi nipuuze namna alivyoshughulikiwa pamoja na nafasi yake.
Ujumbe wa Ndugai utaishi nao hadi 2025
 
Kosa la ndugai liko wapi kwa mjibu wa sheria? Je, ndugai kavunja katiba katika kutoa maoni yake...!

Kosa la ndugai, linapaswa liwe la kichama na si kama anavyosakamwa aachie ngazi!

Kwa katiba ipi na sheria ipi inayodai sipika akitoa maoni yake kuhusu jambo la kiserikali atawajibika/wajibishwa?

Chama ndicho chaweza kumwajibisha ikiwa ziko taratibu za aina hiyo ila si kwa kumvua madaraka ya usipika!

Ngoja litokee hili, Tutajiona mapanzi mbele ya dunia kwa jinsi itavyoonyesha katiba yetu isivyiheshimiwa na kujitoshereza!

Sasa nimeelewa kwamba, Tz katiba yetu ni mbovu kuliko chochote!

Kwa nchi zenye watu wenye kupima ukweli wa jambo kupitia katiba walizonazo, Kusingeeleweka ikiwa sipika anashinikizwa kuachia ngazi kwa jambo ambalo halipo kikatiba

Mh Sipika ni mkuu wa mhimili unaojitegemea, lkn pia ni RAIA wa Tz mwenye Uhuru wa kutoa maoni yake katika jambo lolote lile huku akizingatia sheria za nchi

Niko na Ndugai na hana kosa kisheria na kikatiba
 
Bora kaondoka mnafiki mkubwa Ndugai Ndumila kuwili asiye na haya


wote mliokuwa mkimpigia Magufuli vigelegele na baada ya kufa mkaanza kumponda hadharani achieni ngazi wapuuzi nyie

Mwacheni mana Samia aunde timu yake isiyobeba MI ndumila kuwili kama huyo Ndugai
 
Shinikizo la kutaka Spika ajiuzulu ktk nafasi yake limeshikiwa bango zaidi na wafuasi wa Mbowe/Chadema.

Niwazi kabisa Spika alikuwa mwiba mkali sana kwa ktk kusimamia sheria na kanuni za mbunge na haswa kwa wapinzani ambao walitaka kuleta mchezo.

Sasa leo hii hatuwezi kushangaa kuona genge la Mbowe likishangilia na kupiga mayowe eti Spika ajiuzulu.

Kamwe wana CCM Makini wasikubali kuingia ktk mtego huuu.

Inatosha na Inatosha sana kwa kitendo cha kiungwana alicho kifanya Spika cha kuomba radhi.

Kamwe tusikubali kuendelea kumdhalalisha Spika wetu aliye fanya kazi kwa umahiri mkubwa na kuisaidia nchi yetu.

Ni vyema wana CCM wakawa makini ktk kipindi hiki cha upepo mbaya, wapaswa kuwa watulivu na nidhamu ya hali ya juu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Kazi iendeleee kama kawaida.
Wewe kweli kilaza wakati UVCCM na wabunge wa CCM ndo wameshupalia hili swala kumlinda mwenyekiti wao eboo
 
Sisi Team Magu Tumepokea taarifa hii kwa masikitiko makubwa
Sisi team magu atumtaki huyo zuzu alikuwa anazuia wasema kweli hadi mambo yalipo mkuta yeye tusiyo yajua ndiyo anajidai kumkosoa mama
 
Hili haliachi alama nzuri kwa Taifa letu! Hata Ndugai awe amekosea kiasi gani lakini ipo mbegu mbaya sana imepandwa ambayo toka uhuru haijawahi kutokea!

Tuna safari ndefu sana na kutokubaliana na Ndugai kwenye mengi hakufanyi nipuuze namna alivyoshughulikiwa pamoja na nafasi yake.
Hivi kuna mbegu mbaya iliyopandwa nchi hii kama utawala wa magufuli? Muwe mnatumia vichwa vyenu vizuri

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwa kile kichambo cha kizanzibari hata ningekuwa mimi ndo mgogo ningejiuzulu tu
 
Mode, mimi ni Tomaso, this letter doesn't look real! is this bonafide genuine?. Headed paper gani hii haina address?.
Hiyo barua ya kujiuzulu ikowapi?.
please do the needful.
P
Mzigo ni wenyewe mkuu.
 
Inakuwaje wanajamvi!

Nikiwakilisha vijana wote wa JF kutoka Arusha na kanda ya kaskazini kwa jumla. Tunatoa amri Job Ndugai ajiuzulu mara moja nyadhifa zake zote za uspika na ubunge.

Kaliletea taifa aibu na kuidharau serikali ya mama Samia ya awamu ya 6. Pia msamaha alioomba haukuturidhisha ulikuwa wa kinafiki.

Ajiuzulu mara moja bila kupoteza muda ili angalau ailinde heshima yake ndogo iliyosalia.
Sasa akibaki mbunge ataweza kuwa anauliza maswali au atapiga kimya tu.
 
Back
Top Bottom